Uchunguzi Makini Juu ya Ukristo

Author(s): 

Mwandishi wa kijitabu hiki ame fafanua vizuri kuwa mizizi ya imani ya Ukristo hailingani na mafundisho hasa ya Yesu.
Licha ya kuwa mfuasi mzuri wa madhehebu yake ya kiprotestanti, alijikuta ana maswali mengi kuhusiana na misingi halisi ya imani.
Na hilo ndilo lilimpeleka kufanya utafiti wa kina hadi amefikia uamuzi wa kubadilisha dini na kuwa mwislamu- dini lililojibu maswali yake yote.
Msomaji atafaidika kwa ksoma kitabu hiki.

Get PDF Get EPUB Get MOBI
Translator(s): 
Miscellaneous information: 
Uchunguzi Makini Juu ya Ukristo Tafsiri ya kitabu kiitwacho A Closer Look at Christianity Kimeandikwa na Barbara Brown Kimetafsiriwa na Aziz Hamza Njozi Kimetolewa na Tanzania Ithna Ashariyah Community (T.I.C.) S.L.P. 2736 Dodoma - Tanzania

Dibaji

Wengi wetu tunaridhika kuishi tu bila udadisi na tunayakubali mambo "kama yalivyo"; tunayapuuza na kuyadharau maswali madogo madogo yanayohitaji kujibiwa na yanayoleta mashaka katika akili zetu, hasa masuala yanayohusiana na dini. Kwa kufanya hivi, ndiyo ni kweli kwamba tunayopuuza, lakini kamwe hatupati utulivu wa akili na amani ndani ya nafsi zetu, kwa sababu daima nafsi zetu zinataka kuujua ukweli na sio kuupuuzia.

Wengine miongoni mwetu, hata hivyo, haturidhiki kuyachukua mambo kama yalivyo na hivyo kwa bidii na shauku tunafanya jitihada kuyatafutia majibu sahihi maswali yanayojitokeza katika maisha yetu. Tunahoji imani za baba zetu, hatupo tayari kuzikubali na kuzifuata kibubusa bila hoja na dalili za kutosha. Barabara hii haipitiki kwa urahisi kwa namna yoyote, lakini kwa mwenye bidii ya kutosha, malipo yake ni kuona ukweli, yakini, na utulivu wa akili.

Nimelelewa katika familia ya kikristo na nikakua katika madhehebu ya kiprotestanti yakieleweka kama "Imani ya kikristo iliyofanyiwa marekebisho." Licha ya ufuasi wangu mzuri wa dini - uhudumu wa kanisa mara mbili kila Jumapili na siku za mapumziko, darasa la (mafunzo ya) Jumapili, madarasa juu ya mafunzo, misingi na imani ya kanisa, shule za Biblia katika msimu wa kiangazi na kambi maalum juu ya Biblia - bado nilijikuta na maswali mengi kuhusiana na misingi halisi ya imani ambayo hakuna yeyote wala taasisi yoyote ya kidini ambayo ingeweza kuyajibu. Kwa miaka thelathini na saba nilitangatanga ndani ya ukungu wa utata kuhusiana na Mwenyezi Mungu na njia na namna sahihi ya kutoa heshima na utii wangu kwake mpaka mwaka 1991, nilipoupata Uislamu.

Mgogoro wa "Kimbunga cha Jangwani" katika Mashariki ya kati ulikuwa umefikia kilele chake, ubavuni mwa vitabu juu ya mbinu na silaha za kivita katika duka la vitabu mjini petu kulikuwa kitabu kidogo kilichoandikwa juu yake "Understanding Islam" (Kuuelewa Uislamu). Nilikifunua, nikiwa na hamu ya kutaka kujua juu ya dini hii "ya ajabu" ya Mashariki ya kati kama wenzangu wengi walivyokuwa wakitaka kujua juu ya dini hili. Udadisi wangu ghafla ulibadilika na kuwa mshangao, baada ya kusoma kurasa za kitabu hiki, nilikuta Uislamu umetoa majibu kwa maswali yangu yaliyokuwa yakinitatiza kwa miaka yote hii - sikupoteza muda zaidi, nikawa Muislamu. Baada ya muda mrefu sasa nikawa nimefikia na kupata nilichokuwa nikikitaka, kupata utulivu katika nafsi yangu juu ya uhusiano wangu na Mwenyezi Mungu.

Maadam Mwenyezi Mungu amenipa uwezo wa kujieleza vizuri katika karatasi, ninataka kuwafikia wale wote wenye maswali yanayowasumbua katika akili zao kuhusiana na dini, na nina matumaini kuwa huenda nikawasaidia kufikia majibu ya maswali hayo. Maelezo nitakayoyaeleza katika kitabu hiki yanaweza kuwashangaza na hata kuwashtua baadhi ya wasomaji, lakini kazi ya kutafuta ukweli daima huwa sio rahisi, hususan mbele ya imani zilizoaminiwa kwa muda mrefu na kanuni zake.

Nilianza kazi yangu siku nyingi kidogo kwa kuandika vijitabu vingi vidogo vidogo:

1) Tatu katika moja (three in one) uchambuzi wa imani ya Kikristo juu ya Utatu Mtakatifu kilichotolewa mwanzoni mwa 1993 na Shule Huria ya Chicago (The Open School of Chicago).

2) Kijitabu kiitwacho "A Closer Look at Christianity" (Uchunguzi makini juu ya ukristo) ambacho kinahusiana na uchunguzi juu ya ukristo kwa mujibu wa Biblia.

3) Kitabu kiitwacho "A Case of Corruption" (Suala la Maovu) ambacho kinahusiana na uongezaji na upunguzaji wa baadhi ya mambo katika Biblia.

Kitabu ulichonacho mikononi ni mkusanyiko wa vitabu vyote hapo juu, pamoja na utafiti zaidi nilioendelea kuufanya katika vitabu vyangu vya awali na vile vya mwisho kwa ajili ya wasomaji binafsi. Ni matarajio yangu kwamba, katika kurasa zinazofuatia, wasomaji watakuwa na nafasi ya kuona na kuelewa mtazamo wa ukristo kama mimi nilivyouelewa.

Barbara A. Brown
23 March 1993

Utangulizi

Uchunguzi wa karibu, katika dini mbili kati ya hizi - Uyahudi na Uislamu - utaonyesha hili kuwa ni kweli: Wote Wayahudi na Waislamu wanamuabudu Mungu mmoja, Muumba wa Mbingu na Ardhi.

Hii dini nyingine, Ukristo, ina mushkeli kidogo, hususan wakati tunapoelezea maana ya imani ya kumuamini Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika tofauti na inavyoaminiwa na Ukristo.

Badala ya kumfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu awe ndio kiini na msingi mkuu wa imani yao, Wakristo wamebadilisha muelekeo wao na kumfanya Yesu, anayeeleweka kwao kama "Yesu kristo" au "Yesu Aliyepakwa mafuta" kuwa ndio msingi mkuu wa imani. Kwa Wayahudi Yesu alikuwa "Kijana mzuri wa kiyahudi". Kwa Waislamu Yesu alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu lakini alikuwa binadamu; mmoja wa wajumbe wateule wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa Wakristo, hata hivyo, Yesu ni zaidi ya hayo.

Ukristo, kiini chake kikuu ni Yesu Kristo. Dini hii imepata jina lake kutokana na jina la Yesu Kristo. Misingi na imani zote muhimu za kikristo kiini chake ni Yesu kristo. Sikukuu kubwa za Kikristo huwa ni kumbukumbu ya matukio katika maisha ya Yesu Kristo. Alama ya imani ya Kikristo, msalaba, ni alama ya Yesu Kristo. Sala na dua za Wakristo huelekezwa kwa Yesu Kristo, kwa vile wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwenyewe huwa hawezi kuombwa na binadamu wa kawaida.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Kikristo Fritz Ridenour: "Msingi wa Ukristo ni kwamba Yesu Kristo hasa ndiye sababu ya kuwepo Ukristo na kwamba yeye ndiye anayeushikilia na kuumiliki".1

Wakristo wengi leo wanashindwa kuelewa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu bila ya Yesu kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu badala yao. Bwana Ridenour anasema kwamba Ukristo ni: "....Uhusiano na mwanadamu, Yesu Kristo".2 Na Wakristo wengi sana wana imani hii, hawamwelewi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kwa kupitia kwa Yesu Kristo.

Wakristo wanasema mwabudu Mwenyezi Mungu, lakini Yesu pia picha yake iwepo akilini. Kwa jinsi wanavyomuona - kwa nyongeza ya Mwenyezi Mungu, kama Mungu halisi, Ukristo ni dini yenye miungu wawili, sio mmoja, na dini yenye Mungu zaidi ya mmoja sio dini inayompwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na mshirika.

Hali hii ilikujaje? Ilikuwaje dini ya Ukristo imbadilishe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni binadamu) na kumfanya yeye Mwenyewe (Yesu kristo) kuwa Mungu?

  • 1. How To Be A Christian In An Unchristian World, p. 176 (Jinsi ya kuwa Mkristo katika ulimwengu usiokuwa wa kikristo, uk. 176).
  • 2. Ibid, p. 14. (Kitabu hicho hapo juu = Ibid, uk. 14).

Agano Lililovunjika

Akiwa amechoshwa na ibada ya masanamu miongoni mwa watu wake, Nabii Ibrahim aliiacha nchi yake karibu miaka 2000 kabla ya Yesu ili apate uhuru wa kumuabudu Mwenyezi Mungu mmoja.

Ilikuwa vigumu kwake kuiacha nyuma familia yake. Hivyo Mwenyezi Mungu alimbariki kwa kumpa watoto wawili wa kiume. Kisha akamfariji Nabii Ibrahim kwa kumwambia kuwa mtoto wake mdogo, Is-haq atafanya naye Agano la Milele. Is-haq akazaliwa katika nchi ya Kiyahudi ya watu "Wateule" wa Mungu. (Baadaye tunaona ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa mtoto mwingine wa Nabii Ibrahim, Ismail).

Licha ya heshima na utukufu huu wa kuitwa "watu wateule" wa Mungu, Wayahudi waliendelea bila kuacha kurudia ibada ya masanamu na Mwenyezi Mungu aliendelea kupeleka Mitume mmoja baada ya mwingine ili kuwaonya Wayahudi juu ya kutoridhishwa Kwake na tabia yao. Baada ya maonyo kushindwa kuibadilisha tabia yao, nchi jirani zilizokuwa maadui ziliingia na kuwapiga vibaya Wayahudi.

Ingawa Mwenyezi Mungu aliwakubalia muda wa amani na nafuu mara nyingi aliposikia kilio chao cha kutaka rehema yake, lakini sasa hivi, hasira Yake ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba mnamo mwaka 581 kabla kuja Yesu, kwa sababu ya kiburi na jeuri yao iliyoendelea, Aliruhusu Wababiloni kuwafagia Wayahudi wote wa Ufalme wa Yuda Kusini, ambako Mfalme Nebuchadnezzar na jeshi lake waliosonga mbele na kuupiga vibaya mji wa Jerusalem na wakawachukua Wayahudi kama mateka.

Upande wa Juu wa Ufalme wa Kiyahudi wa Israel ulipatwa na balaa kama hili mwaka 721 kabla ya Yesu katika mikono ya Waassyria.

Wakiwa wametawanywa na jumba lao la ibada kuharibiwa vibaya, Wayahudi waliamua kuanza kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu. Hata hivyo imani ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu mmoja asiye na mshirika ilikuwa imepotea kabisa, badala yake kulikuwa mvurugiko uliokuwa ukiongezeka siku hadi siku wa mambo waliyoyaongeza wenyewe na mengine kuyapunguza katika vitendo vyao vya ibada.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa ulimwenguni katika kipindi ambacho Yesu alipokea wito kutoka Mwenyezi Mungu wa kumtaka aje kama Mtume kwa Wayahudi.

Kazi Na Ujumbe Wa Yesu

"Maana Mwana wa Mtu alikuja kuwaokoa wale waliopotea". (Mathayo18:11)

"Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo". (Mathayo 15:24)

Yesu pia aliweka wazi ni nini Mwenyezi Mungu alimtaka afanye:

"Mimi sikunena kwa mamlaka yangu mimi mwenyewe, ila Baba aliyenituma ndiye aliyeniamuru niseme nini na niongee nini". (Yoshua12:49)

"Msidhani ya kuwa nimekuja kutengua sheria ya Musa au mafundisho ya Manabii, sikuja kutengua bali kukamilisha". (Mathayo 5:17)

Uchunguzi makini wa maneno ya Yesu unaonyesha kwamba, kinyume na Wakristo wanavyo fikiri, Yesu hakuwa na nia ya kuanzisha dini mpya; alikuja tu kuukamilisha na kuusisitizia ujumbe ambao Mwenyezi Mungu aliwapa Mitume wote waliotangulia kabla yake: kuwa Mwanadamu alitakiwa atii sheria za Mwenyezi Mungu na amuabudu Mwenyezi Mungu tu.

Hakuna wakati wowote katika kazi na maisha yake ya utume ambapo Yesu alidai kuwa zaidi ya mwanaadamu, aliyepewa ufunuo na kuongozwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Bila chembe ya shaka yeye mwenyewe alijiita kuwa ni mwana wa mtu, na akaweka wazi, katika aya nyingi ndani ya injili, kwamba yeye hakuwa lolote isipokuwa ni Mjumbe na Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu.

"Yesu akamjibu, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mwenyezi Mungu peke yake". (Marko 10:18)

".. anayenipokea mimi, hanipokei mimi bali anampokea Yule aliyenituma". (Marko 9:37)

"Na uzima wa milele ndio huu, kukujua wewe uliye peke yako, Mungu wa kweli na kumjua Yesu kristo uliyemtuma". (Yohana 17:3)

"Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu, ninyi mwataka kuniua". (Yohana 8:40)

"Nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu". (Yohana20 :17)

Licha ya juhudi zake zote - maneno ya ajabu pamoja na miujiza mingi - Yesu alikataliwa, hususan na watu wake.

Miaka mitatu baada ya kuanza kazi yake ya utume, alikamatwa na kuhukumiwa kwa shutuma kwamba anasambaza maneno ya chuki miongoni mwa watu dhidi ya watawala na maneno mabaya dhidi ya vitu vyao vitukufu vya kidini. Mafanikio yalikuwa yamemkwepa - katika mwisho wa maisha yake hapa duniani, alikuwa amepata wafuasi kidogo sana wasiozidi 500.

Hali hii ilibadilika baadaye baada ya kuja nabii mpya, aliyedai kuzungumza kwa jina la Yesu, miaka michache baadaye.

Mwanzilishi Halisi Wa Ukristo - Paulo Wa Tarsus

Mmoja wa wanafunzi hawa wa Yesu (Wanazareti) aliyeitwa Stephano alielekeza mahubiri yake mbele zaidi ambapo alitoa mahubiri makali kukemea maovu mbele ya Mahakimu wa kiyahudi walioeleweka kama Sanhedrin. Wakifoka kwa hasira kwa sababu ya maneno yake ya "kishetani", mahakimu waliruka na kumkamata, kisha wakampeleka nje ya mji ambako walimpiga mawe mpaka kufa. Kisa hiki kinapatikana katika "Matendo ya Mitume", sura ya 7, katika Biblia.

Mauaji ya Stephano yalishuhudiwa na kijana mdogo wa kiyahudi aliyeitwa Saulo (Paulo). Paulo alizaliwa katika mji wa Tarsus, si muda mrefu sana baada ya Yesu. Saulo (Paulo) alikuwa amejiunga na moja ya madhehebu ya kiyahudi "Pharisees". Hawa Wapharisees waliojipa mamlaka na kujihalalishia kuwaua wanafunzi wa Yesu (Wanazareti), sasa hivi walikuwa na nia kubwa ya kuendelea kuwakamata na kuwaua wanafunzi wa Yesu. Kufuatia mauaji dhidi ya Stephano, Paulo mwenyewe alichukua na kufanya kazi muhimu katika kuendeleza mauaji haya dhidi ya wanafunzi wa Yesu.

Utendaji kazi wake katika kuendeleza mauaji haya ulikuwa mzuri mno kiasi kwamba alifanywa kuwa ni ajenti mkuu wa harakati hizi katika mji wa Jerusalem, na alipewa kumbukumbu muhimu ili kuendeleza safisha safisha hii katika miji ya jirani.

Ni takriban miaka ishirini na tano tangu kupaa kwa Yesu mbinguni, ambapo huyu muuaji na mpinzani mkubwa wa Yesu na wafuasi wake alipokuwa njiani kuelekea Damascus kwenda kuwasaka wafuasi wa Yesu ambapo aliona katika ndoto anayodai kuwa alimuona Yesu, aliyemuuliza kuwa kwa nini alikuwa anataka kumuua (Yesu) kwa kuwatesa watu wake (Yesu).

Maelezo mengi yametolewa kuonyesha nini kilimtokea Saulo siku hiyo. Kama vile ugonjwa unaotokana na kupigwa na miale ya jua kwa muda mrefu hasa kichwani, mawenge na hata kifafa. Lakini hakuna lenye yakini tukiachilia kwamba maelezo yote haya yanakusudiwa kumbadilisha muuaji wa wanafunzi na wafuasi wa Yesu na adui mkubwa wa ujumbe wa Yesu, na kuwa mhubiri mzuri wa Yesu asiyekuwa na mfano wake.
Saulo alibadilisha jina lake na kuwa Paulo na akaenda katika jangwa la Arabuni ili kutafakari ni jinsi gani angetekeleza amri aliyoamini kuwa imetoka kwa Yesu ya kwenda kuhubiri.
Nini hasa angefanya ilikuwa ni kitendawili kwake, hata hivyo, maadamu wayahudi walikuwa wamemkataa Yesu na ujumbe wake, Paulo hakuona uwezekano wa kuwashawishi kwa mahubiri na kuwapata. Baada ya kutafakari akaona itakuwa ni vizuri zaidi aache kushughulika na wayahudi na badala yake aeleze jitihada zake kwa wasio kuwa wayahudi (Gentiles). Ili kufanikisha hili busara na akili nyingi vilitakiwa kutumika.

Warumi na Wagiriki ambao hawakuwa Wayahudi ndio hasa Paulo aliowalenga kuelekeza mahubiri yake. Hawa walikuwa wapagani waliokuwa wakiabudu miungu wa kike na miungu wa kiume na iliyokuwa mingi sana. Majumba ya ibada za masanamu na masanamu yenyewe yalienea kwa wingi nchi nzima, na sheria ya kirumi iliwataka watu wote, isipokuwa Wayahudi, kusujudia na kutoa heshima kwa miungu hii ya kisanamu.

Paulo alielewa kwamba watu waliokuwa na imani ya kipagani iliyowakolea kiasi hicho wasingeweza kukubali kwamba neema ya Mungu na uokovu vingeletwa na mtu tu aliyeaminiwa kuwa muongofu na mtenda haki. Ili kupata mafanikio ya haraka katika kazi yake Paulo alielewa wazi kwamba alilazimika "kulegeza" mambo kidogo, akizingatia utamaduni wa Warumi na Wagiriki (Watu wa Mataifa).

Paul Maier, katika kitabu chake "Wakristo wa Mwanzo" (First Christians), anatuambia kwamba ilipita miaka kumi na tatu tanguwakati Paulo "alipopokea wito kutoka kwa Yesu" mpaka alipoanza kuhubiri. Katika hiyo miaka kumi na tatu, Paulo kwa kutumia ujanja na ubunifu wake wa hali ya juu alijifunza mambo mengi kuhusiana na mila na desturi za Warumi na Wagiriki, ambapo hatimaye alirudi Damaskas akiwa amejipatia silaha muhimu kwa kutambua kwamba Warumi na Wagiriki wangedai na kuhitaji Mungu ambaye wangeweza kumuona na kumshika katika hii dini yao mpya, na alikuwa tayari kuwakubalia hili pindi wakihitaji.

Paulo alifanikiwa sana katika kazi yake hii na aliweza kuwapata Warumi na Wagiriki wengi mno. Japokuwa dini ya ukristo inachukua jina lake kutoka kwa Yesu kristo, Paulo mkazi wa Tarsus lazima atambulike na kueleweka kuwa ndiye mwanzilishi halisi wa Kristo, kwa vile yeye ndiye aliyebuni na kutunga misingi muhimu na imani za kikristo, na akajenga na kuimarisha Makanisa katika ulimwengu wote wa zama zake. Wakristo hawalikatai hili:

"Hakuna mtu yeyote katika historia ya ukristo mwenye athari kubwa na umaarufu kama Saulo mkazi wa Tarsus".1

Katika kitabu "The 100" (Watu 100) chenye orodha ya watu wenye athari kubwa ulimwengu na maarufu kuliko wote mia moja mwandishi wa kitabu hicho Michael Hart anasema:

"Hakuna mtu mwingine aliyefanya kazi kubwa ya kueneza ukristo kama Paulo." 2

Kuna tatizo moja kuhusiana na jambo hili, kwamba mafundisho ya Paulo, mwanzilishi halisi wa ukristo, hayawiani na hayawezi kupatikana katika mafundisho ya Yesu wala katika mafundisho ya Mitume waliotangulia kabla yake.
Si hivyo tu, bali Paulo alionana mara chache sana na wanafunzi wa Yesu ambao wangeweza kumuongoza na kumuweka sawa, hawakukubaliana na mafundisho ya upotoshaji ya Paulo, na Paulo alilielewa hili. Hatimaye hata hivyo, Paulo alifanikiwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kushawishi watu, mbali na ukweli kwamba yeye na wafuasi wake waliwazidi sana wanafunzi wa Yesu kwa nyadhifa zao kijamii, utajiri na elimu, aliweza kupata idadi kubwa ya wafuasi wa Kirumi na Kigiriki. Mafundisho ya Yesu yaliyokusudiwa kwa Wayahudi yaliyokuwa yakifundishwa na wanafunzi wake hayakuweza kufurukuta tena mbele ya mafundisho ya Paulo.

Hebu tujaribu kufanya uchunguzi wa makini juu ya uzushi ambao Paulo aliuingiza katika dini "yake" ya Ukristo.

  • 1. Islam Revealed, p. 129 (Uislamu wawekwa wazi, uk. 129).
  • 2. The 100: A Ranking of the Most Influential Persons In History, p. 62 (Maarufu 100. Mtiririko wa watu wenye Athari kubwa kuliko wote katika Historia, uk. 62.)

Misingi Na Imani Za Ukristo

Tukizungumza kwa haraka haraka, msingi na imani ya Uungu inasema kwamba Yesu ni mwana Mungu - Neno la Mungu lililofanywa mwili.

Hata hivyo, kama tulivyoona hapo nyuma, Yesu mwenyewe hakuwahi kudai kuwa yeye ni Mungu, Paulo alimpa sifa hii kwa sababu moja kubwa: alitaka kupata wafuasi wengi miongoni mwa Warumi na Wagiriki (watu wa mataifa).

Wajentaili (Wagiriki na Warumi) walikuwa ni wapagani waliokuwa wakiabudu miungu wengi wenye historia ndefu iliyojaa imani za ajabu ajabu zisizokuwa na hoja wala dalili za kiakili. Miungu wengi wa kipagani wa wakati ule - Mithrus, Adonis, Attis na Osiris, hawa wakiwa ni baadhi tu - wote walikuwa ni watoto wa mungu mkuu anayetawala, na kila mmoja wa watoto hawa wa mungu (ambao nao ni miungu) alikufa kwa ajali mbaya katika utoto wake, kisha akaja muda mchache baadaye ili kuokoa maisha ya watu wake.

