
Kufunga mikono katika Sala: Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: "Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema Yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (5:3).