Aya 101 – 111: Hakuna Ujamaa Baina Yao Siku Hiyo
Maana
Basi itakapopuziwa parapanda, hapo hakutakuwa na nasaba baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.
Kupuziwa parapanda ni kinaya cha kufufuliwa walio katika makaburi. Kutokuweko nasabu maana yake ni kutokuwako kuhurumiana baina ya jamaa na ndugu: "Siku mtakapoiona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshae." Juz. 17 (22: 2).
Siku hiyo hakutakuwa na kitu chochote isipokuwa imani na matendo mema: "Na kila mmoja kati yao atamfikia siku ya Kiyama peke yake. Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi." Juz.16 (19:95-96).
Kuna Hadith isemayo kuwa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama atasema: "Leo ninaziondoa nasaba zenu na ninaweka nasaba yangu, wako wapi wenye takua?
Neno nasaba limetokana na kunasibiana. Neno udugu linafasiriwa kutoka neno la kiarabu Qaraba, lenye maana ya ukaribu. Hakuna ukaribu na Mungu isipokuwa kwa takua. Tazama Juz. 4 (3:199 - 200) kifungu cha 'Takua' Vile vile Juz. 11 (10:5-10) Kifungu 'Wako wapi wacha Mungu.'
Basi ambao mizani zao zitakua nzito hao ndio wenye kufanikiwa. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia hasara nafsi zao na watadumu katika Jahannam.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:8) kifungu 'Mizani ya matendo.' Vilevile tumeizungumzia mara ya pili mizani hii katika Juz. 17 (21:47) kifungu 'mizani siku ya Kiyama.'
Moto utababua nyuso zao nao humo watakuwa wenye kukunjana.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameleta ibara ya uso kwa niaba ya mwili wote, kwa sababu uso ndio kiungo kizuri zaidi.
Imepokewa Hadith kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye amesema: "Moto utababua nyuso zao, ni mbabuo utakaoenea hadi kwenye visigino vyao.
Je, hazikuwa Aya zangu mkisomewa na nyinyi mkizikadhibisha?
Huku ni kusutwa, kwa kukadhibisha kwao hoja za Mwenyezi Mungu na ubainifu wake.
Watasema: Mola wetu! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tuliopotea.
Wanakiri dhambi zao baada ya kukatikiwa na kufungwa mlango wa toba! Umetangulia mfano wake katika Juz. Juz. 8 (7:5) na Juz. 17 (21:14).
Mola wetu! Tutoe humu motoni. Na tutakaporudia, basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.
Watayasema haya baada ya kudhihiri hukumu na baada ya kuwathibitikia uhakika. Hapo mwanzo walikuwa wamezama katika uasi wao. Ndio maana Mwenyezi Mungu atasema:
Tokomeeni humo, wala msinisemeshe.
Ni maneno yakukemewa mbwa hayo ambayo yamedhihirisha ghadhabu za Mwenyezi Mungu.
Hakika lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu tusamehe na uturehemu, na wewe ndiwe mbora wa wanaorehemu. Lakini ninyi mliwafanyia maskhara mpaka wakawasahahulisha kunitaja na mlikuwa mkiwacheka.
Baada ya kuwasuta wakosefu na kuwakemea, hapa anawabainishia kwamba wao walikuwa wakiwafanyia kejeli na kuwacheka waja wema wa Mwenyezi Mungu ambao wanataka maghufira na rehema kutoka kwa Mola wao, kiasi ambacho kejeli ziliwafanya wamsahau Mungu.
Hakika mimi leo nimewalipa kwa vile walivyosubiri. Hakika hao ndio wenye kufuzu.
Waumini walivumilia maudhi ya wakosefu, ndio Mwenyezi Mungu akawaneemesha hawa na akawaadhibu hao.
فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ {34}
قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ {112}
قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ {113}
قَالَ إِنْ لَبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ لَوْ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ {114}
أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ {115}
فَتَعَالَى اللَّهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ {116}
وَمَنْ يَدْعُ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِنْدَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ {117}
وَقُلْ رَبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنْتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ {118}