Paulo alilizingatia hili, akawapa wapagani jambo linalofanana na hilo katika Ukristo, akamfanya Yesu kuwa Mungu, kwa kudai kuwa alikuwa mtoto wa Mungu (Mkuu) na kwamba, yeye pia alikufa kwa ajili ya dhambi zao. Kwa kufanya hivyo Paulo aliyapatanisha (aliyafananisha) mafundisho ya Yesu na imani za kipagani ili kuufanya Ukristo ukubalike zaidi kwa watu wa mataifa (Warumi na Wagiriki).

Ilivyo hasa, Paulo hakutangaza wazi kwamba msingi na imani hii ya Mungu imetokana na upagani. Ni yule tu anayejaribu kuichimba historia - watu na utamaduni wao - ndio ataweza kuuona ukweli huu. Paulo alithibitisha imani na msingi huu wa Uungu kwa namna nyingine. Paulo alihisi kuna sababu kama tano zinazomfanya Yesu awe Mungu.

1) Yesu alizaliwa na mwanamke bikira bila ya "msaada" wa baba wa kibinadamu

Kulijibu hili, tunaweza kuangalia mfano wa Adam, mwanadamu wa kwanza. Aliumbwa bila ya baba wala mama lakini hatumfikirii kuwa yeye ni Mungu.

2) Yesu alifanya miujiza

Kuliangalia hili tunaweza kuangalia mfano wa Nabii Musa na Nabii Elisha, wote walifanya miujiza mikubwa mikubwa, lakini hakuna yeyote kati ya hawa anayefikiriwa kuwa ni Mungu. Ukweli kwamba Yesu alifanya miujiza sio ushahidi kwamba Yesu alikuwa Mungu, na wakati miujiza hii ilipotokea, ilitokea kwa uwezo na ridhaa ya Mwenyezi Mungu sio kwa uwezo wake Yesu mwenyewe.

Miujiza yake ilifanyika kwa kusudio lile lile kama la Mitume waliotangulia kabla yake nalo ni kuuthibitisha ukweli wa ujumbe na utume wake kwa watu waliokuwa wagumu kuamini.

3) Yesu alikuwa na tabia njema "isiyofikiwa na yeyote"

Kujibu hili tunaweza kuonyesha baadhi ya mifano katika injili - kama vile kumwita Petro "Shetani" katika Mathayo 16:33, na kuwaita wengine "nyoka na kizazi cha nyoka wenye sumu" katika Mathayo 23:33, na katika Mathayo 5:22 tunaambiwa kuwa "anayemwita mwenzake pumbavu" anastahili kuingia moto wa Jahanam. Hivyo tukiangalia maneno aliyomwambia Petro kuwa ni shetani na kwamba wengine ni nyoka wenye sumu inaleta mashaka juu ya sifa hii kwamba Yesu alikuwa na tabia njema isiyoweza kufikiwa na yeyote.

4) Yesu alifufuka kutoka katika mauti

Ni kweli, "kuyashinda mauti" ni muujiza, lakini vipi kuhusu Nabii Eliya ambaye hakufa kabisa, lakini alichukuliwa kwenda mbinguni moja kwa moja kwa kutumia troli yenye matairi mawili iliyokuwa kama moto (Wafalme wa pili 2:11)? Ni muujiza mkubwa kabisa, lakini bado hatumchukulii yeye kuwa ni Mungu. Na mwisho, Wakristo wanasema kwamba:

5) Yesu alitabiriwa katika Agano la Kale

Wakristo hufanya haraka kusoma Isaya 53 kama utabiri wa kuja kwa Yesu na ujumbe wake kwa wanaadam. Tatizo hapa ni kwamba halikutajwa jina halisi katika sura hii. Bila kutaja jina kamili, nani anaweza kuelewa ni Nani hasa anayetabiriwa katika sura hii.

Neno "Mwana wa Mungu"

Neno "Mwana wa Mungu" hali kuwa neno jipya au geni, lilitumika katika Agano la Kale kumaanisha Daudi (Zaburi 2:7), pia lilitumika katika mambo ya Nyakati wa Kwanza 22:10 kuwa Nabii Suleiman (Solomon) ni mwana wa mungu, na Nabii Adam ameitwa mwana wa Mungu katika Luka 3:38 katika agano jipya.

Katika hotuba yake maarufu kule Mlimani ambayo imeelezewa kwa urefu katika Mathayo 5, Yesu anawaambia wasikilizaji wake:

"Heri yao wapatanishi kwa maana wataitwa wana wa Mungu". (Mathayo 5:9)

Katika aya zote hizi neno "Mwana wa Mungu" halimaanishi maana ya kilugha - yaani baba kumzaa mtoto kabisa bali linamaanisha upendo na mapenzi ya Mungu kwa watu waongofu (wacha Mungu). "Mwana wa Mungu" ina maana ukaribu maalumu kwa Mwenyezi Mungu, na si kwamba Mwenyezi Mungu kamzaa huyo mwana. Juu ya yote kila mtu ni mwana wa Mungu kwa vile Mwenyezi Mungu ndiye Muumbaji wa uhai na kila kitu.

Neno "Masiya - Masihi"

Neno jingine linalotumika na Wakristo kuipa uzito nadharia kwamba Yesu ni Mungu ni neno Masihi (Angalia Yohana 1:41). Neno Masiya ni la kiebrania lenye maana "Mtu wa Mungu aliyepakwa mafuta " na neno "Kristo" ni tafsiri tu ya kigiriki ya neno la Kiebrania "Masiya." Masihi au kristo, Kiebrania au Kigiriki - yote yana maana moja "Mtu wa Mungu aliyepakwa mafuta".

Neno hili hata hivyo, halikutumika kwa Yesu peke yake, limetumika kwa watu wengine kabla yake pia. Katika Zaburi 2:2, limetumika kwa Nabii Daudi na katika (Isaya 45:1) neno Masihi pia limetumika kwa Koreshi.

Wayahudi waliwaita Wafalme wao "Masiya" kwa dhana kwamba Mungu aliwapaka mafuta na kuwatawaza kuwa Wafalme. Wazo zima la neno Masiya ni la kiyahudi, lililotumika kwa mkombozi wa taifa ambaye waliamini kwamba, kwa msaada wa Mungu angewaokoa kutokana na uonevu na ukandamizaji wa watu wa Mataifa. Hata hivyo neno Masihi ndani yake halikuwa na maana ya uungu.

Neno "Mwokozi"

Neno la mwisho linalotumiwa na Wakristo ni "mwokozi". Hata hivyo neno "mwokozi" halikuanza kutumika kwa Yesu. Shamu (Syria) ilipofanya vita dhidi ya ufalme wa Israel, Jehoahaz, mfalme wa wakati ule, aliomba kwa Mwenyezi Mungu kutaka msaada katika Wafalme wa pili 13:5, Mungu alimwambia:

"Bwana akawapa Israel mwokozi". (2 Wafalme13:5)

Pindi Jehoahaz mwana wa mfalme, alipochukua ufalme, alifanya kama Mungu alivyoahidi katika 2 Wafalme 13:25, Jehoahaz alikuwa mwokozi wa watu wake kwa sababu aliwashinda Wasyria (Washamu) na akairejesha miji ya kaskazini ya ufalme wa Israel. Neno "Mwokozi" halina kabisa maana ya Uungu ndani yake

Uungu wa Yesu: Utumiaji wa Tafsiri Mbaya

Mbali na majina, njia nyingine inayotumiwa na wakristo wanapojaribu kuthibitisha uungu wa Yesu ni kutafasiri vibaya baadhi ya vifungu vya aya za Biblia. Kuna vifungu viwili wanavyopenda sana kuvinukuu kwa kusudio hili:

1) Aya ya kwanza ni Yohana 10:30 ambapo Yesu anasema:

"Mimi na Baba yangu ni kitu kimoja".

Uchambuzi wa kiakili na kimantiki wa aya hii unaonyesha kwamba, Yesu anazungumza kwa jina la Mungu na sio kwamba yeye ni Mungu. Yesu na Mungu ni kitu kimoja kimadhumuni - sio kwa asili yao. Mkristo anaweza kuangalia zaidi katika Yohana 17:1-26:

"Baba saa imefika! Mtukuze mwanao ili naye akutukuze. Maana ulimpa Mwanao mamlaka juu ya watu wote ili awape uzima wa milele wote hao uliompa. Na uzima wa milele ndio huu, kukujua wewe uliye peke yako Mungu wa kweli na kumjua Yesu Kristo uliyemtuma--".

Katika dua hii ya Yesu inadhihirisha wazi kwamba yeye hakuwa Mungu bali alikuwa ni mja na Mtume wa Mungu.

Kuthibitisha wazo hili la kuwa kitu kimoja kimadhumuni (Yesu na Mungu) na si kwa asili yao. Hebu tuangalie aya kadhaa katika sura ya kumi na saba ya Yohana, aya ya kwanza ikiwa ni Yohana 17:8. Hapa Yesu anasema:

"Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa; nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako; na wanaamini kwamba wewe ulinituma".

Katika Yohana 17:11 kuna uthibitisho mwingine unaoonyesha kuwa Yesu na Mungu ni kitu kimoja kimadhumuni (Yaani kuwapa uongofu wanadamu). Yesu anasema:

"Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja".

Nukta hii ya kuwa pamoja imeelezewa zaidi katika Yohana 17:21-23.

Kwa kifupi maelezo ya Yesu yaliyo katika Yohana 10:30, hayajaribu kuthibitisha kuwa yeye ni Mungu bali yeye na Mungu ni kitu kimoja kimadhumuni, kama inavyoonekana katika aya zilizotajwa hapo awali katika Yohana 17.

2) Aya nyingine ambayo Wakristo wanapenda kuitumia ni Yohana 14:9. Ndani yake Yesu anamwambia Filipo:

"Aliyeniona mimi amemuona Baba".

Ni vizuri kwa Wakristo wanaotumia aya hii kuthibitisha uungu wa Yesu wakaangalia Yohana 5:37, ambapo Yesu anasema:

"Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nanyi hamjapata kamwe kusikia sauti Yake, wala kuuona uso wake".

Kama Mkristo atakuwa hakuridhika na aya hiyo juu basi anaweza kuangalia Agano la Kale katika kitabu cha kutoka 33:20, Mungu anamwambia Musa:

"Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi".

Ili kuielewa vizuri aya hii ya Yohana 14:9, ni lazima tuiangalie kiusanifu: Kwa vile Yesu alikuwa ameleta ujumbe wa Mungu, kumuona na kumsikiliza yeye ilikuwa ni sawa na kuwepo Mwenyezi Mungu. Yesu alikuwa anafanya mambo kwa amri ya Mwenyezi Mungu - si kwamba yeye mwenyewe alikuwa Mungu. Hii inaonekana zaidi katika Yohana 8:19, ambapo Yesu anasema:

"Kama mngenijua mimi, hata Baba pia mngemjua".

Zipo aya nyingine zaidi ambazo mkristo anaweza kuzigeukia katika jitihada zake za kumpa Yesu Uungu, lakini zote si chochote ila ni kuzielewa vibaya au kuzitafsiri vibaya kwa ajili ya kutaka kusoma au kukiona kitu fulani ambacho kiuhalisia hakipo. Katika Yohana 17:3 tunaweza kuona kuwa Yesu hakuleta ujumbe mpya; hapa anasema:
"Ili wakujue wewe Mungu wa kweli na wa pekee na wamjue Yesu Kristo uliyemtuma".

Hapa anatuambia kwamba ni lazima tumuamini Mungu mmoja tu na ambaye ni wa kweli na kwamba yeye, Yesu ni mjumbe tu aliyetumwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Je! Yesu Aliwahi Kujitangaza Kuwa Yeye ni Mungu?

Wakristo wengi, mara nyingi huonyesha rejea nyingi katika injili ya Yohana ambapo Yesu anajiita "Mwana wa Mungu". Kwa upande mwingine wanapuuzia rejea nyingi katika injili hiyo hiyo ya Yohana ambapo Yesu anajiita "Mwana wa Binadamu". Hii inaonyesha wazi kuwa neno "Mwana wa Mungu" kama linavyotumika hapa halina maana ya kilugha. Yesu alikuwa na ukaribu maalum kwa Mwenyezi Mungu - alikuwa mwana wa Mungu kama ilivyo sisi wote ni wana wa Mungu.

Katika Mathayo 16:13, Yesu anawauliza wanafunzi wake kuwa wanafikiri yeye, Yesu, ni nani? Wakristo wanalipenda zaidi jibu la Petro ambalo lipo katika Mathayo 16:16 ambapo Petro anasema "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliyehai."

La kufurahisha zaidi, katika swali hilo hilo linalopatikana katika Marko 8:16, Petro anasema "Wewe ni Kristo". Ni maneno kidogo tu yameongezeka kwenye Mathayo ikilinganishwa na Marko, lakini yanabadilisha maana yote ya maneno. Zaidi ya hilo, kuna nukta moja ambayo wakristo wanaipuuza inayopatikana katika aya chache zinazofuatia chini ya Mathayo 16. Katika aya ya 20 - pia katika Marko 8:30 - Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa wasimwambie mtu yeyote zaidi kuwa yeye ni Kristo. Kwa nini hakutaka watu wengine walijue hili?

Je! Paulo Alifanikiwa Kitu Gani?

Kwa kusema kwamba Yesu alikuwa Mungu, Paulo aliwaridhisha sana Watu wa Mataifa kwa sababu ni jambo walilokuwa wamelizoea (Katika imani yao ya kipagani kulikuwa imani kama hii) na mafanikio yake yakawa hayana kikwazo. Bidii na uwezo wake mkubwa wa kushawishi watu pamoja na kuwa kwake tayari kuchanganya ujumbe halisi wa Yesu na imani za kipagani zilimpelekea kumpachika Yesu uana wa Mungu - imani potofu kabisa, kwa sababu uana (wa Mungu) una maana (mwana) aliyeumbwa, wakati Uungu una maana "uwezo wa kuwepo milele na bila kuumbwa".

Baadaye viongozi wa kanisa waliamua kuondoa utata huu kiulaini kwa kusema kuwa Yesu alikuwa Mungu aliyevaa mwili wa kibinadamu - na ni wa milele "aliyeamua" kuwa mwanadamu katika tumbo la Bi Mariamu. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa na asili (maumbile) mbili - Umungu na ubinadamu ambavyo viliungana na kuwa mtu mmoja. Huenda hawa viongozi wa kanisa walikuwa na nia nzuri lakini katika maelezo haya wameleta utata na mkorogano zaidi.

Mtazamo wa Uislamu juu ya Yesu

Kama ilivyo katika Biblia, Qur’ an pia inasema, Yesu alizaliwa bila ya baba (mwanadamu). Hii hata hivyo haina maana kwamba Yesu alikuwa Mungu, isipokuwa inaonyesha tu kwamba Mungu aliyeweka kanuni za maumbile (Laws of Nature), kama vile mtoto kuzaliwa na wazazi wawili, baba na mama, ana uwezo vilevile wa kuzisimamisha kanuni hizi na kufanya anavyotaka.
Kama Yesu angekuwa ni Mwana wa Mungu kiuhalisi kabisa - angekuwa ni mshirika katika uungu na yeye mwenyewe angekuwa ni Mungu, na kwa msingi huu Mungu angekuwa amezaa, amezaliwa, ameishi kama binadamu na kufa. Fikra hii ni mbovu mno na haikubaliki mbele ya watu wenye kufikiri na wenye akili.

Uislamu unashikilia kwa nguvu kuwa Yesu alikuwa ni Binadamu, aliyepewa ujumbe na Mwenyezi Mungu.

"Hakuwa Isa mwana wa Mariamu isipokuwa ni Mtume tu". (Qur'an 4:117)

Msimamo na imani kwamba Yesu alikuwa Mungu ni tofauti na kinyume kabisa na imani ya kuamini umoja wa Mwenyezi Mungu - kuwa Mungu ni mmoja tu.

"Kwa kuwa Allah ni Mungu Mmoja. Utakatifu na heshima vinamstahiki yeye. Ametukuka kwa utukufu mkubwa na ameepukana kuwa na Mtoto". (Qur'an 4:171)

Nadharia, msingi au imani yenye mzizi yake kwenye ukafiri (upagani) na ambayo inakwenda kinyume na imani ya kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu mmoja tu asiyekuwa na mshirika, haina nafasi na haikubaliki kabisa katika Uislam.

3) Tatu katika mmoja (Trinity)?

Kwa haraka haraka imani ya Utatu Mtakatifu inasema kwamba Mungu mkuu ameundwa na vitu vitatu: Mungu Baba, Mungu Mwana - Yesu, na Mungu Roho Mtakatifu. Pamoja na kuamuamini Yesu, imani ya Utatu Mtakatifu ni moja ya misingi mikubwa kabisa ya Ukristo na ambayo juu yake imejengwa misingi na imani nyingine za Ukristo".1

  • 1. This Is The Catholic Church, p. 4. (Hili ni Kanisa Katoliki, uk. 4).

Imani ya Kuamini Kuwepo Kwa Mwenyezi Mungu Mmoja Asiyekuwa na Mshirika (Monotheism)

Kamusi iitwayo "Webster's New World Dictionary" imelitafsiri neno "Monotheism" kuwa ni imani kuwa kuna Mungu Mmoja tu".1 Uyahudi, Ukristo na Uislamu zote zinadai kuwa zinaamini na kufuata imani hii. Imani hii ilihimizwa sana na Nabii Musa katika kifungu katika Biblia kinachoeleweka kama "Shema" au shema ya imani ya kiyahudi:

"Sikieni, enyi Israel: Bwana Mungu wetu ni Mungu Mmoja tu" (Marko 12:29)
Alipokuja Nabii Muhammad (saww) takriban miaka 600 baada ya Yesu, alileta ujumbe huo huo:

"Na Mola wenu ni Mungu mmoja tu: hakuna Mungu mwingine isipokuwa Yeye". (Qur'an 2:163)

Ukristo umeondoka kwenye imani ya umoja (upweke) wa Mwenyezi Mungu na umepotea kwenye utata na mkorogano wa Utatu Mtakatifu: Vipi Mwenyezi Mungu anaweza kuwa mmoja wakati unamjumuisha Yesu na Roho mtakatifu?

Athari za Paulo na Walengwa (hadhira) Wake : Watu wa Mataifa (Gentiles)

Ingawa imani na msingi (doctrine) huu haukupendekezwa rasmi na Paulo, hapana shaka yoyote kwamba alikuwa na wazo hilo akilini. Na bado kama Yesu atachukuliwa kuwa ni mwana mwenye asili ya uungu basi itabidi tumtafute baba yake mwenye asili ya uungu pia. Kulikuwa pia mijadala juu ya Roho Mtakatifu, ambaye Paulo alidai kuwa ni chombo cha usafiri kilichotumika kuleta ufunuo kwa mwanaadam. Kimsingi, Paulo alitaja hivi vitu vitatu vinavyounda utatu mtakatifu yaani Mungu Baba, Yesu - Mungu mwana, na Mungu Roho Mtakatifu.
Lakini kanisa halikuvitambua rasmi mpaka karne ya nne ambapo kanisa liliitangaza rasmi imani hii ya utatu mtakatifu na kwamba Mungu Mkuu ameundwa na Utatu Mtakatifu.

Kama ilivyo kwa imani nyingine zilizobuniwa na kuanzishwa na Paulo katika Ukristo, Utatu Mtakatifu pia, chanzo na asili yake ni imani za kipagani (kikafiri). Mfumo wa ibada wa watu wa Nimrod, ulianza Babylon lakini wakati wa zama za Paulo ulikuwa umeenea sana hadi maeneo ya miji alipokuwa akiishi Paulo na watu wengi walikuwa ni wafuasi wa imani hii. Nimrod, alikuwa ni kijana mdogo aliyekuwa amemuoa mama yake.
Watu wake waliamini kuwa Nimrod alikuwa Mungu na kwamba Baal, Mungu wa jua, alikuwa ndiye baba yake. Baada ya kufa katika umri wake mdogo, mama yake Nimrod akawa mkuu wa ibada hizi za kipagani na akaanzisha imani kwamba mwanaye alikuwa anaendelea kuishi katika maumbile ya kiroho. Kwa hiyo kwa mara ya kwanza utatu mtakatifu ukawa umeibuka. Baal, Mungu Baba, Mama wa Nimrod, na Nimrod - Mungu Mwana. Ni kutokana na kisa hiki kwamba Paulo alianzisha Utatu Mtakatifu katika Ukristo.

Utatu Mtakatifu Katika Biblia

Kuna rejea mbili tu katika Biblia juu ya utatu mtakatifu, na zote zinatatanisha.

1) Rejea ya kwanza inapatikana katika Mathayo 28:19. Hapa, Yesu anawaambia Wanafunzi wake "Nendeni, mkafundishe na kuhuburi mataifa yote, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu".

Katika aya hii kuna utatanishi mkubwa:

a) Aya hii inataja nafsi tatu kila mmoja ikijitegemea ambazo baadaye ziliunganishwa na kuwa utatu mtakatifu wa Kikirsto na aya hii haizizungumzii nafsi hizi tatu kuwa ni sehemu tu ya Mungu Mkuu.

b) Tukichunguza zaidi juu ya mada hii hii - "Tume Kuu" katika Marko 16:15, Yesu anasema: "Nendeni ulimwenguni mkahubiri Injili kwa watu wote". Je, maneno ya ziada (yaliyozidi) tunayoyaona katika rejea ya Mathayo yametoka wapi?

c) Ubatizo katika zama za mwanzo wa kanisa ulifanywa kwa jina la Yesu tu, kama ilivyoaminiwa na kuidhiniwa na Paulo katika nyaraka zake mbalimbali.

2) Rejea ya pili inapatikana katika 1Yohana 5:7 ambapo imeandikwa "Kwa kuwa wapo watatu wenye kumbukumbu za mbinguni, Baba, Neno, na Roho Mtakatifu: na watatu hawa ni "Mmoja".

Japo rejea hii ipo wazi zaidi juu ya utatu matakatifu, wasomi na wanazuoni wa Biblia katika karne ya 19 walikubali ukweli kwamba maneno "Baba, Neno na Roho Mtakatifu" ni maneno ya uzushi yaliyoongezwa - na maneno haya hayamo katika Biblia za zamani. Na pia maneno haya yameondolewa katika Biblia mpya za siku hizi.

Mbali na aya hizi mbili, kinachoshangaza zaidi ni kule kukubali ukweli kwamba maneno Baba, Neno, na Yesu kristo (bila shaka na maneno mengine mengi) hayakuwepo ila yamezusha na kuongezwa ndani ya Biblia. Zaidi ya hayo Hakuna rejea nyingine Ya Aina Yoyote katika Biblia inayozungumzia Utatu Mtakatifu. Kwa kifupi dhana ya utatu katika ukristo - Mungu Baba, Yesu Mwana na Roho Mtakatifu kama Mungu Mkuu anayemuongoza mwanaadamu - haikuwahi kutolewa hata siku moja na Yesu au Mtume yeyote mwingine aliyetangulia kabla yake.
Misingi na asili ya imani hii tayari ilikuwepo katika imani ya kipagani ingawa Paulo mwenyewe ilikuwa siri yake, hakutangaza waziwazi lakini alifanya hivi ili imani ya kikristo ifanane na ya kipagani katika mambo ya msingi ili apate wafuasi wengi wa kipagani. La kusikitisha ni kwamba licha ya ukweli imani hii kwamba imeundwa na mwanadamu, Paulo, lakini kanisa liliichukua imani hii na kuifanya kuwa ni msingi mkuu wa imani ya Ukristo.

