read

Barua Ya Haraka Kwa Msichana Wa Karne Ya Ishirini Na Moja

Kwako msichana wa karne ya ishirini na moja.

Wale wanaopigania uhuru hawakupiganii wewe, ati mwanamume fulani apigania uhuru wako kama unavyofahamu, sivyo, bali hao wenye njaa wanapi­gana wapate uhuru kwenye mwili wako wakuvutia, au ati mwanamke fulani atake uwe huru kwa sababu yeye yuhuru, la hasha, anachotaka ni kukuingiza wewe uwe pamoja naye katika pepo hiyo na mapo­chopocho, yeye anapotea na ataka wewe pia uanguke kwenye shimo la maovu kama yeye ili umuondolee hisia zake za kujiona yuko peke yake katika maovu hayo.

Hebu peleleza maisha yao hasa hao wanaopigania uhuru ugundue ukweli ulivyo: kwa hakika wote hao wana maovu yao wanataka kujificha uovu wao chini ya joho tukufu, na inaweza kuwa wana kasoro katika namna ya kufikiri au kwenye mambo mengine.

Pengine mtu anaweza kuwa kama Bw. Sartre anaye­pigania ‘uhuru’ akiulizwa nini maana ya uhuru, anasema: “Ni mwanamke awe na uhuru wa kufanya mapenzi na kila mtu.” Anapoulizwa ‘hata mkeo’ anajibu, “ndiyo, hata mke wangu akipenda kufanya hivyo.” Baadaye watu walipo yachunguza maisha yake ya utotoni waligundua kuwa alikuwa na kasoro.1

Au pia inawezekana mwanamume akiwa ni wa aina nyingine mathalan, aina ya wale ambao mkewe au mabinti zake wana kasoro, au anataka tu kustarehe na wanawake wengi kwa masaa tu na kuwapokonya maua ya maisha.

Au pia inaweza kuwa ni kwa sababu nyingine; almu­radi ni lazima utambue kuwa hakuna ‘anayekupi­gania’ uwe huru. Na jichunge sana usijaribu kuingia kwenye janga lolote, kwani utapotea.

Ukitawaliwa udhihirishe uso, nywele au mguu wako ‘kidogo’, usisadiki kwamba yataishia hapo tu bali yatafikia mahali ambapo hapana mwisho mwema. Unataka nikupe dalili?

Hebu chukua jarida lolote dukani uliangalie, kwa haraka kitu utakachokiona ni wasichana wadogo ambao kila mmoja wao aweza kuwa ‘mama’ na akai­shi maisha matulivu ya ndoa, lakini wameufuata mwito wa kuonyesha nyuso, nywele na miguu ‘ki­dogo’ na wakaukubali mara tu baada ya muda mfupi walipogundua, tayari wameshakuwa ‘wasi­chana wanaohitajika wakati wa haja’, Ee Mungu! azirehemu enzi za utawa (za zamani)!

Na msichana anapokuwa chombo cha kutumiwa kwa matamanio ya wengine anapoteza thamani yake, hata wewe rafiki wajua vizuri hilo. Na hata mwanamume anayemtafuta msichana kama huyu humpenda kwa muda mchache tu unaoteketea mara moja tu na kuwacha moshi mzito unaompoteza msichana huyo, na anapokufa hakuna hata mtu mmoja atakayemlilia. Ndiyo, ni kweli kwamba pengine utajisikia hamu ya jinsiya na ikawa inaweza kupatikana lakini ole wako usikubali kujiingiza kwenye hiyo. Kwani njaa yako yaweza kuwa ya uwongo na kuukosa heshima yako ya kike ni ukweli kabisa. Na mwanamke anapoukosa uwanawali wake basi haupati tena, au sivyo!

Dada mpendwa, wakikuhadaa ufanye kazi kiwandani au ya safari na utapata mshahara mkubwa uweze kukidhi mahitaji yako na ya watoto usiwasadiki kwani nia yao si wewe uchume bali nia yao wakupate; kum­buka ya kwamba asilimia themanini ya wanawake wafanyao kazi viwandani nchini Marekani wame­sinywa na kazi, kama ripoti zinavyoonyesha.

Na kumbuka pia ya kwamba mwandishi wa kike maarufu, Helen Michel amesema kwa uhuru, maendeleo ya ki uchumi na nafasi za kimataifa ali­zozipata mwanamke wa Ufaransa hazijamkwamua kutokana na matatizo yake mazito na wala haziku­badilisha hali yake na kuweza kupeleka jahazi la mai­sha.

Isitoshe, hakuna anayekupenda sana zaidi ya Mwenyezi Mungu aliyekuumba kwa hivyo usitende ila yale anayoyasema.

  • 1. Jean Paul Sartre mwandishi na mwanafalsafa wa kifaransa aliyezaliwa mwaka 1905 (A.D.)