Anayeafikiana Na Imamiyya Katika Baadhi Ya Nukta
Pia wapo wanaoafikiana na Imamiyya katika baadhi ya nukta za suala hili.
An-Nawawy amenukuu kwa kusema: Atwau na Tausi wamesema: “Kivuli cha kitu kikilingana na kitu chenyewe hapo umeingia wakati wa Al-Asr na ufuatao ni wakati wa Adhuhuri na Al-Asr kwa kushirikiana mpaka jua litakapozama.
Kauli hii inahusu Adhuhuri kwa kivuli cha kitu kulingana na kitu husika, kisha inafanya wakati uliobaki ni wa kushirikiana Adhuhuri na Al-Asr mpaka jua litakapozama. Kauli hii inakaribiana na ile ya Imamiyya.
Malik amesema: “Kivuli kikilingana na kipimo cha kitu kilichosimama ndio mwisho wa wakati wa Adhuhuri na mwanzo wa wakati wa Al-Asr kwa kushirikiana. Hivyo kivuli kikizidi kipimo ziada ya wazi basi wakati wa Adhuhuri umekwisha.1
Kauli hii inafanya sehemu ya wakati kuwa wakati wa kushirikiana kati ya Adhuhuri na Al-Asr nao ni - baada ya kivuli kulingana na kipimo cha kitu kilichosimama - mpaka kivuli kinapokizidi kipimo hicho kwa ziada ya wazi, ni wakati wa kushirikiana kati ya Adhuhuri na Al- Asr.
Pia imenukuliwa toka kwake kuwa, wakati wa Adhuhuri unaendelea mpaka kuzama kwa jua.2
Na kuna kauli nyingine ambazo zina namna fulani ya muafaka na fiqhi ya Imamiyya.