  • 1. Webster's New World Dictionary, p. 879. (Kamusi mpya ya ulimwengu ya Webster, uk. 879.)

Ukristo wa Mwanzo

Tertullian, mwanasheria na kiongozi wa kanisa katika mji wa Carthage, alikuwa ni wa kwanza kutumia neno "utatu mtakatifu" katika karne ya tatu alipotoa nadharia kwamba, Mwana na Roho Mtakatifu ni sehemu za Mungu Mkuu lakini wote ni kitu kimoja (Mungu mmoja).

Mabishano makali juu ya mada hii ya utatu mtakatifu yaliendelea kwa miaka mingi miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa kanisa. Baadhi waliafikiana na Tertullian kwamba Utatu Mtakatifu ndani yake ulikuwa na nafsi au asili tatu, lakini baadhi walidai kuwa utatu ulikuwa utatu wa ufunuo tu - kwamba Yesu alijazwa na Roho Mtakatifu wa Baba ambapo Roho huyo aliishi ndani yake (Yesu).

Mfalme Constantine alijikuta katika vita na mapigano mnamo mwaka 381 B.K, wakati mabishano juu ya utatu mtakatifu yalipokuwa makali sana baina ya viongozi wawili wakubwa wa kanisa kutoka Alexandria, Arius - afisa wa ngazi ya juu wa kanisa, anayemfuatia askofu, na Alexander, aliyekuwa askofu wake.

Mkutano wa Baraza la Nisea (NICEA)

Mfalme Constantine, japo alikuwa hajui la kufanya juu ya mambo na imani za kanisa za kibubusa lakini alikuwa na yakini kwamba umoja wa kanisa ulikuwa muhimu sana kwa ajili ya dola na ufalme wenye nguvu. Constantine alijaribu kuwapatanisha hawa viongozi wawili wa kanisa. Askofu aliposhindwa kumaliza tatizo hili, Constantine aliitisha mkutano wa baraza la Wasomi wakubwa katika masuala ya dini kwa mara ya kwanza katika historia ya kanisa lililokutana mwaka 325 B.K katika mji wa Nicea.

Maaskofu 300 walihudhuria mkutano huu; baada ya kufanya kazi kwa wiki sita, imani ya utatu mtakatifu iliundwa rasmi. Mungu wa Wakristo kuanzia siku hiyo alitambulika kuwa ana nafsi tatu - au asili tatu - katika muundo wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Imani hii mpya iliyozinduliwa rasmi na Baraza la Nicea ilieleza hivi:

"....... tunamwabudu Mungu mmoja katika utatu mtakatifu, na utatu katika umoja --- kwa vile kuna nafsi moja ya baba, nyingine ya mwana na nyingine ya roho mtakatifu ---- sio miungu watatu, isipokuwa ni Mungu mmoja - nafsi zote tatu ni sawa milele hata milele --- kwa hiyo yeyote anayetaka kuokoka (kuokolewa) ni lazima aamini imani hii ya utatu mtakatifu".1

Licha ya jitihada za Costantine, mabishano na mzozo juu ya utatu haukuisha na wala haukukaribia kuisha japo Costantine mwenyewe alikuwa na matumaini makubwa ya kumalizika kwa mgogoro huu. Arius na askofu mpya wa Alexanderia aliyeitwa Athanasius walianza mabishano hata baada ya kutiwa saini Imani ya Nicea; "Arianism" - yaani imani ya Arius - iliyokuwa kinyume na utatu mtakatifu iliharamishwa na yeyote ambaye hakuamini imani ya utatu mtakatifu alikamatwa na kufungwa.

Hakuna Ustahimilivu Tena

Mnamo mwaka 451 B.K. katika mkutano wa Baraza la Chalcedon, imani ya Nicea, Constantinopole (inayoamini Utatu Mtakatifu) ilifanywa kuwa ndiyo imani rasmi inayotambulika na yenye mamlaka. Mabishano juu ya utatu hayakuendelea kuvumiliwa hata kidogo; kuzungumza dhidi ya utatu ilionekana ni kashfa dhidi ya dini na Mungu, na adhabu yake ilikuwa ni kipigo kikali na kuharibiwa au kuondolewa baadhi ya viungo na pengine kuuliwa kabisa. Sasa Wakristo wakawageukia Wakristo, wakiwaharibu au kuondoa baadhi ya viungo vya miili yao na kuwachinja maelfu kwa melfu kwa sababu ya tofauti ya maoni.

Ingawa adhabu za kikatili za wakati ule sasa hivi hazipo, utatanishi na mabishano juu ya utatu mtakatifu unaendelea mpaka leo. Wakiwa hawajakata tamaa, bado wakristo walio wengi bado wanashikilia kwa nguvu imani hii ambayo ni msingi wa imani yao.

Utatu Mtakatifu: Inakubalika Kimantiki?

Imani ya utatu mtakatifu inaweza kuwa msingi mkuu wa imani ya Ukristo lakini haina ukweli au msingi wowote kutoka kwenye Maandiko Matakatifu - imani yote imeundwa na mwanadamu kwa asili yake. Huu ni mfano - mwingine wa kwamba ni jinsi gani imani za kipagani zilivyoingizwa kwenye ububusa wa ukristo ili kuufanya ukristo ukubalike zaidi kwa wapagani.

Wakristo walio wengi, wanapoombwa kuielezea imani hii (ya utatu), hawawezi kutoa jibu lolote isipokuwa kusema: "Ninaamini hivyo kwa sababu niliambiwa niamini hivyo". Wanalielezea kwamba "Ni siri ya Mungu - hakuna mtu anayejua" ingawa Biblia inasema katika Wakorinto wa kwanza 14:33 kwamba:
"Mungu sio mwanzilishi wa utatanishi na migongano". (Mysteries).

Hata aliyeipa nguvu na kuihimiza imani hii ya utatu aliona ugumu mkubwa katika kuielewa imani hii. Inasemekana kwamba Athanasius, askofu aliyeitwa na kuitangaza rasmi imani hii ya utatu, alikiri kwamba alivyokuwa akizidi kuandika juu ya imani hii, ndivyo uwezo wake wa kuielezea imani hii ulivyokuwa ukizidi kupungua.

  • 1. Excerpts from the Athanasian Creed.. (Nukuu kadhaa kutoka katika dhehebu la Athanasi).

Mtazamo wa Uislamu juu ya "Mungu Mmoja"

Wakati ukristo unababaika kueleza maana ya "Mungu mmoja" tatizo hilo halipo katika Uislamu:

"Wamekufuru wale wasemao - Mwenyezi Mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu - (yeye ndiye wa tatu wao). Hali hakuna Mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja (tu peke yake). (Qur'an 5:73)

Mwandishi Mmarekani wa kiislamu Suzanne Hannef ameliweka jambo hili wazi kabisa pale aliposema: "-- Mungu sio kama nanasi au chungwa linaloweza kugawanywa katika sehemu tatu zinazounda kitu kimoja kizima. Kama Mungu ni nafsi tatu au ana sehemu tatu, basi kwa vyovyote vile hawezi kuwa Mmoja, wa pekee (kwa sababu tayari zipo nafsi nyingine mbili zenye sifa ya uungu). Wala hawezi kuwa Asiyeonekana, kwa sababu tayari Yesu ambaye ni moja ya nafsi ya Mungu ameshaonekana, jambo linaloharibu sifa muhimu za Mungu Halisi Na Wa Kweli.1

Tukiliangalia suala hili kwa upande mwingine: utatu una maana Mungu ana vijisehemu vitatu vilivyo tofauti tofauti (havikuungana) - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ikiwa Mungu ni mmoja tu (kwa mujibu wa wale wanaoamini utatu mtakatifu kuwa ni Mungu mmoja) itakuwaje huyo huyo mmoja awe Baba na awe Mwana? Ina maana kuwa yeye atakuwa ni mtoto (mwana) wa yeye mwenyewe. Matumizi ya akili na mantiki hayakubaliani na utatanishi na mkorogano wa mambo kama huu.
Ukristo unadai kuwa unaamini kuwepo Mungu mmoja asiyekuwa na mshirika, lakini kwa kuwepo utatu mtakatifu unaodaiwa kuwa una nafsi tatu zote zikiwa na uwezo na sifa za uungu, hakuna shaka katika fikra za Waislamu kwamba ukristo umeshapoteza kabisa imani ya kumwabudu Mungu mmoja. Wakristo wameondoka kwenye ibada na imani ya Mwenyezi Mungu mmoja na badala yake wameingia kwenye ushirikina kwa sababu sasa hivi hawamwabudu Mwenyezi Mungu mmoja bali wana waabudu miungu watatu.

Wakristo hawazichukulii shutuma hizi kuwa ni nyepesi. Kwa upande wao wanawashutumu Waislamu kwamba hawaelewi hata maana ya utatu mtakatifu, wakidai kwamba Qur'an inauelewa utatu kuwa ni Allah. Mungu Baba, Yesu - Mungu Mwana na Bi Mariamu - mama yake Yesu - eti ndiyo maana Qur'an inaupinga utatu mtakatifu. Ambapo Kanisa katoliki lilibuni cheo cha "Mama wa Mungu" tangu mwaka 431 B.K., katika mkutano wa Baraza la Efesazi (Ephesus), uchunguzi makini wa aya za Qur'an ambazo hutumiwa zaidi na Wakristo kuthibitisha shutuma zao zinaonyesha madai kwamba Qur'an inamhesabu Bi Mariamu kuwa ni "Mmoja" wa nafsi tatu za Mungu katika utatu ni ya uongo.

Qur'an inaishutumu vikali imani ya utatu Mtakatifu (4:171), (5:73). Pia inaishutumu ibada ya kumwabudu Yesu na Mama yake Bi Mariamu (5:116). Hakuna sehemu yoyote katika Qur'an ambapo Qur'an inazikubali au kuzichambua nafsi tatu za utatu wa kikristo. Msimamo wa Qur'an ni kwamba Nani au Nini kinachounda imani hii si suala la msingi, bali imani yote ya utatu ni tusi dhidi ya upweke (umoja) wa Mwenyezi Mungu.

Hakuna sehemu yoyote katika dini inayompwekesha Mwenyezi Mungu (Uislamu) inapotajwa kumuabudu yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mmoja, na juu ya hili Qur’an ina msimamo thabiti:

"Na - - Mola wenu ni Mungu Mmoja: hakuna mungu mwingine isipokuwa yeye, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa kurehemu". (Qur'an 2:163)

"- - Mimi ni Mola wenu na Mwenye kuwaruzukuni: kwa hiyo msimuabudi yeyote asiyekuwa Mimi". (Qur'an 21:92)

Kifo Kimoja Kufuta Dhambi za Wote?

Kwa haraka haraka, imani ya kafara inaeleza kwamba Yesu alipatwa na masaibu makubwa na kufa msalabani ili kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi.

Imani ya Kuwepo kwa Dhambi ya Asili

Lau Paulo angekuwa mfanyabiashara bila shaka angejenga nyumba iliyojaa fedha, lakini alikuwa mtu mbunifu hodari na mjanja sana, hii inaweza kuonekana kwa jinsi alivyounda mfumo wenye mzunguko mrefu usiokuwa na ulazima wa imani kwa ajili ya uokovu katika Ukristo. Hii inaweza kuonekana vizuri zaidi katika Imani ya Mateso na kifo cha Yesu - Imani ambayo imani nyingine zote - ile ya uungu wa Yesu, Utatu Mtakatifu na kuokoka kwa imani peke yake zimejengwa juu yake.

Mbele ya Paulo, wanadamu wote ni waovu na wadhambi, sifa ambayo wote wameirithi kutoka kwa Adam na dhambi lake la kula tunda la mti uliokatazwa katika Bustani ya Eden. Hii "dhambi ya asili" imewatambaa na kuwaambukiza wanadamu wote tokea wakati wa Adam. Kwa sababu ya maambukizi haya ya dhambi, mwanadamu hawezi kijinusuru kutoka kwenye minyororo ya dhambi hata afanye jitihada kubwa kiasi gani. Yesu ndiye angeweza kumkomboa na kumnusuru mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi kwa kuwa yeye hakuzaliwa kutokana na mbegu ya mwanadamu.

Japokuwa kimantiki (kiakili) hii ni dhulma kwa Mwenyezi Mungu na Mwanadamu, ukristo kwa moyo mkunjufu umeichukua na kuihalalisha imani hii ya dhambi ya asili ili kuithibitisha dhana yao ya ujumbe na kazi ya Yesu, yaani kuteswa na kufa kwa ajili ya dhambi za mwanaadamu.

Alipokuwa akiunda imani hii ya dhambi ya asili yaelekea Paulo alisahau maneno ya Mungu katika Ezekiel 18:20 -22:
"- - Mtoto hatabeba dhambi za baba, wala baba hatabeba dhambi za mtoto."

  • 1. What Everyone should Know About Islam and Muslims, pp. 183-4. (Mambo yampasayo kila mmoja kuyajua juu ya Uislamu na Waislamu, uk. 183- 4).

Mwokozi Yesu: Muhanga wa Mwisho

Kwa mujibu wa Paulo, mwokozi alikuja katika sura ya Yesu: Mungu alimtuma mwanaye wa pekee duniani ili aje apate mateso na hatimaye afe msalabani ili damu itakayomwagika iwe kafara ya dhambi za wanaadamu, kwa hiyo Yesu ndiye aliyetolewa kafara (mhanga). Paulo alipata fikra hii kutokana na kafara zilizokuwa zikitolewa na Wayahudi kwa Mungu - ambapo maelezo yake yanapatikana katika agano la Kale na akahisi kwamba kafara hizi zilitolewa ili kupata msamaha wa Mungu kutokana na madhambi ya watu.

Wakati baadhi ya kafara hizi zilizotolewa na Wayahudi zilifanywa kwa ajili ya maondoleo ya dhambi, Mitume waliokuja baadaye walikataza jambo hili. Katika Hosea 6:6, kwa mfano, tunasoma:

"Kwa kuwa Ninataka upendo thabiti na sio kafara".
Mungu alitaka upendo - ambao husababisha kumwamini Yeye na utii wa sheria yake - kwani hii ni bora kuliko damu ya kafara. Hata Yesu mwenyewe aliusisitiza ujumbe huu tena, katika Mathayo 9:13, ambapo anasema:

"Nendeni na mkajifunze maana ya maneno haya: Ninataka rehema sio kafara."

Paulo aliyaweka yote haya pembeni akasema kwamba Yesu, kiumbe mkamilifu, alikuwa "Kafara (muhanga) wa mwisho" alipoyatoa maisha yake msalabani.

Nadharia ya Paulo ni kwamba Mungu hawezi kuchukuliwa kuwa ni Muadilifu mpaka amuadhibu mwenye dhambi. Toba peke yake haiwezi au haitoshi kuwa sababu "muhimu" kwa ajili ya kusamehewa madhambi yaliyofanywa. Anasema kuwa kuteswa na kufa msalabani kwa Yesu, ni muhimu sana kwa sababu heshima, haki, utukufu na uongofu wa Mungu haviwezi kukamilika kwa toba "tupu". Mkristo anaamini kwamba Yesu alisuluhisha na kupatanisha baina ya wanadamu na Mwenyezi Mungu kupitia kifo chake.

Mwandishi wa Kikristo, Anis Shorrosh alilichunguza jambo hili kwa umakini sana miaka mingi iliyopita, na akahitimisha kwamba hakuna ukweli juu ya kuteswa na kufa katika kukiri imani na toba; nani atakayechukua mzigo wa dhambi zetu? 1

Kutokana na suala zima kwamba Mwenyezi Mungu alimtaka Yesu ayatoe maisha yake kwa ajili ya dhambi za wanadamu, Paulo alimchukua Mwenyezi Mungu anayewapenda na kuwajali viumbe wake akamfanya kuwa ni katili na aliye mbali sana ambapo kitu kingine chochote kisichokuwa damu ya Yesu hakiwezi kumfikia wala kumridhisha.

Mungu wa Upendo

Fikra ya kwanza kubuniwa na Paulo na ambayo hutumika mara nyingi katika Ukristo kuhusiana naYesu ni Upendo na Mungu.

Kwa mujibu wa wakristo, upendo wa Mungu umekuwepo tu kwa sababu ya kusulubishwa na kufa kwa Yesu - alama ya upendo wa Mungu ni msalaba, kwa mujibu wa Wakristo. Kwa mujibu wa namna yao ya kufikiri, Mungu alitupenda mno hata akamtuma mwanae wa pekee ili apate mateso na hatimaye afe ili amwokoe mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi.

Je, Mungu Aweza Kufa?

Tukiendelea na dhana yenye kutatanisha kwamba Mungu wa Wakristo anaweza tu kusamehe dhambi ndogo kwa kusababisha dhambi kubwa - dhambi ya kumtoa Yesu ili auliwe - dhambi ya kuua, tunalazimika kujadili mada ya uungu ili tuweze kuijadili mada hii. Mungu ni wa milele, alikuwepo tangu na tangu na atakuwepo milele na milele: Hakuumbwa; Hawezi kufa; n.k.

Kama Yesu ni mtoto wa Mungu, kama wakristo wanavyodai, hii ingemfanya na yeye kuwa Mungu pia, ingewezekanaje yeye, kama Mungu, afe msalabani kama wanavyodai?

Ikiwa "mwili wake wa ubinadamu" ndio ulikufa, hii italeta maana kwamba alikufa kama mtu mwingine yeyote. Na kama ni hivi - imani yote ya kuwa Yesu aliteswa na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanaadamu, itakuwa haina msingi wowote - kwani damu ya mtu wa kawaida haiwezi kuwa fidia ya dhambi za mtu mwingine.

Athari za Upagani Katika Imani Ambazo Paulo Aliziingiza Katika Ukristo

Paulo hakuielewa maana halisi ya kafara zilizokuwa zikitekelezwa na Wayahudi katika Agano la Kale; waliteketeza kafara hizi kama shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutokana na rehema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu aliwajaalia - na sio kwa ajili ya kuhakikishiwa msamaha wa Mwenyezi Mungu kutokana na madhambi yao.

Karibu dini zote za kipagani zinaamini kwamba kafara wanazozitoa kwa miungu yao ni kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi yao. Mimea, wanyama na hata watu waliuawa ili kuwa na uhakika ya "rehema ya Mwenyezi Mungu".

Sio hivyo tu bali karibu wafuasi wa dini zote za kipagani huchukua vyakula hasa mikate na pombe, vinavyokuwa vimetengwa kwa ajili ya sadaka kwa miungu. Wapagani waliamini kwamba kwa kula vyakula hivi vilivyotengwa kwa ajili ya miungu, wao pia (wapagani) walikuwa wanapata baadhi ya sifa na nguvu za kimungu - roho za miungu hao ziliingia na kuishi ndani yao (hao wapagani).

Paulo alichukua imani hii akaiingiza katika Ukristo, akaiita kuwa ni "Sakramenti ya chakula cha Bwana au Ekaristi". Kwa sababu inachukuliwa kuwa ni sehemu kubwa ya imani ya kuteswa na kufa kwa Yesu. Mfumo na tendo hili la Ekaristi umekuwa ni moja wa Sakramenti muhimu kabisa katika Ukristo kwa sababu ni alama na ukumbusho wa tendo la Yesu kutoa mwili na damu yake kama kafara na fidia ya dhambi za mwanadamu.

Imani hii ambayo Paulo aliingiza katika Ukristo kutoka kwenye upagani ilimrahisishia sana kazi. Kwa hadhira yake - watu wa mataifa hawakuona taabu yeyote kuingia katika ukristo kwani imani ya Mungu kufa akiwa kijana na baadaye kuwa hai kuwaokoa watu wake ili kuwepo katika imani zao za kipagani. Ikiwa miungu wao akina Adonis au Mithran waliwahi kufanya kitu cha aina hii kwa ajili yao kwa nini Yesu ashindwe kulifanya hilo sasa hivi?

Paulo Alifanikiwa Kitu Gani?

Watu wa mataifa kwa mara nyingine tena walifarijiwa: walikuwa na waokozi katika dini zao za zamani za kipagani, na mara hii tena, Paulo aliwapa mwokozi mmoja katika imani yao mpya ya Ukristo. Aliwaambia kwamba walichokuwa wanatakiwa kukifanya ili kuwa na yakini kwamba Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao ni kuamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao, hilo tu ndilo walilotakiwa kulifanya.

Katika sheria ya Kiyahudi, mambo muhimu katika kafara au fidia kwa ajili ya madhambi ni Rehema ya Mwenyezi Mungu, toba na jitihada za dhati katika kufanya mambo ya kheri; kafara ya damu haikuhitajika. Katika jitihada zake za kuwapata watu wa mataifa, Paulo alilitafsiri upya Agano la kale na akawapa Wakristo wapya mwokozi wao - mtu ambaye huyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine.

Wakristo wa leo hawana ukaribu na upagani kama ilivyokuwa katika wakati wa Paulo. Imani yake ya kuteswa na kufa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi za wanadamu - aliyoiingiza katika ukristo, imekuwa ni tatizo kubwa kwa Wakristo kuielezea ikaeleweka, baada ya kuona jambo zima linatatanisha wakati nguvu za hoja na akili zinapojaribu kufurukuta na kutaka kutumika.

  • 1. Ibid, p. 135. (Kitabu hicho hapo juu).

Mtazamo wa Uislamu Juu ya Dhambi Ya Asili

Uislamu inaichukulia imani ya dhambi ya asili na kifo cha Yesu kama inavyoaminiwa na Wakristo kama ifuatavyo:

1) Dhana ya Dhambi ya Asili

Imani ya ukristo juu ya dhambi ya asili haina nafasi yoyote katika Uislamu, kwani Waislamu wanaamini kwamba mwanadamu huzaliwa akiwa hana dhambi yoyote. Ndani ya Qur'an, Mwenyezi Mungu anasema:

"Uelekeze uso wako katika dini iliyokuwa sawa ambayo Allah amemuumbia mwanadamu, ambayo inawiana na maumbile ya mwanaadamu". (Qur'an 30.30)

Aya hii inatueleza kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu katika umbile zuri kabisa, na akiwa ni twahir, asiyekuwa na dhambi lolote; na kwamba umbile lake lilikuwa linamwongoza kutii na kuinyenyekea sheria ya Mwenyezi Mungu.1 Dhambi hairithiwi: ni kitu ambacho mwanaadamu hujiletea mwenyewe anapofanya jambo ambalo hakutakiwa kulifanya au anapoacha kufanya jambo ambalo alitakiwa kulifanya. Kusema kwamba kila mmoja wetu huja duniani anapozaliwa akiwa na mzigo wa dhambi iliyofanywa na babu yake wa nyuma kabisa huko itakuwa si chochote isipokuwa ni kukana sifa ya Mwenyezi Mungu ya Uadilifu na Rehema yake.

