Aya 16 – 20: Kukimbia Hakutawafaa
Maana
Sema: Hakutawafaa kukimbia; ikiwa mnakimbia kifo au kuuawa.
Walikimbia jihadi kwa kuhofia mauti, na mtu hawezi kuepuka kifo kwa kukimbia, wala mwenye kukipenda pia hawezi kubakia.
Na hata hivyo hamtastareheshwa isipokuwa kidogo tu.
Ikiwa mtasalimika kifo kwenye uwanja wa vita, basi mtakutana nacho baada ya muda mchache tu, kisha muingie motoni. Lakini mashahidi watakwenda kwenye Pepo yenye neema. Imam Ali (a.s.) anasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, mapigo elfu moja ya panga kwangu ni mepesi zaidi kuliko kufa kitandani.”
Sema, ni nani atakayewalinda na Mwenyezi Mungu akiwatakia uovu au akiwatakia rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Tutaifasiri na kauli yake nyingine Mwenyezi Mungu: “Sema ni nani awezaye kuwasaidia chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka kuwadhuru au akitaka kuwanufaisha?” (48:11). Umetangulia mfano wake katika Juz. 13 (13:11).
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanaozuilia na wanaowaambia ndugu zao: Njooni kwetu! Wala hawaingii vitani ila kidogo tu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawajua wanafiki na kwamba wao wanawazuia watu wasiende vitani na kuwaambia: Kuna haja gani ya vita njooni tule raha. Wanapofichuka basi wanakwenda vitani kwa kujisukuma, kama vile wanapelekwa machinjioni, wanapigana kidogo kidogo na kuwa wazito. Watu wa aina hii wanapatikana kila wakati.
Wana choyo juu yenu kwa mali na ushindi, ubakhili wote Mwenyezi Mungu anausamehe; isipokuwa ubakhili wa jihadi na mali.
Ikija hofu utawaona wanakutizama na macho yao yanazunguka kama ambaye amezimia kwa mauti, lakini hofu inapoondoka wanawaudhi kwa ndimi kali.
Aya hii inaelezea woga wa wanafiki na udhaifu wao kwenye kifo. Wana jeuri ya ya dhambi wakiwa salama, lakini ukianguka mshindo macho yao yanazunguka kwa fazaa na woga, wakishasalimika ndimi zao zinaanza kuwauma waumini wanaopigana jihadi.
Katika Nahjul-balagha kuna maelezo haya: “Hakika mnafiki anazungumza yanayomjia kwenye ulimi wake: hajui anayostahiki na yaliyo wajibu kwake.” Mtume naye anasema: “Haiwi sawa imani ya mja mpaka uwe sawa moyo wake, wala hauwi sawa moyo wake mpaka uwe sawa ulimi wake.”
Na wanaifanyia choyo kheri.
Makusudio ya kheri hapa ni ngawira. Yaani wao wakati wa vita ni waoga, lakini wakati wa kugawanya ngawira wanapandisha sauti kwa kuhoji na kwamba wao wana haki zaidi kuliko wote. Hao hawakuamini; bali walidhihirisha imani wakaficha kufuru, wakapi- gana pamoja nanyi kwa unafiki na riya.
Basi Mwenyezi Mungu amezipomosha amali zao.
Yaaniamebatilishakupiganakwaokwasababukulikuwanikwaajiliya asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Kuna Hadith inayosema: “Yeyote ambaye kuhama (kuhajiri) kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi kuhama kwake ni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ambaye kuhama kwake ni ili aipate dunia au mwanamke wa kumuoa, basi kuhama kwake ni kwa lile alilolihamia.”
Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.
Hilo la kupomosha kupigana kwao. Ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sababu Yeye si dhalimu.
Wanadhani yale makundi hayajaondoka.
Makundi yaliondoka bila ya kurejea, lakini wanafiki hawamini macho yao; si kwa lolote ila ni kwa kuwa wanatamani lau makundi yale yangelimfyeka Mtume na sahaba zake. Matamanio yao haya yakawapa picha kuwa makundi yale bado yako yameuzingira mji wa Madina na kwamba watawamaliza Waislamu kesho au keshokutwa.
Wanatamani wangelikuwa jangwani pamoja na mabedui wakiuliza habari zenu.
Wanafiki wakihakikisha kuwa makundi yameshindwa; kisha yarudi tena mara ya pili Madina, basi watatamani wanafiki lau wangelikuwa mbali na Madina wakikaa jangwani wawe wakiuliza tu yaliyowapata waislamu.
Na lau wangelikuwa pamoja nanyi wasingelipigana isipokuwa kidogo tu.
Huu ni mfano wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyotangulia ‘Walahawaingiivitaniilakidogotu.’
لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا {21}
وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا {22}
مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا {23}
لِيَجْزِيَ اللَّهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ إِنْ شَاءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا {24}
وَرَدَّ اللَّهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّهُ قَوِيًّا عَزِيزًا {25}
وَأَنْزَلَ الَّذِينَ ظَاهَرُوهُمْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِنْ صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا {26}
وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَمْ تَطَئُوهَا ۚ وَكَانَ اللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا {27}