read

Dibaji

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asema:

"Ee Allah! Hawa (Ali, Fatima, Hasan na Husain) ndio Ahlul Bait wangu, basi watoharishe kwa tohara kamili."

"Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain..."

"Hao (Hasan na Husain) ni maua yangu katika dunia."

"Ewe Mwanangu (Husain)! Mwili wako ni mwili wangu na damu yako ni damu yangu;"

"(Ewe Husain), wewe u Sayyid, mwana wa Sayyid, na ndugu wa Sayyid; wewe u uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) mwana wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) na ndugu wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu); na baba wa uthibitisho tisa ambao wa tisa wao ni Qaim wao ambaye atakuwa al-Mahdi."

"Hasan na Husain ni Masayyidi wa Vijana wa Peponi."

"Ewe Mola wangu! Mpende yule ampendaye Husain."

"Adhabu atakayoipewa yule muuaji wa Husain huko Motoni itakuwa sawa na nusu (nzima) ya adhabu yote watakayopewa wenye dhambi wa ulimwengu."

"...., Allah hujirafikisha na wale wajirafikishao na Husain, yu adui wa wale walio maadui zake."

"Yeyote awapendaye Hasan na Husain amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia."

***************

Ahlul Bayt (a.s.) Assembly ya Tanzania (ABATA), inayo furaha kwa kutoa Kitabu hiki cha Mashairi kwa watu wazungumzao Kiswahili. Yakiwemo mapendekezo ya Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mwenyekiti wa ABATA, kwamba tuchapishe vitabu vya Majlis na Mashairi (Nauha na Utenzi) juu ya "Masaibu ya Karbala."

Kwa hiyo mwezi Aprili, 1998 tulichapisha Kitabu cha Majlis kinachoitwa, "Maombolezo ya Kifo cha Imam Husain (a.s.)" ambacho kimetokea kupendwa sana Afrika ya Mashariki. Alhamdulillah.

Sayyid Murtaza Rizvi na Sheikh Abdul-Majid Nassor, kwa ushauri wa Mwenyekiti wa ABATA, wameyakusanya Mashairi haya kutoka sehemu mbalimbali, wakayapanga na kupata kitabu kiitwacho "Mashairi ya Masaibu ya Karbala" ambacho unacho mkononi mwako hivi sasa.

Hiki ni Kitabu cha tatu ambacho kimetolewa na Ahlul-Bayt (a.s.) Assembly ya Tanzania, na tunayo furaha kubwa kutoa kitabu cha Mashairi ya Karbala kwa Kiswahili ambacho ni cha kwanza katika lugha ya Kiswahili.

Allah Subhanahu wa Ta'ala atoe malipo yake kwa wale wote ambao wamesaidia katika uchapishaji wa kitabu hiki.

Wamaa Tawfeeqi Illa Billah.
P.O. Box 75215
Dar es Salaam
Tanzania
24, Februari, 1999

F. A. Hameer
Katibu Mkuu
Ahlul-Bayt (a.s.) Assembly ya Tanzania