Ingawa Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu uhuru wa kuchagua na kufanya mambo anayoyapata hapa duniani, mwanaadamu ni kiumbe mwenye mfumo maalumu na mwenye asili na uwezo maalum. Mwanadamu atalipwa au kuadhibiwa kwa lile alilofanya yeye mwenyewe, si kwa lile lililofanywa na ndugu yake wa zamani huko. Matendo yetu wenyewe ndiyo yatakayoangaliwa siku ya hukumu na katika muda wa uhai wetu, Mwenyezi Mungu hutupatia kila nafasi inayowezekana ili tuweze kufanikiwa na Mwenyezi Mungu si mwenye kutudhulumu, mwenye kututwisha mzigo wa dhambi ambazo hatukuzifanya. Kwa hiyo ni sisi wenyewe ndio tutakaoitengeneza au kuiharibu hatima yetu hapa duniani na kesho huko akhera.

Hii ni kwa sababu Waislamu wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu alimsamehe Adam, kosa lake la kutotii amri ya Mwenyezi Mungu.

"Kisha Iblis aliwatekelezesha (wakala tunda katika ule mti) katika Bustani, na akawatoa katika ile hali waliyokuwa nayo -- kisha Adam akafunuliwa kuwa anatakiwa atubu, alipotubu Mwenyezi Mungu alimsamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwingi kusamehe, Mwingi wa Rehema". (Qur'an 2:36-37)

Mwenyezi Mungu alimsamehe Adam, na vilevile alimuondolea aibu na alamu ya kutorehemewa ambayo wakristo wanadai kuwa inarithiwa na wanadamu wote tokea wakati huo wa Adamu mpaka leo na watakaondelea kuzaliwa.

2) Kifo Cha Yesu

Kuhusiana na suala la kifo cha Yesu msalabani - ingawa ni wazi kwamba Yesu, kama alivyokuwa kwa mitume wengine kabla yake, walipatwa na masaibu makubwa kwa sababu ya kujaribu kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu ambao hawakuonyesha nia na ari ya kuupokea. Na alikuwa anajua vizuri kwamba hili lingemtokea, hata hivyo hakufikia kiwango cha kuuliwa na hususan kuuliwa kulikopangwa na Mungu - kama a livyodai Paulo baadaye, yaani kuuliwa ili kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi.

Katika Bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwa unyenyekevu na shauku kwa Mwenyezi Mungu kuwa "kikombe kinipite" (Mathayo 26:39), ambapo kikombe hiki kinamaanisha kukamatwa na kufa kwake. Hivi kweli tunaamini kwamba mja mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu anaweza kuomba rehema akanyimwa?

Wazo zima la kuteswa na kufa kwa Yesu msalabani ili awe kafara ya dhambi za wanadamu halikubaliani na hoja za kiakili na mantiki linapohusishwa na Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu. Je, inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni mwadilifu kwa kiwango cha juu kabisa akakataa kumsamehe Adam - na kizazi chake baada yake kwa ajili ya dhambi lake tu (Adam) - mpaka Yesu aje? Je, inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu amlazimishe mmoja wa waja wake akataka na kuruhusu kudhalilishwa na kuuwawa kwa mmoja wa mitume wake aliyekuwa mnyenyekevu na mtii sana kwake? Je, inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu amlazimishe mmoja wa waja wake afe kwa ajili ya dhambi za watu wengine? Katika Uislam, hatudhani kuwa hili linawezekana.

Tukiliangalia hili kutokana na mtazamo wa upendo Mwenyezi Mungu, hoja zile zile zinajitokeza kuhusiana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu: Je, Mungu mwenye upendo mkubwa kwa waja wake angewaadhibu wanaadam wote bila kuja Yesu? Je, Mwenyezi Mungu mwenye upendo mkubwa kwa waja wake angehitaji kuwa ni lazima mmoja wa waja wake wema na waaminifu (Yesu) adhalilishwe na kuuawa ili awasamehe wanadamu madhambi yao? Yeyote na kila mtu anaweza kushangaa na kujiuliza hii ni Aina gani ya upendo wa Mungu unaoweza kudai kiasi cha gharama kikubwa kiasi hicho na cha kutisha namna hii.

Uislam unashikilia kwa nguvu msimamo kwamba kila mtu anawajibika kwa vitendo vyake: kila mtu ataadhibiwa kwa maovu yake. Hai-ingii akilini kwamba Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu anaweza kumuadhibu mtu kwa dhambi alizofanya mtu mwingine.

"Kila nafsi italipwa kutokana na matendo yake na nafsi haitaulizwa juu ya matendo ya nafsi nyingine". (Qur'an 6:164)

Hakuna mtu anayeweza au atakaye adhibiwa kwa dhambi za mtu mwingine. Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba kila mmoja wetu atalipwa au kuadhibiwa kutokana na aliyoyafanya yeye mwenyewe katika maisha yake.

"Na Mwenyezi Mungu hamtwishi yeyote mzigo mkubwa kuliko ule anaoweza kuubeba. Kila jema nafsi inalolifanya ni kwa faida yake, kila uovu inaoufanya ni kwa hasara yake." (Qur'an 2:286)

3) Kuhusiana na Kafara

"Na katika kila ummah tuliwafundisha namna ya kufanya kafara ili wapate kulikumbuka na kulitukuza jina la Mwenyezi Mungu kwa riziki alizowaruzuku - - - nyama na damu havimfikii Mwenyezi Mungu, ni uchaji Mungu wenu ndio humfikia". (Qur'an 22:34,37)

Kwa hiyo, Uislamu haumini kwamba Yesu aliuliwa. Qur'an inasema:
"Walisema kwa jeuri, tulimuua Yesu kristo, mwana wa Mariamu, mjumbe wa Mwenyezi Mungu --- lakini hawakumuua wala hawakumsulubisha - bali Mwenyezi Mungu alimpaisha juu kwenda kwake (Mwenyezi Mungu)." (Qur'an 4:157-158)

Kwa kifupi, imani ya ukristo kuwa Yesu aliteswa na kuuliwa ili awe kafara ya dhambi za wanadamu haina nafasi yeyote katika Uislam. Waislamu wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu anachotaka ni toba ya kweli:

"Ombeni msamaha kwa Mwenyezi Mungu na tubuni toba ya kweli. Kwani Mola wangu bila shaka ni mwingi rehema na Mwenye kuwapenda waja wake." (Qur'an 11:90)

Uokovu Unatoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake

"Lakini kwa yeyote atakayetubia, akaamini, na kufanya vitendo vizuri, atakuwa ni miongoni mwa wale watakaookoka (na adhabu ya moto). (Qur'an 28:67)

Tukimwamini Mwenyezi Mungu, na tukijinyenyekesha kwake na kuufuata Mwongozo wake, tutakuwa na yakini (uhakika) wa Huruma na Rehema yake. Kama aya hapo juu inavyoonyesha, ikiwa toba yetu ni ya kweli, Mwenyezi Mungu anaweza na hutusamehe madhambi yetu. Hakuna haja ya mwombezi kwani kila mmoja wetu anaweza kumweleza Mwenyezi Mungu shida zake zote moja kwa moja na wakati wowote. Kwa kifupi hakuna haja ya mwokozi: Mwenyezi Mungu peke yake anaweza kulifanya hili.2
4) Kuokoka kwa Imani Peke Yake

Kwa haraka haraka, imani ya wokovu katika Ukristo inasema kwamba mwanadamu anaweza kuokoka kwa kuamini tu kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu.

Kuwaridhisha Watu wa Mataifa (Gentiles)

Kulikuwa bado kuna suala juu ya nini kitakachotokea baada ya kifo. Mitume wote walifundisha juu ya raha za peponi na shida za motoni, Yesu pia alilifundisha hili. Waumini wapya wa Paulo walihofishwa sana juu ya hili. Walitaka kujua ni namna gani wangeweza kuwa na uhakika wa kuingia peponi pindi mwisho wa dunia utakapofika.

Sheria ya Kiyahudi ilifundisha kwamba mtu angeweza kuokoka kwa kutii sheria za Mwenyezi Mungu, watu wa mataifa, hawakulifurahia wazo hili. Walikwenda kulalamika kwa Paulo kwamba kutii sheria za Mwenyezi Mungu lilikuwa ni jambo gumu sana kwao. Katika kulitatua tatizo hili, Paulo alisema utii wa sheria halikuwa jambo la lazima:

"- - Ni dhahiri kwamba sheria haiwezi kumfanya mtu akubalike mbele ya Mungu- - - hakuna uhusiano kati ya sheria na imani --- kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria- - -". (Wagalatia 3: 11-13)

Japokuwa sheria ilikuwa inamweleza mwanadamu yepi ni mazuri na yepi ni maovu na kuwahimiza kufanya mema na kuepuka maovu Paulo alisema kwamba kuja kwa Yesu kulibatilisha msingi kwamba utii wa sheria ni muhimu kwa ajili ya wokovu:

"Maana mtu hufanywa akubalike mbele ya Mungu kwa imani si kwa kutimiza matakwa ya sheria." (Waroma 3:28)

Licha ya ukweli kwamba Yesu mwenyewe alisema kuwa hakuja kuivunja sheria bali kuikamilisha (Mathayo 5:17), Paulo alilidharau kabisa wazo hili, akasema kwamba kumuamini Yesu peke yake kunatosha kumfanya mtu aokoke. Kwa mujibu wa Paulo, kuja kwa Yesu na kuyatoa maisha yake kama kafara ya dhambi za wanadamu, kulikuwa ndio mwisho wa haja ya kufuata sheria ya Mungu ili kupata wokovu. Sasa hivi imani peke inatosha. Uokovu sasa hivi haukutegemea ubora wa maisha ya mtu kimaadili au vitendo vizuri alivyovifanya, bali unategemea imani mtu aliyokuwa nayo.

Laana ya Sheria

Paulo alikuwa na sababu nyingine kuhusiana na msimamo wake juu ya sheria ya Mwenyezi Mungu. Katika kumbukumbu la Torati 21:23, Mungu anamwambia Musa kwamba mtu "aliyetundikwa katika mti"--- kwa maneno mengine aliyesulubiwa "amelaaniwa na Mungu".

Ili kulinda hoja yake kuwa Yesu alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu, na kwa sababu sheria inasema aliyesulubiwa amelaaniwa, Paulo aliamua kuiponda sheria kwa kusema:

"Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria, wako chini ya laana. --- Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajiliyetu; maana maandiko yasema "Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa". (Wagalatia 3:10:13)

Kwa sababu Paulo aliiona sheria ya Mungu kuwa ni laana, hivyo maneno ya Mungu katika kumbukumbu la Torati 21:23 hayakuwa na maana yoyote. Alipotosha maneno ya aya hii kwa kusema kuwa kwa sababu Yesu alipatwa na laana kwa kuwa aliuliwa kwa kusulubiwa msalabani na kwa vile yeye hakuwa na hatia, aliibeba laana hii kwa sababu ya dhambi za wengine. Na kwa sababu hii (Yesu) hakuwa na chembe chembe zozote za aibu au udhahili unaotokana na laana. Alilofanya Paulo hasa ni kulipa utukufu jambo ambalo awali lilikuwa linaonekana ni la aibu sana (kutundikwa msalabani) ili aweze (Paulo) kutetea imani aliyoanzisha kwamba uokovu umepatikana kwa sababu ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu kwa kudai kuwa kutundikwa kwake msalabani (Yesu) hakukumletea aibu yoyote japo sheria haikubaliani na wazo hili.

Anis Shorrosh anasema: "Msalaba, alama ya aibu, kupitia kwa Yesu ulibadilika na kuwa changamoto. Msalaba, uliokuwa alama ya kifo, kupitia kwa Yesu, ulibadilika na kuwa alama ya uhai".3

Kwa sababu ya upinzani mkali kutoka kwa wanafunzi wa Yesu, Paulo alilazimika kwenda pole pole katika utekelezaji wa jambo hili. Alianza na kitu kimoja ambacho watu wa mataifa walikipinga sana, yaani kutahiri (tohara). Kwa mujibu wa Paulo, Ibrahimu alikuwa mwongofu hata kabla ya kutahiriwa, sasa kwa nini watu waendelee kusumbuliwa kwa kuwataka watahiriwe? Paulo aliuupuza ukweli kwamba Mungu alikuwa ameweka agano hili mamia ya miaka kabla ya kuja Ibrahim. Kwa upande wake Nabii Ibrahim alipewa amri hii kutoka kwa Mungu juu ya kuwatahiri watoto wa kiume wote kuanzia wa zama zile na wote ambao watafuatia baadaye katika kitabu cha Mwanzo 17:14, Mungu aliliweka wazi jambo hili:
"Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu".
Mtu anaweza kushangaa vipi Paulo aamue kuyafuta maneno haya ya Mungu bila uoga wowote. Ubatizo ulichukua nafasi ya tohara (kutahiri), kumwagiwa maji sasa kumefanywa kuwa ndio alama ya agano baina ya Mungu na Mkristo. Watu wa mataifa walifurahia sana mabadiliko haya yaliyofanywa na Paulo.

Baada ya hili alianza kufanya mabadiliko katika uhalali na uharamu wa vyakula, na masuala mengine yalifuatia moja baada ya jingine. Ndani ya muda mfupi, sheria ya Mwenyezi Mungu haikuonekana tena kuwa ni mwongozo, unaostahiki kufuatwa katika maisha ya kila siku bali lililokuwa muhimu ni tu kuwa na imani kuwa Yesu aliteswa na hatimaye kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Hii ilikuwa inatosha kabisa kwa uokovu na sio kufuata sheria ya Mungu.

Kwa mujibu wa Paulo, suala la kufanya matendo mazuri kwa Mkristo linaweza tu "kuja lenyewe". Na muhimu zaidi kwa mkristo ni kuelewa kwamba vitendo vizuri peke yake haviwezi kumfanya mtu aokoke hata kidogo. Jambo pekee linaloweza kumfanya mtu aokoke ni imani juu ya uwezo wa Yesu wa kuokoa na kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ili tupate kuokoka - imani hii peke yake inatosha kumfanya mtu aokoke na adhabu ya moto wa jahanamu.

Paulo Alifanikiwa kwa Kukamilisha Jambo Gani ?

Paulo iliwapatia wakristo wapya imani ya wokovu kwa imani peke yake kwa sababu kubwa moja: Kupata wafuasi miongoni mwa watu wa mataifa. Watu wa mataifa walikuwa wamechunguza matendo mbali mbali ya kidini yaliyokuwa yanafanywa na Wayahudi lakini walikuwa wanasita kuukubali ukristo kwa sababu ya kuepuka miongozo na kanuni katika sheria ya Musa.

Imani na msingi huu wa mwisho yaani kuokoka kwa imani peke yake, imani ya kumwamini Yesu, ilikuwa ni imani kubwa na muhimu sana kuliko zote iliyobuniwa na Paulo. Na japokuwa ilikuwa ni dhambi kubwa sana kufanya mabadiliko katika imani kubwa na muhimu kama hii, lakini mabadiliko haya ndiyo yaliyopelekea mafanikio makubwa aliyoyapata Paulo katika kazi yake, kwa sababu aliwapa mambo yote muhimu waliyoyataka. Na kwa sababu hii watu wengi walimiminika makundi kwa makundi kuingia katika hii dini mpya ya Paulo yaani "Ukristo wa Paulo" sio "Ukristo wa Yesu". Yesu hakuwa amekusudia kufundisha mafundisho tofauti na yale waliyokuwa nayo Wayahudi kutoka kwa Nabii Musa wala hakukusudia kuanzisha dini mpya, lakini kwa sababu ya Paulo, Ukristo ulizaliwa na kuenea duniani kote, shukrani ziyaendee mafundisho ya Paulo.

  • 1. Islam In Focus, p. 137 (Uchunguzi juu ya Uislamu, uk. 137).
  • 2. What Everyone Should Know About Islam and Muslims, p. 183. (Mambo yampasayo kila mmoja kuyajua juu ya uislamu na Waislamu, uk. 183).
  • 3. Islam Revealed, p. 137. (Uislamu wawekwa wazi, uk. 137).

Mtazamo wa Uislamu

Mungu alimtuma Yesu kwa Wayahudi kwa sababu waliiacha ibada ya Mwenyezi Mungu kwa madai na visingizio kwamba wanafuata sherehe na uchambuzi wa kina wa sheria. Vitabu 63 vya Talmud - ambavyo ni tafsiri na uchambuzi wa sheria ya kiyahudi - ni uthibitisho juu ya jambo hili. Wayahudi waliamini kwamba wokovu unapatikana kwa kutii sheria ya Mungu.

Yesu alitumwa katika jitihada za kuwaelewesha kwamba vitendo vizuri peke yake sio mwisho wa mambo yote bali walitakiwa pia kumuamini Mwenyezi Mungu. Yesu alihimiza tena na tena kwamba "ibada tupu bila imani thabiti", si jambo lililotakiwa na Mungu kutoka kwao bali lililokuwa likitakiwa ilikuwa ni kufuata sheria zilizomo katika maandiko matakatifu "kwa dhati, uchaji Mungu na kumhofu Mwenyezi Mungu kwa dhati".1 Hili ndilo jambo ambalo Yesu alilifundisha bila kuchoka lakini kwa bahati mbaya, leo hii haya sio mafundisho ambayo Ukristo unasimamia utekelezaji wake ule ujumbe wa Yesu:

"Amri kuu kuliko zote ni, sikieni, Enyi Israel; Bwana Mungu wetu ni Mungu mmoja".

Unaopatikana katika Marko 12:29, si chochote ila ni maandishi tu katika karatasi Paulo alimpachika Yesu uungu, kisha akaandaa masharti ya uokovu kwamba kilichotakiwa ni imani peke yake juu ya Yesu kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Utii wa sheria ya Mwenyezi Mungu ulitupiliwa mbali na ukaitwa kuwa ni "Laana". Qur'an imeliweka jambo hili wazi kabisa. Imetaja masharti ya uokovu kuwa ni mawili, kumwamini Mwenyezi Mungu Mmoja na kutii sheria zake.2 "Kwa wale ambao wameamini na wakafanya vitendo vizuri Mwenyezi Mungu amewaahidi msamaha na malipo makubwa". (Qur'an 5:9)

  • 1. What Everyone Should Know About Islam and Muslims, p. 180. (Mambo yampasayo kila mmoja kuyajua juu ya Uislamu na Waislamu, uk. 180.)
  • 2. (Qur'an 5:9)

Uchunguzi Juu Ya Misingi, Mafundisho Na Imani Za Kikristo

Wayahudi walifanikiwa kuyazimisha mafundisho ya Yesu; lakini si Wayahudi tu bali hata dini ya Ukristo tuliyo nayo leo ambayo mafundisho na imani zake zote muhimu zimeanzishwa na Paulo pia imeyafutilia mbali mafundisho na imani zote zilizofundishwa na Yesu. Licha ya hoja zozote zinazoweza kutolewa na mkristo, hatuwezi kupata ushahidi wowote ambapo Yesu amethibitisha au kazitaja imani hizi nne (uungu wa Yesu, Utatu Mtakatifu, kufa kwa Yesu kwa ajili ya dhambi za wanadamu, na uokovu kwa imani peke yake) katika Injili.
Maadamu Yesu hakuwa na mpango wa kuanzisha dini mpya, basi bila ya chembe ya shaka ni wazi kwamba pia hakuunda au kuanzisha misingi au imani zozote za dini, kwani kama angekuwa na nia ya kuanzisha dini mpya basi angelazimika pia kuanzisha imani na misingi mipya ya dini. Lakini maadamu hakuanzisha wala hakuwa na nia ya kuanzisha dini yoyote mpya basi pia hakuna imani yoyote mpya ya dini aliyoianzisha.

Imani, misingi na mafundisho yote ya Ukristo ni kazi ya Paulo ambayo aliifanya kwa shabaha ya kuungwa mkono na kukubalika kwa wafuasi wapya miongoni mwa ambao hawakuwa Wayahudi wa zama zake. Kwa kuingiza na kuchanganya imani za kipagani katika mafundisho ya Yesu, Paulo alipata mafanikio makubwa mno katika kazi yake lakini kwa kufanya hivi aliharibu na kuivunjilia mbali imani ya kuamini Mwenyezi Mungu mmoja asiye kuwa na mshirika. Kwa kufanya hivi Paulo alifanikiwa kuyapotosha kabisa mafundisho yote ya Yesu na badala yake akaanzisha maradhi mabaya na yaliyoenea kwa haraka aliyoyatoa katika upagani - ambapo imani hizi bado tunazo mpaka leo katika ukristo. Ni hapa kwenye kiini na kitovu cha mafundisho ya Yesu palipotoshwa na hii ndio sababu kuu ya tofauti za msingi kati ya Uislamu na Ukristo.

Inafurahisha kuona kwamba "imani na misingi ya Ukristo" ambayo Qur'an inaikubali inaweza pia kuthibitishwa kwa urahisi kabisa, kuwa ni sehemu ya mafundisho ya wanafunzi wa mwanzo kabisa wa Bwana Yesu, ambapo imani na misingi ambayo Qur'an inaikataa inaweza kuthibitishwa kuwa ni maongezo (nyongeza) yaliyoongezwa na viongozi wa juu wa kanisa au Paulo. Waliyaongeza haya kwa sababu walipendezwa na falsafa na mifumo ya dini za Wapagani wa Kigiriki na wa Kirumi". 1

  • 1. Jesus in the Qur'an, p. 14. (Yesu katika Qur'an, uk. 14).

Maandiko Matakatifu Ya Kikristo

Dini iliyofunuliwa kutoka kwa Mungu ina nguvu na inakubalika sawa sawa na vile ufunuo ulivyo na nguvu na unavyokubalika. Kwa upande wa ukristo, msingi huu ambao ni mkubwa na mkuu kuliko yote ni dhaifu kabisa kutokana na kuingizwa mikono na akili za watu ndani ya Biblia. Ufunuo hauna mushkeli, tatizo ni juu ya nini kilitokea baina ya muda ufunuo ulipoteremka mpaka kipindi ufunuo huu ulipoandikwa.

Uchunguzi Makini Juu ya Agano La Kale

Wayahudi walishuhudia nyumba yao ya ibada ya Jerusalem ikiharibiwa kabisa mnamo mwaka 581 B.K. Pamoja na tukio hili pia, Torati yenyewe halisi pia iliharibiwa na baadaye walifanikiwa kurejesha hasara iliyotokea, lakini walizifanyia mabadiliko makubwa nakala chache zilizopata bahati ya kutoharibiwa kabla ya kuandika nakala nyingi zaidi kwa ajili ya matumizi ya kila mtu.
Ukweli kwamba nakala chache za Agano la Kale zilizonusurika kuharibiwa zilizifanyiwa mabadiliko makubwa unakubalika na wasomi na wanazuoni wakubwa isipokuwa wachache. Mabadiliko yalifanywa katika fani (style) muundo wa lugha na sarufi (grammer), ili kuzipamba habari na visa mbalimbali vilivyomo katika Biblia, na pia walithubutu hata kuviondoa kabisa vitu ambavyo wao waandishi hawakuvifurahia. Kwa kifupi, kazi za waandishi hawa ziliathiriwa sana na wakati walioishi pamoja na hisia, maoni, na imani zao binafsi.

Mifano kadhaa ya maongezo na mapunguzo yaliyopelekea kuchafuliwa kwa agano la kale ni kama ifuatavyo

1) Kuna aya mbili zinazotofautiana juu ya uumbaji zinazopatikana katika kitabu cha mwanzo: Katika sura ya kwanza imeandikwa kwamba uumbaji ulichukua siku sita. Ajabu ni kwamba katika sura ya pili, imeandikwa kwamba Mungu aliifanya kazi hii kwa siku moja (2:4). Tukiendelea na mikorogano hii iliyofanywa na waandishi ni juu ya ukweli kwamba Adam alikuwa ni kiumbe wa mwisho kuumbwa (1:27) wakati katika aya ya pili imeandikwa kwamba alikuwa ni kiumbe wa kwanza kuumbwa kabla ya kiumbe kingine chochote (2:4-9).

Tukiacha aya hizi mbili zinazotofautiana juu ya uumbaji, katika kifungu cha kwanza na cha pili pia kuna aya nyingine mbili zinazotofautiana juu ya gharika (mafuriko) katika kitabu cha mwanzo 6,7 na 8. Katika vifungu hivi, aya mbili zinatofautiana juu ya idadi ya wanyama ambao Nuhu aliwaingiza katika Safina. Aya nyingine mbili zinatofautiana juu ya sababu ya gharika, na aya nyingine mbili zinatofautiana juu ya muda ambao mafuriko yalidumu.

2) Katika kitabu cha Mwanzo 22:2, Mungu anatoa amri ifuatayo kwa Nabii Ibrahimu:

"Mchukue sasa mwanao, Is-haq mwanao wa pekee".

Hapa maneno "mwanao wa pekee" yeyote anaweza kukubali kwamba maneno haya yaliongezwa makusudi kwa lengo la kupotosha ukweli fulani kwa sababu wakati ule Ibrahimu alikuwa na watoto wawili Is-haq Na ndugu yake mkubwa Ismail, hakuwa Is-haq peke yake.

3) Na kama ni kweli kwamba Nabii Musa ndiye mwandishi wa kitabu cha kumbukumbu la Torati kama inavyodaiwa, inawezekanaje akaandika habari juu ya yaliyotokea wakati wa kifo chake kama inavyoonekana katika kumbukumbu la Torati kifungu cha 34?

Pia kuna suala juu ya jinsi Mungu anavyo onyeshwa katika Agano la kale kuwa ni katili na asiyekuwa na huruma hata kidogo:

1) Katika kitabu cha Hesabu 21:5-6, inaonyesha kwamba Mungu alipeleka nyoka wenye sumu kali kwa Wayahudi ambapo watu wengi waliumwa na kufa kwa sababu tu walilalamika juu ya chakula chao.

2) Katika kumbukumbu la Torati 7:2, inaonyesha kwamba Mungu aliwaamuru Wayahudi wawaue watu wote watakaowakamata kama mateka katika vita - wasionyeshe huruma na rehema hata kidogo.

3) Katika Samuel wa Pili 24:1-7, inaonyesha kwamba Wayahudi 70,000 walikufa kutokana na maradhi hatari ya kuambukiza yaliyoletwa na Mungu kwa sababu ya kutoridhishwa kwake na sensa (kuhesabu watu) iliyofanywa na Daud.

Mbali na kuonyeshwa sifa hizi za kutisha alizonazo Mwenyezi Mungu, kuna mifano mingi; inayowadhalilisha Mitume mbalimbali wa Mwenyezi Mungu:

1) Mabinti wa Luti walimnywesha pombe baba yao ili waweze kufanya naye mapenzi katika kitabu cha Mwanzo 19:30-38.

2) Inasemekana kwamba Daud alikuwa mzinifu katika Samuel wa pili 11:4-5.

3) Inasemekana Suleimani alikuwa muabudu masanamu katika Wafalme wa Pili 11:9-10.
Ndiyo, ni muhimu kujua kuwa Mitume hawa wa mwanzo walikuwa ni wanadamu katika nyanja zote, lakini kusema kuwa walifanya hayo yaliyotajwa hapo juu ni kuvuka mpaka Mno.

Haya sio yote. Katika vitabu vya Samueli, Wafalme na Mambo ya Nyakati kuna matukio mengi kama haya yaliyotokea katika historia ya mwanzo ya kiyahudi na pia ndani yake kuna idadi kubwa ya migongano na kupingana katika uelezeaji wa matukio haya. Kitabu cha Isaya, ambacho ni kitabu kinachopendwa sana cha "utabiri" kwa Wakristo kinatofautiana na vingine kwa kuwa na mifano inayonga'a ya maovu katika Agano la kale. Kwa mfano nukuu ya neno kwa neno, tazama Isaya 37, ambapo takribani ni nukuu ya neno kwa neno ya jitihada za mtunzi (mwandishi) wa Biblia inayopatikana katika Wafalme wa Pili 19.

Hii ni mifano michache tu inayoweza kupatikana katika Agano la Kale katika kuthibitisha tuhuma kwamba Biblia imebadilishwa mara kadhaa na kupotolewa na mikono ya watu. Ni vigumu kuzitetea tuhuma hizi hasa kwa sababu kuna mifano mingi mno inayothibitisha tuhuma hizi katika Biblia tukiachilia ukweli kwamba hakuna maandiko ya asili (original) ya Agano la Kale yaliyopo leo hii.

Uchunguzi Makini Juu Ya Agano Jipya

Ambapo Agano la kale lina umuhimu mkubwa sana kwa Wayahudi, kwa Wakristo halina nafasi muhimu kiasi hicho ambapo wao wanaliona kuwa kwa sehemu kubwa ni mkusanyiko wa utabiri wa manabii juu ya kuja kwa Yesu. Amri na mafundisho yake hayana uthabiti wala umuhimu wowote kwao.

Mapenzi ya Wakristo yapo kwenye Agano Jipya. Katika vitabu hivi 27 vya Agano Jipya kimsingi kuna maandiko ya Paulo; vitabu ambavyo vinajumuisha vitabu vinne vya Injili - ambavyo ilivyo hakuviandika kwa mkono wake japokuwa alianzisha wazo la kuviandika. Kwa asili, maelekezo yote ya kuandika vitabu hivi yalitolewa na Paulo.

Baada ya kufanya uchunguzi makini katika vitabu vyote viwili, Biblia na Qur’an, Dr. Maurice Bucaille anasema kwamba: "---- kuzisoma injili kikamilifu (vitabu vinne vya Injili) ni kama kuwayumbisha na kuwavuruga Wakristo kabisa".1

Ametoa maelezo haya kwa sababu kwa mujibu wa utafiti wake, migongano, mikorogano, umyakinifu, uwingi wa makosa na upotoshaji wa maandiko: "--- vinaongezea juu ya ukweli kwamba vitabu vya Injili vina sura na vifungu ambavyo bila chembe ya shaka ni zao la fikra na ubunifu wa wanadamu".2
Mifano mbalimbali juu ya migongano katika vitabu vya Injili ni:
1) Injili ya Mathayo ina mtiririko wa kizazi cha Yesu (Mathayo 1:7) ambapo unamuonyesha kutoka kwa Ibrahimu hadi kwa Suleiman, mtoto wa Daud, ambapo mtiririko wa kizazi hiki katika Injili ya Luka (3:31) unamuonyesha Yesu kutoka kwa Adam kupitia kwa Nathan ambaye ni mtoto mwingine wa Ibrahim asiyekuwa Suleiman kama ilivyo katika Mathayo. Na hata mtu akijaribu kulinganisha majina yaliyopo katika orodha ya Mathayo na ile ya Luka hayawiani kabisa.

Nukta muhimu ya kuzingatia hapa ni kwamba aina Yoyote ya mtiririko wa kizazi chaYesu kwa Ukoo wa ubabani kupitia kwa Yosefu ni jambo la kichekesho kwa sababu Yesu hakuwa na baba wa kibailojia. Ukoo sahihi wa Yesu unaweza kuwa ni ule unaopitia kwa mama yake, Mariam - sio kwa Yosefu (Yusuf).

2) Injili ya Yohana inakhitilafiana sana na Injili nyingine tatu katika Kila upande na sura ya maisha ya Yesu na kazi yake kama vile sehemu alipozaliwa na kukua, ubatizo wake, na hata maeneo aliyofanya kazi na ukubwa wa kazi yake. Inasemekana kwamba 92% ya maelezo na habari zilizomo katika injili ya Yohana hayamo kabisa katika zile injili nyingine tatu.3

Moja ya tofauti kubwa kati ya injili ya Yohana na zile nyingine tatu ni kwamba Yohana hasemi lolote juu ya Komunio Takatifu (chakula cha Bwana yaani mkate na divai). Katika maelezo ya Yohana juu ya Karamu (chakula) ya Mwisho, inayopatikana katika vifungu vya 13-17, Yesu anawaosha wanafunzi wake miguu na kisha anatoa hotuba ndefu ambapo sasa inaonyesha kutatanisha kidogo juu ya Mfariji atakaye kuja baada yake, hapakugusiwa hata kidogo juu ya komunio takatifu - yaani mkate (mwili wa Bwana) na divai (damu ya Bwana) ambayo ni jambo muhimu mno kwa Ukristo leo hii.

3) Mathayo na Yohana hawajazungumza lolote juu ya kupaa kwa Yesu. Luka ameandika juu ya hili katika Injili yake na pia katika kitabu chake kingine kiitwacho Matendo ya Mitume wakati na mahali vinatofautiana kuhusiana na mada hii katika vitabu hivi viwili.

Marko pia anazungumzia juu ya kupaa kwa Yesu, lakini sasa hivi wanazuoni na wasomi wa Biblia wanakubali kwamba taarifa yote juu ya tukio la kupaa mbinguni kama ilivyoandikwa katika injili ya Marko "Sio sahihi" (angalia sehemu ya mbele kuhusiana na aya zinazothibitisha hili).

Kuhusiana na "mafundisho tusiyokubaliana nayo" hebu tuichunguze imani ya kafara, (yaani kwamba Yesu aliteswa na kuuawa ili awe kafara ya dhambi za wanadamu) ambayo imejengwa juu ya msingi kwamba Yesu alikuwa kiumbe mkamilifu katika kila hali. Mtu anaweza kushangaa, kutokana na dai hili, vipi Wakristo wanazithibitisha nukuu (aya) mbalimbali katika vitabu vya injili zinazoonyesha kuwa Yesu hakuwa mkamilifu baadhi yake ni hizi zifuatazo:

1) Katika Mathayo 16:23, Yesu anamwita Petro "Shetani" na "mtego wa hatari". Petro anapojaribu kumkinga.

2) Katika marko 11, Yesu anaulaani mti kwa sababu tu haukuwa na matunda msimu ambao haukuwa wa matunda ilipotokea kwamba alikuwa na njaa na kupitia kuangalia kama kulikuwa tunda lolote na akawa hakupata.

3) Katika Yohana 2:1- 4, Yesu anaonyesha kukosa adabu kwa mama yake.

Katika Mathayo 28:19 Yesu anawaambia wanafunzi wake waende wakawabatize watu kwa jina la Baba na Mwana na Roho matakatifu. Ukweli kwamba maneno haya yaliongezwa baadaye katika Biblia inaweza kuthibitika kwa kusoma barua ya Paulo ambapo anasema hapo awali ubatizo ulifanyika kwa jina la Yesu peke yake.

Tunaona kwamba katika Marko, 16:15 Yesu anasema:

"Enendeni ulimwenguni kote, mkahubiri injili kwa watu wote (viumbe wote)".

Marko anazungumzia katika 16:15 tukio lile lile linalozungumziwa na Mathayo katika 28:19, sasa maneno ya ziada tunayoyaona katika Mathayo (ambayo hayapo katika Marko) yametoka wapi?

Yesu Katika Injili

Kama ilivyodokezwa hapo awali, Agano Jipya, na hususan vitabu vitatu vya injili - lina nafasi maalumu kwa Wakristo. Wanavichukulia vitabu hivi vinne kama mwongozo, kwa sababu moja muhimu. Vitabu hivi vinne vya injili viliandikwa Kwa Ajili Ya Wakristo na viliandikwa Na Wakristo. Katika injili nne Yesu wa kihistoria amewekwa pembeni kwa manufaa ya Yesu aliyefanywa Mkristo (Paulo).

Waandishi wa Injili wenyewe bado wana maswali mengi. Ingawa hakuna uhakika ni nani aliyeziandika injili hizi nne, wanazuoni wengi wa Biblia wamekubaliana kwamba Mathayo na Marko hawakuwa waandishi wa Injili zinazobeba majina yao. Injili ya Luka inadhaniwa kuandikwa na rafiki wa Paulo ambaye alikuwa mtu wa mataifa (Hakuwa myahudi) ambaye hakuwahi hata kumuona Yesu; ni sehemu ya kwanza ya maandiko yake juu Ukristo wa Mwanzo ambayo inajumuisha kitabu cha Matendo ya Mitume.
Ingawa wakristo wengi wanasema kwamba Injili ya Yohana iliandikwa na mwanafunzi wa Yesu aliyekuwa na jina kama hili (yaani Yohana). Sasa hivi wanazuoni wa Biblia wanatia mashaka juu ya hili kutokana na ukweli kwamba kitabu hiki kiliandikwa mwaka 100 Baada ya kristo, na Yohana, mwanafunzi wa Yesu alikufa shahidi mwaka 70 Baada ya kristo, miaka 30 baada ya kifo chake.

Katika kuikubali nadharia kwamba watu wengine tofauti na wanafunzi wa Yesu waliandika vitabu vinne vya injili lazima pia ikubalike kwamba waandishi hawa inawezekana kwamba hawakuona kwa macho yao au kusikia kwa masikio yao mengi - kama si yote - ya matukio waliyoyaandika. Hata tukiamua kusema kwamba wanafunzi wa Yesu waliziandika injili kwa mikono yao, tunaelewa kwamba hawakushuhudia matukio yaliyotokea pindi Yesu alipochukuliwa na maaskari kutoka katika Bustani ya Gethsemane kwa sababu imeandikwa: "- - kisha wanafunzi wote walimuacha wakakimbia --", katika injili zote mbili katika Mathayo 26:56 na katika Marko 14:50. Kwa kifupi, mengi tunayoyaona katika injili ni fununu na tetesi tu - si maandiko ya watu, walioshuhudia matukio yenyewe.

Nukta nyingine tunayoweza kuiangalia katika uchunguzi wetu juu ya injili ni kwamba katika injili zote nne hakuna hata moja iliyoandikwa wakati wa Yesu, ikizingatiwa kuwa hakuna taarifa iliyohifadhiwa juu ya kazi zake (Yesu) katika wakati wa uhai wake. Kwa kweli, karibu miaka arobaini ilipita kuanzia kipindi Yesu alipoondoka duniani mpaka kitabu cha kwanza cha injili kilipoandikwa.
Mwishoni wakati injili ya Marko inakuwa tayari, Paulo alikuwa ameshaanza kuhubiri kwa takriban miaka ishirini; na alikuwa tayari ameshaandika barua (waraka) yake kwa Warumi, ambapo alielezea imani na mafundisho yake yote aliyoyaandaa na kuyaingiza katika Ukristo. Kutokana na ukweli huu tunaweza kuona kwamba mafundisho ya Paulo, bila chembe yoyote ya shaka, yaliwaathiri na kuwavuta waandishi wa injili kwa kiasi kikubwa katika maandiko waliyoyaandika.

Vitabu vinne vya injili viliandikwa kati ya miaka 70 B.K. na 100 B.K. ya Marko ilikuwa ya kwanza, ikafuatiwa na ya Mathayo, kisha Luka na mwisho Yohana. Injili tatu za mwanzo zinafanana sana katika uandishi wake, uchunguzi wa haraka utaonyesha kwamba waandishi wa injili ya Mathayo na Luka walichukua (waliibia) habari nyingi sana kutoka kwa Marko walipokuwa wanaandika injili zao. Hii ndio sababu injili hizi tatu zinaonekana kuelezea kitu kimoja.

Injili ya Yohana inatofautiana sana na injili nyingine, hata hivyo hii ndio yenye mashaka zaidi juu ya ukweli na usahihi wake hasa kwa sababu mwandishi alijishughulisha zaidi na umuhimu wa Yesu katika imani ya ukristo kuliko yale yaliyosemwa na kufanywa naYesu.

Tunaweza kuhitimisha, kwa sababu ya uchache wa muda, kwamba kuandika kutokana na tetesi au fununu, na mvuto wa Paulo aliowaathiri waandishi, sura ya Yesu iliyoletwa kwetu katika injili si ya yule Yesu wa kihistoria (Yesu halisi). Badala yake, waandishi hawa waliandika juu ya Yesu aliyetokana na masimulizi ya kale, kwa kutumia hoja ya kithiolojia kwamba waandishi hawa waliukristisha ukweli (yaani waliufanya ukweli uwe wa Kikristo). Waandishi walikuwa na imani kali za kikristo, na waliandika wakiwa na mtazamo huu akilini.

Matokeo yake ni kwamba injili hizi nne zina visa na masimulizi ya kale badala ya ukweli. Ujumbe wa Yesu aliokuja nao kutoka kwa Mungu wote umepotea kwa sababu ya shinikizo la yale ambayo watu walitaraji na kutaka Yesu aseme na kufanya badala ya lile lililofanyika kiukweli.

Nakala za Nakala za Biblia

Nakala zote za mwanzo za Biblia zilikuwa ni nakala tu. Nakala hizi ziliandikwa kwa mkono. Nakala ya kwanza kuchapwa kwa mashine ilitoka katika karne ya kumi na tatu ambayo iliitwa Biblia ya "Gutenburg". Maandiko ya asili (original manuscripts) yalitupiliwa mbali na badala yake zikaanza kutumika nakala mpya kwa sababu zile zilikuwa zimechoka na kuchanika chanika kutokana na kutumiwa kwa muda mrefu. Nakala hizi mpya baadaye, zilitumika kutengenezea nakala nyingi zaidi.

Hata hivyo, kila nakala iliyotengezwa, ilimaanisha kuwepo kwa nafasi zaidi ya kufanya mabadiliko - aidha ya bahati mbaya au ya makusudi ambayo yote haya yaliingizwa katika Biblia. Kama ilivyokuwa kwa Agano la Kale, Agano Jipya pia lilipatwa na balaa la kuongezewa na kupunguziwa baadhi ya maneno, aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya kutoka kwa waandishi wake.

Ni lazima ionyeshwe kwamba hakukuwa na namna yoyote ya kurudi nyuma na kuangalia usahihi wa kazi za waandishi hasa kwa vile hakuna maandiko ya asili (original manuscripts) ya Agano la Kale wala Jipya. Nakala zilizopo ambazo tunaweza kusema ni za zamani kabisa ni za karne ya saba au ya nane baada ya kristo ambapo zilichambuliwa na kuchaguliwa ambazo ni bora zaidi kutokana na nakala nyingi na za aina mbalimbali zilizokuwepo wakati ule.
Kwa upande wa Agano Jipya hakuna nakala ya asili iliyopo. Tuna nakala tu, ambazo tunaweza kusema ni za zamani zaidi ambazo ziliandikwa katika karne ya nne, kipindi ambacho maandiko "rasmi au maandiko ya kiofisi" yaliwekwa na kanisa. Ukosefu huu wa nakala za asili (original manuscripts) uliondoa kabisa uwezekano kwa yeyote kujaribu kukagua usahili; na mabadiliko mbalimbali yaliyopenyezwa katika Biblia.

Suala la Kutokamilika

Makanisa ya mwanzo ya kikristo hayakuwa na seti maalum (ya kiofisi - rasmi) ya maandiko Matakatifu. Baadhi ya Makanisa yalikuwa na seti fulani ya vitabu wakati Makanisa mengine yalikuwa na seti tofauti ya vitabu. Kuna baadhi ya watu waliridhika hata kuwa na kitabu kimoja cha Injili katika vinne, wakiamini kwamba vyote vilikuwa sawa na vilikuwa na habari moja.

Kulikuwa hata vitabu ambavyo katika Biblia za leo havimo - kwa mfano kulikuwa vitabu kumi na tano vilivyozidi katika Agano la kale na vitabu kumi na sita katika Agano Jipya.

Kutokana na ukosefu wa mpangilio maalum katika kanisa kuhusiana na maandiko yake Matakatifu, Maaskofu walikutana pamoja ili kuweka sera ya kiofisi ya kanisa kuhusiana na suala la utatu Mtakatifu katika Mkutano wa Nicea mwaka 325 B.K. ambapo pia waliandaa na kujiwekea Maandiko Maalum Rasmi yatakayotumika katika Kanisa.

Walikusanya nakala moja kwa kila aina (seti) ya maandiko aliyokuwa ikitumika wakati ule na wakafanya maamuzi juu ya ni vitabu vipi vitambulike kuwa ndio maalum na rasmi kwa Wakristo wote na nchi zote za Kikristo (kuwa ni Maandiko Matakatifu). Hatimaye vitabu sitini na sita vilichaguliwa, 39 kwa ajili ya Agano la Kale na 27 kwa ajili ya Agano Jipya.

Vitabu saba katika kumi na tano vilivyozidi katika vitabu vya Agano la Kale viliendelea kutumiwa na kanisa Katoliki, lakini hata hivi baadaye vilitupiliwa mbali na Waprotestanti wakati wa harakati za mageuzi katika karne ya kumi na sita. Hakuna Hata Kimoja katika vitabu kumi na sita "vilivyozidi" vya Agano Jipya kilichofanywa kuwa ni sehemu ya Maandiko Matakatifu maalum na rasmi yanayotumika.

Vitabu hivi vilivyozidi vilipewa jina la "Apocrypha" - neno la kigiriki lenye maana ya "iliyofichika" - vitabu hivi vya ziada ambavyo hapo awali vilikuwa sehemu ya Biblia vilitupiliwa mbali kwa kile kilichodaiwa na viongozi wa kanisa kuwa "vilikhitilafiana" na imani zilizokuwa zikikubaliwa na kanisa. "Waandishi wa vitabu vya Aprocrypha (yaani vitabu vya ziada) bila shaka walikuwa wachamungu na waliofanya kazi kwa dhati na uhodari mkubwa - na tukisoma waliyoyaandika, mara moja tutagundua kwamba maneno yao - yalikuwa yameepukana na udhaifu wa kutokuwa sifa za kuwa maandiko matakatifu -".4

La kushangaza zaidi ni kwamba rejea ya baadhi ya vitabu hivi vilivyofichikana (Apocrypha) zinaweza kupatikana katika Biblia ya leo inayotambulika kiofisi kama vile "kitabu cha vita vya Yehova" kilichotajwa katika Hesabu 21:14 "kitabu cha Jashar" kilichotajwa katika Joshua 10:13.

Hivyo, Biblia, tuliyonayo leo hii, si tu kwamba imekuwa (victim) muhanga wa kuingiliwa, kuongezwa na kupunguzwa bali pia haiwezi kuchukuliwa kuwa ni kamilifu. Inawezekanaje Maneno ya Mungu yakaondolewa na kutupiliwa mbali kwa sababu ya matakwa ya mwanaadamu?

Tatizo la Kutafsiri

Wataliano wana usemo usemao "Wafasiri ni waongo". Msemo huu una ukweli ndani yake na umetokana na uchunguzi makini. Kuchukua kitu fulani kilichoandikwa katika lugha fulani na kujaribu kukiingiza katika lugha nyingine huwa inaleta matatizo kwa sababu mara nyingi wafasiri hupambana na maneno katika lugha moja ambayo hayamo katika lugha nyingine. Neno jingine badala yake lazima litumike na matokeo yake ni kubadilika kwa maana.

Agano la kale mwanzo kabisa liliandikwa kwa Kiebrania, lakini lilitafsiriwa katika karne ya tatu kwenda katika lugha ya Kigiriki kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa wanaishi nje ya Palestina (ambao walikuwa wanaongea Kigiriki - badala ya Kiebrania). Tafsiri hii iliitwa "Septuagint" na ilitumika sana hata na wakristo wa mwanzo.

Agano Jipya liliandikwa katika lugha ya Kigiriki lakini maadamYesu mwenyewe alitumia lugha ya kiaramaiki, hii ina maana kwamba maneno yake yalilazimika kutafsiriwa na hivyo kusababisha uwezekano wa makosa

Tafsiri ya kigiriki iliyokuwa ikiitwa Septuagint iliunganishwa na maandiko ya Agano Jipya yaliyokuwa katika lugha ya kigiriki katika karne ya nne. Maandiko haya yaliyounda Biblia kamili sasa hivi yanaeleweka kama "Codexsinaiticus" na "Codex Vaticanus" na hizi ndio nakala za maandiko ya zamani kabisa zilizopo leo. Hakuna maandiko ya mwanzo kuliko haya yaliyonusurika kutupiliwa mbali.

Katika karne ya nne, Biblia ilitafsiriwa kwenda katika lugha ya Kilatini na Mt. Jerome. Na hii ilibakia kuwa lugha ya Biblia hadi karne ya kumi na sita ambapo watu wa Mageuzi kama John Wycliffe, William Tyndale na Martin Luther walipoifasiri Biblia katika lugha mbalimbali za watu - jambo ambalo lilikuwa haliruhusiwi kabisa na viongozi wa kanisa wa wakati ule na ili kufanikisha lilimgharimu Tyndale maisha yake. Walifanya hivi ili kuwazuia watu kuyasoma, kuyaelewa au kuyahisi maandiko yao Matakatifu - haya yalifanywa makusudi na viongozi wa kanisa.

Tafsiri nyingine zilifuatia ndani ya muda mfupi. Karibu na mwisho wa karne ya kumi na sita kulikuwa na tafsiri za lugha mbalimbali na tafsiri mbalimbali za lugha moja ambazo zilileta malumbano na mabishano makubwa jambo lililomfanya Mfalme James I wa Uingereza kuteua kamati ya wanazuoni hamsini na nne ili kuandaa toleo "rasmi" na litakalotambulika na mamlaka. Watu hawa (kamati) walizisoma tafsiri zote zilizokuwepo wakati ule na, mnamo mwaka 1611, walitoa toleo lililoitwa "King James Versions of the Bible" yaani toleo la Biblia la Mfalme James - ambalo lilikuwa ndio toleo rasmi miongoni mwa Wakristo kwa mamia ya miaka.

Tatizo Lililopo Leo: Matoleo Mapya

Tatizo la uharibifu na upotoshaji lililoambatana na kutafsiri liliisha mwaka 1611, kwa kupatikana toleo la King James Versions of the Bible, tatizo la marudio - "kuiboresha" au kuifanya kuwa ya "kisasa" limeikabili Biblia leo hii.

Kiwango cha uharibifu na upotoshaji huu ni kama ifuatavyo: katika mwaka 1952, makala yenye kichwa cha habari "Ukweli kuhusu Biblia" yalionekana katika gazeti la "Look" (Tazama). Makala haya yalisema kwamba kulikuwa makosa zaidi ya 20,000 (elfu ishirini) katika Agano Jipya peke yake. Mashahidi wa Yehova walilizungumzia suala hili katika toleo la Septemba, 1957 la gazeti lao la "Awake" (Amka) ambapo walisema "- - Wafasiri walifanya makosa katika kufasiri (Biblia) ambayo yamesahihishwa na wanazuoni wa zama hizi- -".5 Mtu anaweza kujiuliza ni jambo la ajabu wanazuoni hawa walilifanya!!

Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo waliamua kuiboresha lugha ilivyotumika katika King James Version. Jitihada zao zilizaa toleo jipya la Biblia liitwalo "American Standard Version" lililotolewa mwaka 1901. Wakristo waliolifanyia kazi toleo hili sio tu kwamba waliikuza na kuiboresha lugha bali pia walifanya mabadiliko katika Biblia yenyewe:

1) Katika kuuthibitisha ukweli kwamba baadhi ya maneno yaliondolewa na mengine kuongezwa, tunaweza kuangalia katika maandiko ya mwanzo ya Biblia yaliyokuwa katika lugha ya kigiriki toleo la Biblia la King James Version Yohana 5:8 ambapo imeandikwa "Baba, Mwana na Roho Mtakatifu". Lakini toleo jipya la American Standard Version, wanazuoni walibadilisha na badala yake wakatumia maneno "Roho, Maji na Damu".

2) Aya nzima inayopatikana katika Mathayo 17:21 ambayo inazungumzia juu ya ukuaji wa usafi wa kiroho kwa sala na kufunga iliondolewa kwenye American Standard Version, na neno "Kufunga" liliondolewa katika aya kama hii inayopatikana katika Marko 9:29.

Maelezo juu ya hili yanayopatikana katika sherehe yake (chini ya ukurasa) yanasema: "Mamlaka nyingi, baadhi zikiwa ni za zamani, zinaiingiza pia aya 21" (ambapo katika Biblia za sasa aya hii ya 21 imeondelewa).

3) Katika kukubali ukweli mwingine juu ya uongezaji na upunguzaji wa baadhi ya maneno katika Maandiko Matakatifu (Biblia), vifungu vya Yohana 7:53 na Yohana 8:1-11 umefungiwa mabano na katika sherehe yake (maelezo ya ziada) wameeleza kwamba vifungu hivi "havipatikani katika Biblia (Maandiko matakatifu) nyingi za zamani".

Baada ya miaka kadhaa viongozi wa kanisa walikutana wakaamua kuliboresha toleo la Biblia la American Standard Version. Matokeo ya jitihada zao ilikuwa ni kupatikana toleo jingine la Biblia linalojulikana kama "The Revised Standard Version" - yaani toleo la Biblia la kiwango bora na lililofanyiwa marekebisho. Toleo hili lilitoka rasmi mwaka 1952.

Katika dibaji ya Toleo hili kuna maelezo haya: "- - - Toleo la King James (King James Version) lina makosa na mapungufu mengi mno na hatari sana kiasi kwamba kuna haja kubwa ya kulifanyia marudio na marekebisho toleo zima - -".

Katika toleo la Biblia la 'The Revised Standard Version' tunakuta kwamba aya katika injili ya Marko zinazozungumzia juu ya kupaa kwa Yesu (Marko 16 : 9-20) zimeondolewa kwa madai kwamba aya hizi hazipatikani katika Biblia (maandiko) za zamani kabisa.

Katika mwaka 1989, toleo la Biblia la 'The Revised Standard Version' la 1952 liliboreshwa tena na hivyo likapatikana toleo jipya "The New Revised Standard Version". Na katika toleo hili aya zinazozungumzia juu ya kupaa kwa Yesu katika Marko 16 zilirejeshwa. Kwa vile Wakristo wengi hawakufurahia "kumomonyolewa" kwa moja ya imani zao za msingi kulikofanywa na Wahariri wa "The Revised Standard Version", ilibidi aya hizi zirejeshwe ili kuwaridhisha.

Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema, kutokana na marudio ya mara kwa mara yaliyofanyika kwa miaka mingi wakati wa kufasiri na "Matoleo" mbalimbali mapya katika Biblia tuliyonayo leo maandiko ya wanadamu ndio mengi zaidi kuliko ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Wakristo Wenyewe Wanasemaje Juu ya Tatizo Hili

Huko nyuma katika karne ya nne, Mt. Augustino aligundua makosa mengi, ndani ya Biblia. Akizungumzia juu ya suala hili katika barua yake Na. 82. Alisema kwamba makosa katika uelewaji ndio sababu ya tatizo hili (la kuona aya zinapingana, na nyingine zipo katika toleo hili, lakini katika toleo jingine hazipo na utatanishi mwingine mwingi). Anasema yeye haamini kwamba watu kuongeza, kupunguza na kubadilisha baadhi ya mambo katika Biblia kuwa ni tatizo ila tatizo ni uelewaji mbaya katika usomaji. Kwa maneno mengine anasema kwamba baada ya msomaji kukumbana na mikorogano hii katika Biblia anatakiwa abuni maelezo fulani yatakayokuwa ni msamaha wa makosa haya.

Utafiti unaojaribu kuangalia na kuonyesha makosa katika Maandiko Matakatifu, tofauti na watu wengi wanavyofikiri, umeanza hivi karibuni. Kwa mamia ya miaka Biblia ilikubalika tu "kama ilivyo". Ilichukuliwa kuwa ni dhambi kubwa sana kujaribu kukosoa kosa, hata dogo lililomo ndani ya Biblia na viongozi wa kanisa walifanikiwa sana kuyazima majaribio yoyote ya kujaribu kuikosoa Biblia.

Kitabu cha kwanza kuonyesha na kukosoa makosa katika Biblia kilichoandikwa na Richard Simon kiitwacho Critical History of the Old Testament (Historia inayojaribu kuonyesha na kukosoa makosa yaliyomo katika Agano la kale), kilitoka mwaka 1678. Kitabu hiki kilileta tafrani na mtafaruku mkubwa lakini kilisaidia sana kufungua njia kwa wale waliokuja baadaye katika karne ya 18 na 19 kwa dhumuni la kufanya utafiti juu ya makosa yaliyomo katika Agano la Kale.

Kutokana na ukweli mwingi usiopingika uliotolewa na watu mbalimbali, Halmashauri ya awamu ya Pili ya Vatican (1962- 1965) ilitoa maelezo yanayoshangaza juu ya jambo hili " - Vitabu vya Agano la Kale vina (ndani yake) habari zisizo sahihi na zenye mapungufu mengi --." 6Agano Jipya pia lina kasoro na mapungufu mengi. Ingawa Halmashauri ya awamu ya pili ya Vatican inashikilia kwamba Injili "kihistoria ni ya kweli " na kwamba wao "kwa uaminifu kabisa wanaeneza yale ambayo Yesu alifanya na kufundisha watu wakati wa maisha yake".7 Wanazuoni wengine wamekuwa na maelezo ambayo ni kinyume kabisa na msimamo wa Vatican.

Katika kitabu chake "The Call of the Minaret" (Wito kutoka katika mnara wa msikiti, Adhana), Dr. Kenneth Cragg anasema kwamba kuna "mambo yaliyoongezwa na kupunguzwa" katika Agano Jipya Injili na ni kazi ya akili ya viongozi wa kanisa ikiongozwa na waandishi, na kwamba katika kazi zao wanatumia uzoefu na historia." 8

Padre Kannengiesser, Profesa katika taasisi ya kikatoliki katika mji wa Paris, alionya katika kitabu chake "Faith in Resurrection" (Imani juu ya ufunuo), kwamba watu wasijaribu "kuyatafsiri na kuyaelewa maneno kama yalivyo" juu taarifa za kweli kuhusiana na Yesu katika Injili - onyo ambalo pia lilitolewa na Padre Rognet wa Paris katika kitabu chake "Initiation to the Gospels".

Carl Andrey, profesa wa falsafa na masomo ya dini katika Chuo kikuu cha Ball State kilichopo Indiana anasema kwamba vitabu vinne vya Injili: "- - - viliandikwa na watu wenye shauku wa harakati za mwanzo za kikristo na kwamba wanatupatia nusu tu ya habari kamili na kwa kiasi kikubwa ni mazao ya fikra za waandishi wao." 9
Mwisho tuna maelezo ya Dr. W. Graham Scroggie wa "Prestigious Moody Bible Institute" ambaye anasema: "Ndiyo, Biblia ni zao la kazi iliyofanywa na binadamu - - - vitabu hivyo vimetokana na akili za watu, vimeandikwa kwa mikono ya watu, na fani ya uandishi wake ni ya kibinadamu.10

Kama huu ndio msimamo wa wanazuoni wa Biblia, wakristo wa "kawaida" watakuwa na lipi la kusema juu ya jambo hili?

Wengi (wa wakristo wa kawaida) hata hawajui lolote juu ya kasoro nyingi zilizomo ndani ya Biblia kwa sababu waandishi wa utangulizi na washereheshaji (wanatoa maelezo ya ziada) wa Biblia. Wanatumia mbinu mbalimbali za kijanja ili kuwafanya Wakristo wasiyajali na wajisahaulishe na maswali ambayo wangejiuliza juu ya kasoro nyingi zilizomo ndani ya Biblia. Pamoja na mambo mengine, waandishi hawa:

1) Wanaandika mambo kama ukweli uliothibitika wakati ukweli na uthabiti wake una mashaka, na

2) Wanayafunika makosa na kasoro zilizomo ndani ya Biblia kwa kutoa nyudhuru na kuomba radhi mbinu ambayo inaondoa umakini wa msomaji kutoka kwenye dosari na kasoro zilizomo ndani ya Biblia na badala yake kuangalia mambo mengine.

Kina wanachokwenda washereheshaji (Commentators) katika kujaribu kutetea kasoro na dosari zilizomo ndani ya Biblia ni alama na ushahidi tosha juu kutojisikia kwao vizuri na ugumu wanaoupata katika jitihada zao za kujaribu kutetea makosa, dosari na kasoro zilizomo ndani ya Biblia.

Pamoja na ukweli huu juu ya kasoro na dosari zilizomo ndani ya Biblia, ajabu ni kwamba mtu anapojaribu kuzionyesha hataambulia chochote kutoka kwa wakristo isipokuwa uadui. Niliwahi kupeleka makaratasi yenye utafiti wangu juu ya kasoro na dosari mbalimbali zilizomo ndani ya Biblia katika mishenari ya kikristo ambapo walinijia muda mfupi baadaye wakinishutumu kwa kufanya "uvamizi dhidi ya Biblia. Muongeaji aliendelea kusema kwamba "Biblia imefanyiwa uvamizi (imevamiwa) kwa karne nyingi, lakini bado ipo. Imestahimili vishindo (vyote) vya nje na ndani".11

Nastaajabu vipi mtu awe na msimamo kama huu mbele ya mifano tele inayoweza kuthibitishwa, sielewi anamaanisha nini katika neno "vishindo". Labda linaendeleza lile linalopatikana katika "kazi bora" ya vitabu vinavyotetea dosari na kasoro zilizomo katika vitabu vya Kikristo iliyomo katika kitabu kiitwacho "Is Bible Reliable." (Je, Biblia inaaminika?).

Katika kitabu hiki, mwandishi Bjug Horstal anasema kwamba Mungu "aliwashawishi" waandishi wa Maandiko Matakatifu "- - - kuandika kasoro na dosari zilizoambatana (zinazotokana) na lugha , na kwamba tunatakiwa tuliache jambo hili kwa Mungu mwenyewe, awe huru kutumia idadi yoyote ile ya fani na hata udhaifu wa kibinadamu kama anavyotaka mwenyewe - - -".12

Mashahidi wa Yehova wameandika kitabu kizima kiitwacho: Bible: God's Word or Man's? (Biblia: Ni neno la Mungu au la Mwanaadamu?), ambacho kinazungumzia kasoro na dosari zilizomo ndani ya Biblia. Katika kitabu hiki, wamelizungumzia suala hili kwa namna tofauti na ya pekee kwa kusema kwamba: 'kuna baadhi ya "kasoro na dosari za wazi" katika Biblia ambazo "ni vigumu kuzitetea". Hata hivyo tusizichukulie dosari na kasoro hizi kuwa ni kugongana na kupingana kwa aya za Biblia; mara nyingi ni kwa sababu ya ukosefu wa taarifa na habari kamili.13

Nilibahatika kupata nakala ya tafsiri ya Biblia ya Mashahidi wa Yehova "The New World Translation of the Holy Scriptures". Nilimuuliza mjumbe mmoja wa ngazi za juu wa jopo la Wafasiri wa mjini petu kuwa ana maelezo gani juu ya aya ya Mathayo 17:21, ambayo inasomeka: "Hakuna aya, kuna namba tu mstari mrefu ulio wazi". Mjumbe yule alibabaika sana alipoangalia sehemu hiyo. Akaahidi kuwa angekuja kuniona kwa mara nyingine tena ningependa kujua anasemaje kuhusiana na suala hili.

Kwa kifupi, Wakristo hawako tayari kuukubali ukweli kwamba Maandiko yao Matakatifu yamepotolewa kwa madai kwamba, ikiwa msingi utayumba na kutokuwa na uhakika, je, tutasimama juu ya nini katika siku za masaibu na mashaka?"14

Sio hayo tu, bali kuna aya inayozungumzia juu ya kuyabadilisha maandiko matakatifu katika maandiko hayo hayo:

" - - - ikiwa mtu yeyote ataongeza (au kufuta) neno lolote katika kitabu hiki, Mungu atamuongezea balaa zilizoandikwa katika kitabu hiki". (Ufunuo 22:18,19)

Ushahidi uko hapo, upo wazi na rahisi kwa kila mtu kuelewa. Ikiwa Mungu aliwaongoza kwa ufunuo kuandika vitabu vya Biblia, hakuna shaka kwamba wanadamu wameingilia na kubadilisha mambo mengi. Swali muhimu kabisa la kumuuliza Mkristo ni kwamba: Inawezekanaje kwa neno la Mungu kubadilishwa, kuondolewa na hata kutupiliwa mbali kwa matakwa ya mwanaadamu??

Msimamo wa Uislamu

Suala zima la wanadamu kubadilisha maneno (ufunuo) wa Mwenyezi Mungu ndio ilikuwa sababu ya Mtume Muhammad (saww) kuteremshiwa Qur'an: Ufunuo wa mwisho kwa Mjumbe wa Mwisho wa Mwenyezi Mungu.

Qur'an katika aya zake kadhaa inazungumzia juu ya kubadilishwa, kupunguzwa na hata kuondolewa kwa baadhi ya mambo katika Maandiko Matakatifu yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu kabla ya Qur'an. Baadhi ya aya ni kama vile.

" - - Walioruka mipaka (ya Mwenyezi Mungu) walibadilisha maneno kutoka katika yale waliyoteremshiwa". (Qur'an 2:59)

"Kundi moja miongoni mwao lilisikia Maneno ya Mwenyezi Mungu kisha likayabadili baada ya kuwa limeyaelewa (maneno hayo)". (Qur'an 2:75)

"Kuna sehemu (kundi) miongoni mwao ambao wanapotosha (wanakibadilisha) Kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kwa ndimi zao pindi wanaposoma ili ufikiri kuwa ni sehemu ya kitabu (cha Mwenyezi Mungu). Lakini sio sehemu ya kitabu; na wanasema Hayo yametoka kwa Mwenyezi Mungu lakini sio --". (Qur'an 3:78)

Aya hizi zinaonyesha ukweli mwingine kwamba, japokuwa Waislamu wametakiwa kuamini ufunuo ulioteremshwa kabla ya Qur'an, imani juu ya vitabu hivi - - Taurati, Zaburi na Injili - - inamaanisha imani juu ya ufunuo Halisi (Original) ulioteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu; na si yale tunayoyakuta katika Biblia zetu za leo, wala si ule uliopatikana katika zama za Nabii Muhammad (saww).

Imani ya Waislamu ni kwamba Qur'an ililetwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kuyasahihisha na kuondoa mambo yote yaliyoongezwa na kuyarejesha yale yaliyoondolewa kwa makusudi na wanadamu katika ufunuo wake wa awali. Mwenyezi Mungu aliweka wazi kwamba huu, Ufunuo wake Mwisho, hautapatwa na masaibu na balaa la kupotolewa (kubadilishwa) kama vitabu vilivyotangulia:

"Bila shaka, Tumeiteremsha Qur'an, na bila shaka sisi ndio tutakaoilinda kutokana na kupotolewa". (Qur'an 15:9)

Juu ya hili, Qur'an ina msimamo thabiti. Imebakia katika hali yake ya asili kama ilivyokuwa wakati ilipoteremshwa kwa Mtume Muhammad (saww). Na pia makaratasi yaliyoandikwa Qur'an juu yake yaliyoandikwa kwa mkono (Original Manuscripts) wakati wa Mtume bado yapo mpaka leo katika mji wa Madina, Arabia. Nakala ya Qur'an iliyoandikwa katika karne ya saba hii ni miongoni mwa nakala za mwanzo kabisa zinazoeleweka tulizonazo leo hii, na iliandikwa kwa mkono juu ya ngozi ya mnyama jamii ya swala miaka michache baada ya kutawaffu Mtume Muhammad (saww). Nakala nyingine iliyoandikwa katika karne ya saba iliyoandikwa katika zama za Khalifa wa tatu, Uthman, ipo katika jumba la makumbusho la Topkapi, Istanbul, Uturuki. Ikiwa mtu atachukua Qur'an iliyo katika lugha ya kiarabu kisha akajaribu kulinganisha na nakala hizi zilizoandikwa katika karne ya saba hatakuta tofauti (khitilafu) yoyote.

Qur'an iliyo katika lugha ya kiarabu haijabadilishwa, kupunguzwa wala kuongezwa lolote licha ya kupita miaka zaidi ya 1400. Kutokana na hili, hakuna uthibitisho bora kuliko huu juu ya kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu kuwa atailinda Qur'an dhidi ya mikono ya watu (kupotolewa), ambayo ni ufunuo wake wa mwisho.

Kuhusiana na waanadamu kuyabadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu, Qur'an inasema:

"Na wasomee na uwafundishe yale yaliyoteremka kwako katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, hakuna atakayeweza kuyabadili Maneno yake na hamtapata msaidizi mwingine yeyote badala Yake (Mwenyezi Mungu)". (Qur'an 18:27)

  • 1. The Bible, The Qur'an and Science, p. 44. (Biblia, Qur'an na Sayansi, uk. 44.)
  • 2. Ibid, p. 109. (Kitabu hicho hapo juu).
  • 3. All Scripture Is Inspired of God and Beneficial, p. 195. (Maandiko yote yametoka kwa Mungu na ni yenye Manufaa, uk. 195).
  • 4. Is the Bible Reliable? p. 30. (Je, Biblia inaaminika? uk. 30)
  • 5. Awake! p. 26 (Amka! uk. 26)
  • 6. The Bible, the Qur'an and Science, p. 41. (Biblia, Qur'an na Sayansi, uk. 41)
  • 7. Ibid, p. 57. (Kitabu hicho hapo juu)
  • 8. Is the Bible God's Word? pp. 1,2 (Je Biblia ni Neno la Mungu? Uk. 1,2)
  • 9. Jesus and the Four Gospels, pp. 6,7. (Yesu na Injili nne, vitabu vinne vya injili, uk. 6,7)
  • 10. Is the Bible God's Word?, p. 1. (Je Biblia ni Neno la Mungu, uk . 1)
  • 11. Personal Communication, Del Kingsriter of Centre for Ministry to Muslims, March 3, 1993. (Mawasiliano ya mtu binafsi).
  • 12. Is the Bible Reliable? pp. 86, 87. (Je biblia inaaminika? Uk. 86, 87).
  • 13. The Bible: God's Word or Man's? p. 97. (Biblia ni neno la Mungu au la Mwanadamu? uk. 97).
  • 14. Is the Bible Reliable? p. 84. (Je Biblia inaaminika, uk. 84).

Imani Halisi Ya Kumuamini Na Kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja Imehuishwa

"Kwa hiyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na litapewa taifa jingine lenye kuzaa matunda". (Mathayo 21:43)

Wafuasi wa Yesu walifurahia sana maelezo haya wakiamini kuwa wao ni "Watu wateule" wapya wa Mungu. Hata hivyo, ukristo unaendelea kupotea kutoka katika njia iliyonyooka.

Mpaka kufikia karne ya nne, ukristo ulikuwa umejiimarisha vizuri kama dini, imani na misingi yake ilipangwa vizuri hasa kwa vile ulikuwa ndio Hukumu na mwongozo wa Maandiko kwa wafuasi wake.

Kama tulivyoona hapo awali, mafundisho sahihi ya Yesu yalikuwa yamesahauliwa na badala yake yakafuatwa mafundisho ya Paulo wa Tarsus. Imani na mila za kipagani ziliingizwa katika Ukristo na Paulo ili apate wafuasi miongoni mwa Watu wa mataifa (Gentiles) waliokuwa wapagani wa zama zake, imani na misingi yote ya Kikristo imetokana na upagani (ukafiri). Kwa kadri wapagani walivyokuwa wakiingia katika Ukristo kwa wingi zaidi, ndivyo imani zaidi za kipagani zilivyokuwa zikiingia zaidi katika Ukristo.

Sikukuu zote za kikafiri (kipagani) zilihamishiwa katika Ukristo: Siku ya kuzaliwa mungu wa wapagani (sanamu) aliyeitwa Mithras ambayo ilikuwa tarehe 25 Desemba (mwezi wa 12). Alifanywa kuwa ndiyo siku ya kuzaliwa Yesu ambapo pia vitendo vya ibada hii ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu vilichukuliwa kutoka kwenye vitendo vya sherehe za Warumi za kusherehekea kuzaliwa Saturn.
Sherehe hizi zilifahamika kwa jina na Saturnalia. Sikukuu ya wafu (wa kipagani) ilifanywa kuwa ni siku ya watakatifu wote; siku iliyotengwa kwa ajili ya kusherehekea kufufuka kwa mungu wa kisanamu aliyeitwa Attis, ilifanywa kuwa ndio siku ya kufufuka kwa Yesu, ambayo pia vitendo vingi vya sherehe hii vilichukuliwa pia kutoka kwenye upagani kwa madhumuni yale yale.

Sabato ya Wayahudi, iliyopangwa na Mungu kuwa iwe siku ya saba ya wiki katika sheria ya Musa, ilibadilishwa na Ukristo na kufanywa kuwa ni siku ya kwanza (yaani badala ya Jumamosi kuwa siku ya saba ilifanywa kuwa ni siku ya kwanza). Jumapili ikajadiliwa kuwa ifanywe kuwa ndio siku aliyofufuka Yesu, lakini lazima ikumbukwe kwamba Jumapili ilikuwa ni siku ambayo Mungu wa kisanamu, Mithras, "aliliteka jua".

Dhana ya Ukristo juu ya masuala ya ngono (sexuality) na ndoa iliathiriwa sana na mila za kipagani zilizokuwa katika dini na falsafa za kipagani za "Neoplatonism", Stoicism na Gnosticism (utawa). Dini zote hizi ziliamini kuwa kujamiiana (ngono) hata ndani ya ndoa ni jambo ovu sana, na kwamba kutooa na kuto-olewa ni sifa kubwa na nzuri sana ambazo kila mtu inambidi ajitahidi kuzipata. Ukristo kwa moyo mkunjufu uliyachukua mawazo haya na hivyo kumuweka mwanadamu na familia kwa ujumla katika hali isiyokuwa asili yake na ambayo ni tofauti na maumbile yake na ambayo kamwe Mungu hakuamrisha hivyo.

Vitendo vya ibada na imani za kipagani zilizoingizwa katika ukristo zilikuwa zinawakera na kuwapa taklifu kubwa wamishenari wa kikristo wa mwanzo, hasa kwa vile mila na tamaduni hizi zilikuwa zimeimarika mno ambapo kwamba ilikuwa haiwezekani kuziondoa kwa namna yoyote ile. Katika mwaka 598 B.K., Papa Gregory, the Great, aliwasaidia mapadri kwa kuwaambia kwamba wanatakiwa kuwaruhusu watu kufuata mila na imani zao za zamani, isipokuwa tu hili linatakiwa "likusudiwe" katika "kumsifu" Mungu. Kwa hiyo watu waliendelea na imani zao katika uchawi, kurogana, mizuka, n.k. kwa vile mapadri waliwaambia kuwa udanganyifu huu ulikuwa ni "kudhihirika" kwa shetani. Watakatifu na "warithi wa watakatifu" walihimizwa zaidi, kwa vile wao waliaminiwa kuwa na nguvu za kumfukuza shetani.

Ukristo, ukiwa umeelemewa na idadi kubwa ya imani na desturi za kikafiri (kipagani) pamoja na kumtambua Yesu -- badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio kiini cha imani yao; ulikuwa umebakia kuwa ni uchafu tu usiokuwa na lolote isipokuwa uchafu.

Haja ya Mtume Mwingine

Wayahudi walipotelea katika vitabu vyao vya sheria; Wakristo walipotea kutokana na kumfanya kwao Yesu kuwa ni Mungu. Mwenyezi Mungu aliamua kumpa mwanadamu nafasi moja ya mwisho ili kuirejesha na kuihuisha imani halisi ya kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja tu asiyekuwa na mshirika.

Nabii Ibrahim, kama ilivyodokezwa katika sura ya kwanza alikuwa na watoto wawili wa kiume Is-haq na Ismail ambaye ndiye aliyekuwa mkubwa kwa Is-haq. Mungu alipoweka agano lake na Ibrahim kuhusiana na Is-haq, alikuwa pia na maneno kidogo ya kuzungumzia juu ya Ismail:

"Na kuhusiana na Ismail, Nimekusikia: Tazama Nimembariki, (nitamzidisha) nitauzidisha uzao wake; atazaa Maseyyid kumi na wawili (Maimamu kumi na mbili ) na Nitamfanya kuwa taifa kubwa". (Mwanzo 17:20).

Agano Lililofanywa kwa Ismail Limetimia

Ismail na mama yake walikaa Uarabuni ambapo waliishi na kuendelea, kwa kadri miaka ilivyokwenda, ndivyo walivyozidi kuwa taifa kubwa lililokuwa limebashiriwa na Mwenyezi Mungu. Katika mwaka 610 B.K. ahadi ya Mungu ya kukibariki kizazi chake (Ismail) ilitimia, wakati mmoja wa kizazi chake, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 40 aliyeitwa Muhammad (saww) alipoitwa na Mwenyezi Mungu ili kuleta ujumbe wake kwa wanaadamu wote.

Agano ambalo Mungu aliweka na Ibrahim sasa lilikuwa limekamilika, na uimarishaji wa imani halisi ya kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika (pure monotheism) -- Uislamu, au kujisalimisha na kujinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu Mmoja -- ulikuwa katika njia yake ya kubadilika kutoka kwenye ndoto kuwa kweli.

Kwa hakika baraka alizopewa Ismail zilikuwa kubwa kabisa kwani Mtume Muhammad alishuhudia katika kipindi cha maisha yake Uislamu thabiti kabisa ukisimama na kuimarika, na aliuleta ujumbe wa Mwenyezi Mungu katika mfumo ambao umeuwezesha kubakia bila kuharibiwa wala kubadilishwa hadi leo hii.

Misingi ya Uislamu ni misingi ya kuaminika na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika: Ibada ya Mwenyezi Mungu na Mungu peke yake, na utii wa sheria yake. Kwa mara nyingine imani ya kumuamini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja ilirejeshwa na kuimarishwa.

Ukristo Na Uislamu

Kwa namna yao ya kufikiri, Mungu aliwafanya Wayahudi kuwa ni watu wake wateule. Kwa hadhi hii waliyopewa Wayahudi, ilimanisha kwamba ni wao tu (Wayahudi) waliotengwa na Mungu kwa ajili ya kuteremshia ufunuo na kupata Mitume wa Mungu kutoka miongoni mwao. Kwa hiyo Wakristo wanahisi kwamba wanaweza kumwamini tu Mtume ambaye ni Mwisraeli, na kwamba wengine wote ni walaghai.

Uislamu unawaletea Wakristo suala jingine kwa ajili ya mjadala. Mara tu baada ya kuanza kuenea kwa kasi kwa Uislam muda mfupi baada ya kuondoka duniani Mtukufu Mtume Muhammad (saww), Wakristo walianza kueneza ukweli kwamba mtu mmoja kutoka Uarabuni ni kweli kwamba alikuwa na ujasiri wa kwenda na kuzunguka maeneo mbalimbali akidai (tangaza) kuwa yeye ni Mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Licha ya Uislam kusisitiza kwamba ingekuwa kinyume na busara na uadilifu wa Mwenyezi Mungu kuteremsha Mitume kutoka katika taifa moja tu, lakini bado wakristo hawakutaka kusikia. Mtume Muhammad hakuwa Myahudi, kwa hiyo mbele ya macho yao, alikuwa ni mtume wa uongo aliyekuja na ushuhuda wa uongo kutoka kwa Mungu wa Uongo.

Awali, mashambulizi ya Wakristo dhidi ya Uislam yalikuwa ni manung'uniko madogo madogo. Baada ya Khalifa wa Ukoo wa Fatimid aliyeitwa Hakim kuyavunja makaburi ya Wakristo Jerusalem katika mwaka 1010, manung'uniko yalibadilika na kuwa ngurumo za simba. Wazungu Ulaya walianza kuishi kwa hofu kubwa ya kuvamiwa na Waislamu, na hii ilikuwa ni sababu ndogo iliyoamsha chuki iliyokuwa imerundikana kwa muda mrefu. Papa Urban II alipoitisha vita vitakatifu "Crusades" mnamo mwaka 1095 ili kuikomboa Ardhi Takatifu kutoka kwa "makafiri", kampeni ya chuki dhidi ya Uislam ilianza kwa kasi ya roketi, ambapo ilifikia kilele chake katika karne ya kumi na mbili.

Katika mashambulizi yao ya maneno dhidi ya Uislam; mambo mengi maovu ya aibu na ya uongo yalipakwa rangi ya ukweli na wale waliodaiwa kuwa ni "wasomi na wanazuoni" wa wakati ule na yakasambazwa kwa wingi kwa karibu watu wote.
Mtume Muhammad (saww) alichukuliwa kuwa ni adui wa Kristo, mtume wa uongo, mwenye kujifaharisha na kujisifia sana, mtawala wa kimabavu, mwenye tamaa nyingi za kimwili, na mengine mengi.

Qur'an ilidaiwa kuwa ni mkusanyiko wa hotuba, maneno ya kipuuzi na yasiyokuwa na maana na kwanza ni "kitabu kinachotia uvivu" kusoma kutokana na kilivyoandikwa mpangilio mbaya na mvurugiko usioweza kueleweka. Mbele ya macho ya Wakristo wa Medievo (yaani walioishi kati ya mwaka 1100 - 1500 B.K), Qur'an haingewezekana kwa namna yoyote ile kuwa ni Maneno ya Mwenyezi Mungu kwa sababu Muhammad alikuwa ni mtume wa uongo. Kwa hiyo walidai kuwa Mtume (saww) aligushi (aliandika mwenyewe).
Kisha akadai kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu. Waliendelea kudai kwamba hakuna ufunuo wowote ulioteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa yalikuwa ni maneno ya kuweweseka ambayo Mtukufu Mtume Muhammad (saww) alikuwa anayasema alipokuwa anabanwa na kifafa, ambayo yeye (Mtume saww) alidai kuwa ni ufunuo.

Dini ya Uislam ilionekana kuwa si chochote isipokuwa ni upotofu na kwamba ni mafundisho yenye makosa, mafundisho yaliyochukuliwa kutoka katika Ukristo. Uislam ulichukuliwa kuwa ni dini ya upanga, na katika jitihada zao za kulichafua jina la Uislam, wakaupachika jina la "Mohammedanism" (yaani dini iliyoanzishwa na kuletwa na Muhammad (saww) badala ya Mwenyezi Mungu.)

Waislamu pia hawakunusurika na ghadhabu hii ya Wakristo wa Medievo (Wakristo walioishi miaka ya 1100 - 1500 B.K) ambao waliwaita (Waislam) makafiri, wapagani, mabedui wa jangwani na wafuasi wa Muhammad (Muhammedans).

Kwa sababu ya kutotaka kwao kuukubali Uislamu, Wakristo wakawa maadui dhahiri wa Uislamu na Waislamu. Katika mashambulizi yao ya maneno, viongozi wa kanisa walitumia mbinu mbalimbali katika hila zao za kuudhuru Uislam; kama vile kuelemea upande mmoja katika hoja zao, upotoshaji, kutafsiri vibaya kwa makusudi, kubuni mambo ya uongo ili kuwashambulia n.k. Wakati haujabadili hali ya mambo, kwa bahati mbaya; zama za vita vitakatifu dhidi ya Uislamu "Crusades" zimepita siku nyingi lakini wakristo bado hawawezi kuukubali Uislamu. Wakristo wa zama hizi, wanatumia mbinu mpya ili kukabiliana na kile wanachokiona kuwa ni "hatari" ya uislamu.

Jitihada za Wamishenari

Matumizi ya nguvu dhidi ya Waislamu ambayo kilele chake ilikuwa ni vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (crusades) yaliungana na jitihada za wamishenari kwa upande wa wakristo katika jitihada zao za "Kuwarejesha makafiri kwa Bwana". Jitihada hizi za wamishenari, hata hivyo zilipata mafanikio kidogo sana licha ya muda wote na fedha zilizotumika kwa mamia na mamia ya miaka ambapo jitihada hii imekuwa ikiendelea.

Jitihada za mwanzo katika kujaribu kuwabadili Waislamu kuwa Wakristo zilikuwa malumbano / mabishano kama yale yaliyotumika kwao, Waislamu walikataa kuyasikiliza malumbano hayo. Uzoefu umewaonyesha Wakristo kwamba matusi hayasaidii kitu, kwa hiyo jitihada za wamishenari wa Kikristo wa zama hizi zimechukua mwelekeo mpya kabisa. Wamejiwekea sera mpya ya "kuwahubiria Waislamu kwa upendo."

Nchini Marekani kuna taasisi moja inayoitwa "Center of Ministry to Muslims" (CMM), kituo cha Mahubiri kwa ajili ya Waislamu, taasisi hii imeandaa mpango maalumu (kifedha na kielimu), unaokusudia kufikisha ujumbe wa Ukristo kwa Waislamu. Malumbano (mabishano) hayatumiwi lakini bado njia zinazotumiwa sio za uadilifu kama vile upotoshaji, kutafsiri vibaya kwa makusudi hata kuzua mambo na habari za uongo. Ukweli juu ya Ukristo umefunikwa kwa utando wenye sukari, na taasisi hii (CMM) unawalenga Waislamu ambao wako peke yao katika nchi hii, bila msaada wa maadili ya familia na marafiki wa kiislamu.

Moja ya jitihada za CMM zinazofurahisha ni gazeti lao la "Noor ul Haq" au "Nuru ya ukweli". Gazeti hili linachapishwa kwa Kiingereza na Kiarabu muundo (format) wake una sura ya kuwa gazeti la kiislamu, lakini ilivyo ni gazeti la kikristo linalokusudiwa kuwafikia Waislamu. Linatumia misamiati ya Kiislamu na aya za Qur'ani, lakini uangalifu ni muhimu sana hapa kwa vile aya hizi za Qur'an zinapotoshwa na kutafsiriwa tofauti na zilivyotafsiriwa na Mtume (saww), ili kuwamezesha Waislamu mafundisho ya kikristo. Kwa Muislamu mwenye elimu ndogo ya dini, ni rahisi kupotoshwa na mafundisho haya.

CMM ni tasisi ndogo sana ikilinganishwa na "Zwemer Institute For Muslim Studies" (Tasisi ya Zwemer kwa ajili ya mafunzo ya Uislamu). Taasisi hii yenye kituo chake California, ambayo imechukua jina lake kutoka kwa mmishenari raia wa Netherlands ambaye alitumia takriban miaka hamsini katika kipindi cha mwanzo cha karne hii kuwahubiria Waislamu katika Mashariki ya Kati, huwafundisha Wakristo mbinu za kuwahubiria Waislamu. Wanafunzi katika taasisi hii wanajifunza Kiarabu, Historia ya Uislamu, Utamaduni wa kiislamu na imani ya Uislam na utekelezaji wake. Watu hawa wamejizatiti kwelikweli, na sio wajinga wa Uislamu kwa namna yoyote ile. Wamefundisha na wamekubali kuuchukia Uislamu lakini sio kwamba hawajui Uislamu.

Hii ni jitihada kubwa kabisa. Wahubiri (daiya) wanafunzi na wamishenari wanaoandikishwa katika taasisi hii huchukua aina zote za mafunzo juu ya Uislamu. Kuna zaidi ya haya. Pia kuna semina fupi zinazotolewa kwa vikundi vya kanisa vinavyopendelea (kufanya hivyo), na taasisi ina kituo cha uchapaji ambacho huchapisha majarida, vitine (pamfleti), vitabu na hata filamu na kanda za video.

Ni taasisi nzuri sana kwa Wakristo, lakini ni hatari sana kwa Waislamu. Wamishenari wa Kikristo wanaotoka katika taasisi hii hawajaribu hata kidogo kuonyesha kuwa Uislamu "ni rundo la kasoro na dosari". Wanajaribu kuonyesha kuwa Uislamu una "vipande vya ukweli ambavyo havikuunganishwa", na kutoka hapa, wanajaribu kumshawishi Mwislamu kwamba vipande hivi vya ukweli vimeunganishwa na kuwa kitu kizima katika Ukristo. Mashambulizi ya maneno sasa hivi yameachwa na baadala yake wanajaribu kujenga mashaka katika nyoyo za Waislamu juu ya imani yao. Wakristo wana matumaini kwamba mashaka haya baadaye yatasababisha kutoridhika, ambako kutapelekea kuhama kutoka kwenye Uislamu kwenda kwenye Ukristo.

Wamishenari wa Kikristo wanaangalia kwa furaha kabisa migogogro iliyomo ndani ya ulimwengu wa Kiislamu leo hii. Taasisi ya Zwemer inawaambia watu wake kuwa:

"Kuhamahama na ukimbizi (unaosababishwa na migogoro) pamoja na kuvurugika kwa maisha ya kawaida kumesaidia kuvuruga utamaduni wa zamani na umeleta uwazi mpya miongoni mwa Waislamu katika kusikia habari njema za Yesu kristo. Imani ya zamani kwamba Uislamu una nguvu isiyoweza kushindwa sasa hivi haina nguvu tena".1

Tarakimu zinazotolewa na Taasisi ya Zwemer kuwa ni ya Wakristo wapya bila chembe ya shaka yoyote zimekuzwa. Hii ni kwa sababu ikitajwa idadi ya ndogo ya Wakristo wapya itakuwa vigumu kupata wanafunzi na fedha za kutosha kwa hiyo wanalazimika kutoa tarakimu kubwa ili ionekane kuwa "mti" wa Ukristo unazaa matunda.

Kwa kadri Uislamu unavyoendelea kukua, mashirika kama CMM na Taasisi ya Zwemer ndivyo yanavyopata nguvu na kujizatiti zaidi. Huu sio wakati kwa Mwislamu kukaa na kulipuuza hili. Siku moja litakuja mpaka mlangoni pake, lazima ajiandae, lazima awe na imani thabiti, na ni lazima mjue jamaa yake (ukristo) ili asitetereke katika imani yake.

Kampeni Dhidi ya Chuki

Ingawa mashirika kama "CMM na The Zwemer Institute" yanatangaza "kuwafikia na kuwahubiria Waislamu kwa upendo", nyuma ya migongo yao kuna mbinu nyingine (ambayo haitangazwi) ambayo hutumiwa mara nyingi katika kuudhibiti Uislamu. Ni mbinu iliyoanza zama za vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (Crusades) na mbinu hiyo kamwe haijafa kifo halisi. Mbinu hii inayotumika katika hila zao za kuudhuru Uislamu imepewa jina la "Vita vitakatifu vya kiakili dhidi ya Uislamu''. Mashambulizi haya ya mdomo dhidi ya Uislamu ni maendelezo ya kazi iliyoanza miaka zaidi ya 900 iliyopita ambapo Papa Urban II alihamasisha vita vitakatifu dhidi ya "makafiri" wa Mashariki ya kati alipokuwa akihutubia umati wa watu katika mji wa Clemont.

Ushahidi kwamba kampeni hii ya chuki dhidi ya Uislamu bado inafukuta unaweza kuonekana katika maduka ya vitabu - hususan maduka ya Wakristo - na katika maktaba za umma (public libraries).

Wale wanaojiita "Wataalamu bingwa wa historia, utamaduni, dini" (Orientalists) katika karne ya kumi na tisa na ishirini, wameandika mambo mengi ya kuchukiza juu ya Ulimwengu wa Kiislamu: Mifano mizuri ni kama vile "Story of Civilization" (Simulizi juu ya ustaarabu) kilichoandikwa na Durant. "The Decline and Fall of the Roman Empire" (Kudidimia na Kuanguka kwa Dola ya Urumi) kilichoandikwa na Gibbons. "Inside Asia" (Ndani ya Asia) kilichoandikwa na Gunther. "The Outline of History" (Dondoo za Historia) kilichoandikwa na H. G. Welles -- ambavyo vyote vinahesabiwa kuwa ni vitabu "vyenye ubora wa kiwango cha juu kabisa" katika ulimwengu wa historia.
Uelemeaji upande mmoja katika uchambuzi wa hoja na uadui umetapakaa katika maeneo yote na katika kila kona. Mtu anaweza kushangaa na kujiuliza vipi watu hawa wajizatiti kulisoma eneo fulani la ulimwengu, eneo ambalo wana chuki kubwa sana dhidi yake. Hata kitabu cha hivi karibuni cha Albert Hourani ambacho kimesifiwa sana kiitwacho "A History of the Arab Peoples" (Historia ya Waarabu) kimejaa uelemeaji upande mmoja katika uchambuzi wa hoja na uadui dhidi ya Uislamu.

Cha ajabu ni kwamba hawa wanaodaiwa kuwa wanapiga vita chuki dhidi ya Uislamu ni Wakristo wenye imani kali. Angalia kwa mfano kitabu "Islam Revealed" (Uislamu wawekwa wazi) kilichoandikwa na Mkristo wa Kiarabu mwaka 1988. Nyuma ya kitabu hiki mwandishi anaahidi kuwapa wasomaji wake "Mtazamo" utakaowafungua macho juu ya imani hatari kama ukoma walivyonayo kila mtu mmoja katika watano hapa duniani (yaani imani ya Uislamu).
Mwandishi wa kimarekani Robert Morey, "anayedaiwa kuwa ni mwanazuoni (msomi) wa kimataifa" katika fani ya ulinganishaji wa dini mbalimbali - zaidi ya hili ni Mkristo mwenye msimamo mkali kidini - hivi karibuni ameandika kitabu kiitwacho "Islam Unveiled: The True Desert Storm" (Uislamu waachwa wazi: Kimbunga (Dhoruba) halisi cha Jangwani) alichokiandika mwaka 1991. Ndani yake anadai "Kuthibitisha" kwamba vitendo vyote vya ibada na imani za Uislamu zimetokana na Ukafiri (upagani) uliokuwepo kabla ya Uislamu. Dr. Morey pia huandaa kipindi cha redio (Radio show) ambacho ni maalum kwa ajili ya kuushambulia Uislamu. Hivi karibuni, katika kipindi hiki alisema: "- - - kama Muhammad angekuwa hai leo hii, bila shaka angechunguzwa kama mharibifu wa akili za watu, muuaji wa halaiki (ya watu,) na mdhalilishaji (mnyanyasaji) wa watoto".

Taarifa kama hizi ni mfano tu wa marundo na marundo ya taarifa zinazokusudiwa kujenga chuki zinazotolewa kila siku dhidi ya Uislamu na ambazo zinastahili kudharauliwa. Taarifa hizi zinakusudiwa kuimarisha na kueneza zaidi propaganda mbalimbali za chuki dhidi ya Uislam zinazoaminiwa na Wakristo walio wengi, na pia kuzidisha kutoaminiana na uadui, inawezekana vipi watu wakahubiriana kirafiki na kwa upendo na ilhali akili za watu zinashindiliwa takataka kama hizi?

Kwa kadri Uislamu unavyoendelea kukua na kuenea, ndivyo mashambulizi haya yatakavyozidi kuongezeka. Wakristo wanahofu, na hii ndiyo mbinu waliyoamua kuitumia katika kukabiliana na hofu hiyo. Ni mbinu ambayo imekuwa ikitumika kwa mamia ya miaka, na ni mbinu ambayo wametokea kuipenda sana. Badala ya kufungua milango ya mazungumzo juu ya tofauti za imani zao, wanafanya haraka kutumia jazba, hasira, na kujenga uadui.

Mbinu na Hila Nyingine Wanazozitumia Kuudhuru Uislamu

Mbali na vitabu, vitine (mapamfleti), vipindi vya redio, n.k. ambazo zimekusudiwa moja kwa moja kuudhuru Uislamu, pia kuna hila nyingine za chini chini zinazofanywa na Wakristo kupitia kwenye kazi za fasihi na zisizo za fasihi (fiction and non-fiction), pamoja na televisheni na mikanda ya video ambapo huuonyesha Uislam na Waislamu kuwa ni kundi chokozi la ugaidi na wagaidi.

Vitabu ni pamoja na "The Source" (chanzo) kilichoandikwa na James Mitchner na kingine cha hivi karibuni "The sum of All fears" (Jumla ya hofu zote) kilichoandikwa na Tom Clancy. Pia kuna vitabu vingine vinavyopotosha kama vile: "Jihad", "The Holy Sword" (Upanga mtakatifu) na "Sacred Rage" (Hasira Takatifu).

Kitabu kingine kinachoonyesha uadui mkubwa ni "Holy of Holies" (mtakatifu wa watakatifu); ambacho kinaelezea jinsi Wafaransa kwa msaada wa Warusi na Waisraeli, wanavyoharibu Msikiti Mkuu (Msikiti mtakatifu) wakati wa hijja. Na bila kusahau kitabu cha kikafiri cha Salman Rushdie, "The Satanic Verses". Mwandishi wa kitabu hiki, Salman Rushdie, amekuwa akieleza mara kwa mara kwamba nia yake haikuwa kuutukana Uislamu isipokuwa majina ya watu na majina ya sehemu (mahali) aliyoyatumia katika kitabu chake yamegongana mno na majina ya watu watukufu na sehemu tukufu za kiislamu kiasi kwamba inakuwa vigumu kuamini maneno yake.

Kashfa zinazofanywa dhidi ya Uislamu kupitia kwenye televisheni zinasikitisha. Katika kipindi cha kiangazi cha mwaka 1991, kulikuwa mfululizo wa midahalo (debates) iliyofanywa baina ya Waislamu wawili na Wakristo wawili kuhusiana na tofauti za dini zao. Midahalo sita ilionyeshwa kwenye televisheni kwa wiki (majuma) kadhaa juu ya injili. Na waislamu walifanya kazi nzuri sana ya kuwakilisha imani yao, hata mbele ya maadui dhahiri kutoka pande zote, ikiwa ni pamoja na msimamizi wa mdahalo, wazungumzaji wawili wa upande wa imani ya Kikristo, na hata hadhira ya wakristo.

Hata hivyo, waandaaji wa kipindi hiki cha televisheni walifanikiwa kupata walichokitaka, kwanza walibadilisha kanda za matangazo ili kuwaonyesha Waislamu katika mwanga mbaya. Pia walitoa kijitabu kuhusiana na mdahalo kwa ajili ya wasomaji wa majumbani ambacho walikipa jina "The facts on Islam" (Ukweli juu ua Uislamu). Jina lenye kufaa zaidi kwa kijitabu hiki lingekuwa "Mambo ya uongo na Fitna dhidi ya Uislamu" (Fallacies of Islam), kwa vile ndani ya yake kuna ukweli kidogo sana, ndani yake kimejaa upotoshaji na uongo dhahiri dhidi ya Uislamu.

Kwa upande wa filamu kuna "Black Sunday" (Jumapili Nyeusi) ambapo "Magaidi" wa kipalestina wanapanga njama za kuwaangamiza wale wote wanaohudhuria "Superbowl" (mashindano ya mwaka ya mpira wa miguu). Nyingine ni "Not Without My Daughter" (Si Bila Binti wangu ), filamu ambayo ianonyesha picha ya kutisha juu ya mahusiano ndani ya familia za Kiislamu.

Mambo na imani mbalimbali za uongo zinazodaiwa kuwa ni za Kiislamu zinapewa nguvu na kendelezwa kwa kutumia mbinu kama hizi. Uislamu una wakati mgumu kwani hautaonekana isipokuwa kwa dhana mbaya na ya uadui.

Sisi kama Waislamu, lazima tuwe thabiti pindi tunaposhambuliwa katika imani yetu - - ikiwa ni kwa "njia ya upendo" au uadui dhahiri. Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia katika Quran tukufu.

"Mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu, na mtasikia udhia mwingi kwa wale waliopewa kitabu kabla yenu, na kwa wale walioshirikisha. Na kama mkisubiri na kujilinda na aliyoyakataza Mwenyezi Mungu (mtakuwa mmefanya jambo) zuri; kwani mambo haya ni mambo makubwa ya mtu kuazimia kuyafanya". (Qur'an 3:186)

  • 1. Muslim Awareness Seminar Notebook, p. 5 ( Semina ya Kujenga Umakini wa Waislamu, uk. 5).

Madhehebu Katika Ukristo

Japo Uislamu pia umegawanyika katika makundi mawili ya Sunni na Shia, lakini mgawanyiko huu ni wa kisiasa, sio wa kidini. Katika Ukristo mgawanyiko ni wa kidini. Japo wote wanamuamini Mungu, lakini tusimsahau Yesu - - - mambo yanakhitilafiana kuanzia hapa.

Ingawa idadi kamili haieleweki, ninafahamu takribani madhehebu hamsini ndani ya Ukristo, tukianzia na wa - Amish, ambao wameamua kujitenga na ulimwengu na mambo yote yanayorahisisha maisha (ya kisasa) kama vile umeme na magari, na kumalizia na Unitarians ambao wanaonekana mbele ya wakristo walio wengi kuwa sio wakristo kwa sababu hawaamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu wala hawaamini utatu Mtakatifu.

Waromani Katoliki, ambao ni dhehebu la kikristo kubwa kuliko yote ulimwenguni leo, wanawatukuza watakatifu (saints) na mama wa Yesu. Mliwaji (yaani mkate) wakati wa kumunio inasemekana kwamba huwa ni mwili halisi wa Yesu, divai huwa ni damu halisi inapobarikiwa na padri.

Kwa sababu ya kutoridhishwa kwao na imani ya kutooa au kutoolewa (celibacy), kanisa la Orthodox lilijitenga kutoka Roma katika zama za kati (middle ages) na sasa hivi kanisa hili lina wafuasi wengi katika Ulaya ya Mashariki. Wanaendelea na mapambo katika makanisa yao kama yale ya kanisa katoliki lakini wana sikukuu tofauti na wanaapa kiapo cha utii kwa "Baba Mtakatifu" mwingine asiye kuwa Yule wa Roman Katoliki.

Mnamo mwaka 1517, kanisa la kiprotestanti lilianzishwa, kwa sababu ya kutokubaliana na baadhi ya mambo (vitendo) ndani ya kanisa katoliki. Baadhi ya mambo hayo ni:

1) Wakatoliki wanapamba na kuyanakshi makanisa yao. Waprotestanti wanayafanya kuwa rahisi.

2) Maandiko Matakatifu ya Wakatoliki yanajumuisha vitabu vya "Apocrypha" (vitabu vilivyofichikana). Waprotestanti hawakubali kitabu chochote katika vitabu hivi.

3) Wakatoliki wana vinyago katika makanisa yao, majumba yao, katika magari yao. Pia wanavichimbia vinyago hivi mbele ya bustani za nyumba wanazotaka kuziuza, na wa misalaba iliyopambwa kwa umbo la Yesu akiwa amesulubiwa. Waprotestanti wanashutumu jambo hili kuwa ni "ibada ya masanamu" kwa hiyo wengi hawana hata msalaba mtupu (usiokuwa na sanamu ya Yesu) ndani ya makanisa yao.

Ndani ya tawi hili la Ukristo la Kiprotestanti kuna madhehebu mengine lukuki (mengi sana).

Walutherani wanafuata mafundisho ya Martin Luther. Baadhi ya Wakristo kutoka katika makanisa yaliyofanya Mageuzi (Reformed Churches). Hata hivyo waliona kuwa Martin Luther hakuwa mwangalifu na makini vya kutosha, hivyo waliamua kufuata mafundisho ya John Calvin.

Wa-Baptisti, ambao wanaamini kuwa watu wazima - - sio watoto - - ndio wanaotakiwa kubatizwa, waliuawa kikatili na wakatoliki na Waprotestanti katika Zama za Kati (Middle Ages) lakini sasa hivi wamekuwa miongoni mwa madhehebu makubwa ya Ukristo.

Kamwe Wakatoliki hawakuwa wa pole kuhusiana na harakati za Waprotestanti, na lilikuwa ni hitajio la uhuru wa kidini lililowahamisha Wazungu kutoka miji yao na kwenda katika nchi za ugenini. Wa-puritan walipohamia Amerika, katika karne ya kumi na saba, kundi zima la madhehebu ya kikristo lilianza kuwepo katika miaka michache iliyofuatia.

Wa-shaker walikuwa na imani kali juu ya imani ya kutokuoa (ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu). Dhehebu hili leo limeshakufa (kutokana na ubovu wa imani na misingi yake).

Wapentekoste wanadai "kuzungumza kwa ndimi" (kuzungumza kwa Roho mtakatifu). Huduma zao za kanisa inasemekana zinafurahisha sana. Pia wanaamini kuwa Biblia ndani yake haina makosa hata kidogo - - - yaani haina kasoro au dosari japo ile ndogo kabisa. Kutokana na nyadhifa zao tumekuja kuwajua watu "maarufu" kama akina Jimmy Swaggert, Jim na Tammy Fay Bakker.

Mashahidi wa Yehova wanatumia muda wao mwingi kutafakari kitabu cha Ufunuo, wakiiota siku ambayo kila na mtu na kila kitu kitakhiliki (kitaangamia) isipokuwa wao.

Wa-Mormon walikuwa na mtume wao, Joseph Smith, ambaye aliwaletea kitabu cha maandiko ambacho wanaamini kuwa ni kitakatifu kama Biblia. Sera yao ya "ndoa za mbinguni" (yaani wake wengi bila mpaka) ilipelekea mwisho wa kuendelea kufanywa kuwa taifa (state) katika nchi hii.

Wanasayansi wa kikristo pia wana kitabu chao cha Maandiko mbali na Biblia; Mary Baker Eddy, mtume wao (wa kike) aliwaambia wafuasi wake kuwa imani na sayansi hushinda vyote - - - hata matamanio ya ngono (sexual desires).

Madhehebu mengi tofauti tofauti yakiwa na vitendo vingi tofauti tofauti, yote yameungana na kukubaliana kwamba imani yao ya Ukristo ndiyo "imani pekee ya kweli". Kiapo hiki cha kishahidi kwenye dini imekuwa ndio sababu ya matukio mengi ya ukatili na utumiaji wa nguvu usioelezeka dhidi ya wale wenye imani tofauti na hii. Matukio haya ni kama vile vita vitakatifu dhidi ya Uislamu (crusades). Upelelezi na hata Maangamizi ya moto ya Nazi (Nazi Holocaust). Kutovumiliana ni kitu chenye kutisha sana na hasa kunapotokana na ushabiki.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia waislamu kuwa:

"Shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarakiane". (Qur'an 3:103)

Ni lazima:

"Subirini na muwashinde makafiri, na kuweni imara (nyoyo zenu) na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu". (Qur'an 3:200)

Kwa sababu:

"Yeyote anayejinyenyekesha kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu, na akafanya mambo mazuri, kwa hakika ameshika kishiko imara kisichokuwa na kukatika: na mwisho wa yote ni kwa Mwenyezi Mungu". (Qur'an 31:22)

Hitimisho

Katika kitabu chake "Basic Christianity" (Ukristo wa Msingi) mwandishi John Stott anasema:

"Kimsingi Ukristo ni Kristo. Nafsi na kazi ya Yesu ni jiwe la msingi ambapo juu yake imejengwa imani ya Ukristo. Na kama siye alisema kuwa ni yeye (ikiwa sio yeye aliyejitangaza kuwa ni Yesu kristo). Na kama hakufanya yale aliyosema alikuja kufanya, jengo zima la Ukristo litaporomoka na kuanguka chini".1

Mtume Muhammad, baada ya miaka ya mapambano dhidi ya Wayahudi wa Madinah juu ya masuala ya dini, alisema thiolojia ni upuuzi wa kitoto - - adui wa dini. Uislamu, tofauti na mifumo mingine, ni dini rahisi ambayo haikuzikwa katika vichaka vya ububusa visivyokubaliana na akili na mantiki. Hakuna kundi la watu wanaoshughulika na masuala ya dini peke yake (clergy), hakuna madaraja ya dini, wala hakuna Sakramenti. Thiolojia haina nafasi katika Uislamu, kwa vile Uislam ni njia kamili ya maisha, na sio rundo la maneno tu.

Licha ya kwamba Uyahudi ulikwenda mrama katika sherehe (fafanuzi) za vitabu vyao vya sheria lakini bado wanayo imani ya msingi na kuu kabisa kuwa Mungu ni mmoja.

Uislamu una maana kujinyenyekesha chini ya taa na milki ya Mwenyezi Mungu, imani ya kuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu asiyekuwa na mshirika ikiwa imani kuu na ya msingi kabisa.

Ukristo kwa upande mwingine unasema kwamba Bwana wake ni Yesu kristo. Kwa mujibu wa Fritz Ridenour:

"------ Tunajinyenyekesha chini ya mamlaka yake".2
Hebu tuangalie tena katika Mathayo 4: 10, ambapo Yesu anasema:

"Msimsujudie yeyote isipokuwa Bwana Mungu wenu. Na mwabuduni Yeye tu".

Dhahiri shahiri, hapa Yesu anatuambia kwamba ni Mungu peke yake ndiye tunayetakiwa kumwabudu.

Dini sio suala la kubahatisha na hotuba bali ni ukweli (fact) na muongozo. Dini ya kweli inajali na kuzingatia utii wa sheria, na utii huu ndio kipimo cha uchamungu wa muumini.

Ndugu zetu wa Kikristo wanatakiwa kuzingatia masuala haya katika nyoyo zao. Sio tu kwamba hawafuati miongozo ya dini zao isipokuwa Jumapili, bali pia wamepotea kabisa kutoka kwenye mafundisho ya mtu ambaye jina lake linaunda msingi wa imani yao. Na badala yake wamebugia imani na mila za kipagani ambazo wamezivisha joho la imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na Mshirika (Monotheism). Marafiki zetu wa kikristo wana kazi kubwa zaidi ya kutafiti.

Waislam hawana budi kukumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu katika Qur'an:

"Wayahudi na Wakristo hawatakuwa radhi nanyi mpaka mtakapofuata dini yao". (Qur'an 2:120)

Pia ni lazima tukumbuke maneno ya mwisho yaliyotolewa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad (saww):

"Leo nimekukamilishieni dini yenu (na) kukutimilizieni neema yangu juu yenu na Nimekuchagulieni Uislamu ndio iwe dini yenu". (Qur'an 5:3).

Baada ya kusema na kufanya yote, ni lazima tuyazingatie maneno muhimu yafuatayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Tunaubanisha na kuuthibitisha ukweli dhidi ya Uongo (Batili) mara Batili ikaondoka. Na adhabu inakungojeeni kwa haya mnayoyasema". (Qur'an 21:18)

  • 1. Basic Christianity, p. 20. (Ukristo wa msingi, uk. 20).
  • 2. How To Be A Christian In An Unchristian World, p. 126. (Jinsi ya kuwa Mkristo katika Ulimwengu usiokuwa wa Kikristo. Uk. 126).

Orodha Ya Vitabu Vitabu Vingine Vinavyohusiana Na Ulinganishaji Baina Ya Uislamu Na Ukristo

• Ahmad, Khurshid. Islam and the West. Lahore, Pakistan: Islamic Publications, Ltd., 1986.

• Ajijole, A.D.A. Myth of the Cross. Chicago: Kazi Publications, 1979.

• Al-Johani, Dr. Maneh Hammad. The Truth About Jesus. Riyadh, Saudi Arabia: World Assembly of Muslim Youth, 1987.

• All Scripture Is Inspired of God and Beneficial. Watch Tower Bible and Tract Society. Brooklyn (NY): WTBTS, 1990.

• Andry, Carl Franklin, Ph. D. Jesus and the Four Gospels. Muncie. IN: Print press, 1978.

• Badawi, Dr. Jamal. Jesus in the Qur'an and the Bible: An Outline. Halifax, Nova Sotia: Islamic Information Foundation.

• Muhammad In the Bible. Halifax, Nova Scotia: Islamic Information Foundation.

• Bainton, Roland H. Early Christianity. Princeton (NJ): Van Nostrand Co., Inc.

• "Bits N Pieces". The American Religion: The Emergence of the Post - Christian Nation: NY: Simon & Schuster, 1992.

• Brown, Aisha. Three In One: The Doctrine of the Trinity. Chicago (IL): The Open School,1992.

• Bucaille, Maurice. The Bible, the Qur'an and Science. Delhi, India Cresent Publishing, 1978.

• Chirri, Imam Mohamad Jawad. Inquiries About Islam. Detroit (MI): Harlo Press, 1986.

• Davies, A. Powell. The Meaning of the Dead Sea Scrolls: NY: New American Library, Inc.,1956.

• Deedat, Ahmed. Is the Bible God's Word? Durban, South Africa: Islamic Propagation Centre.

• Dibble, R.F. Mohammed. NY: Garden City Publishing Co. Inc., 1926.

• Durant, Will. The Age of Faith. NY Simon and Schuster, 1950.

• Evans, Rod L. and Irwin M. Berent. Fundamentalism: Hazards and Heartbreaks. LaSalle (IL): Open Court Publishing Co., 1988.

• Grun, Bernard. The Timetables of History. NY Simon & Schuster, 1991.

• Frazer, Sir James George. The Golden Bough. Ny: Macmillan Comapany, 1940.

• Haneef, Suzanne. What Everyone Should Know About Islam and Muslims. Des Plaines (IL): Library of Islam, 1985.

• Harstad, Bjug A. Is the Bible Reliable? Parkland (WA), 1929.

• Hart, Michael H. The 100: A Ranking of the Most Influential Persons in History. NY: Hart Publishing Co., Inc., 1978.

• Holy Bible. Authorized King James Version. Grand Rapids (MI): Zondervan Corp., 1977.

• Holy Bible. American Standard Version. NY: Thomas Nelson & Sons, 1901.

• Holy Qur'an. Trans. by A Yusuf Ali. Madinah (Saudia Arabia): King Fahd Holy Qur'an Printing Complex, 1989.

• Jammelah, Maryam. Islam Versus the West. Lahore, Pakistan: M.Y. Khan and Sons, 1984.

• Jansen, G.H. Militant Islam. NY: Harper & Row, 1979.

• Johnson, George. Christmas Ornaments, Lights and Decorations. Paducah (KY) : Collector Books, 1990.

• Kingsriter, Del. Sharing Your Faith With Muslim. Minneapolis(MN): Center For Ministry to Muslims.

• Journey To Understanding. Minneapolis (MN): Center For Ministry to Muslims.

• Levy, Leonard W. Treason Against God: A History of the Offense of Blasphemy. NY: Schocken Books 1981.

• Light of Truth, The Canada Maritime Muslim Students' Association.

• Lippman, Thomas W. Understanding Islam. NY: Penguin Books, 1990.

• McCurry, Don M. Muslim Awareness Seminar Notebook. Pasadena, CA: Joy Printing, 1981.

• Maier, Paul L. First Christians: Pentecost and the Spread of Christianity. NY: Harper & Row1976.

• Manchester, William. A World Lit Only By Fire. Buston (MA): Little, Brown and Co., 1992.

• Mankind's Search for God. Watch Tower Bible and Tract Society. Brooklyn (NY): WTBTS 1990.

• Marty, Martin E. A Short History of Christianity. Cleveland (NY): William Collins & World Publishing Co. Inc., 1975.

• Mears, Henretta C. What the Bible Is All About. Minneapolis, MN: The Billy Graham Evangelistic Association, 1966.

• "Media Response Publications Edition". Jan. - March, 1992.

• Mohammad, Ch. Nazar. Commandments By God in The Qur'an. NY: The Message Publications 1991.

• Morey, Dr. Robert A. Islam Unveiled: The True Desert Storm. Shermans Dale, P.A. The Scholars Press, 1991.

• Mufassir, Sulaiman. Jesus in the Qur'an. Plainfield (NY): Muslim Students' Association, 1977.

• Murstein, Bernard I. Love, Sex and Marriage through the Ages. NY: Springer Publishing Co., 1974.

• Neufeldt, Victoria ed. Webster's New World Dictionary. Ny: Simon and Schuster, 1988.

• New Testament For America. Taken from the Holy Bible, New International Version. South Holland, IL: The Bible League, 1984.

• New York Public Library Desk Reference, The NY: Webster's New World, 1989.

• Reach Out In Friendship. Center For Ministry to Muslims Minneapolis (MN): CMM.

• Ridenour, Fritz How to Be A Christian In An Unchristian World. Glengale, CA: G/L Publications, 1971.

• Rosten, Leo. Religions of American. NY: Simon and Schuster 1975.

• Rusell, D.S. Between The Testaments. Philadelphia: Fortness Press, 1960.

• Shorrosh, Dr. Anis. Islam Revealed. Nashvile: Thomas Nelson Publishers, 1988.

• Stott, John. Basic Christianity. Downers' Grove, IL: Inter - Varsity press.

• The Bible: God's Word or Man's? Watch Tower Bible and Tract Society. Brooklyn (YN): WTBTS, 1989.

• Thiessen, John Caldwell. A survey of World Missions. Chicago: Inter - Varsity Press, 1955.

• This Is the Catholic Church. Knights of Columbus. New Haven (CO): K of C, 1955.