Abubakr na Umar hawakuwahi kumzika Mtume (s.a.w.)

Taz: Kanzul Ummal J.5 Uk. 652

Wakati wote huo Imam Ali yuko nyumbani kwa Mtume (s.a.w.) akishughulikia maandalizi ya kumzika Mtume.

Swahili

Saqifa

Kwanza, ni vizuri kujua maana ya neno: Saqifa: Ni Klabu au ukumbi.

Amesema Mwana Aisha kuwa: "Zilipotangazwa habari za kifo cha Mtume (s.a.w.) Umar bin Khattab na Mughira bin Shuubam waliingia ndani alikolazwa Mtume (s.a.w.). Umar akasema: Oh! msiba mzito kwa kuondokewa na Mtume, kisha walitoka nje, walipokuwa mlangoni Mughira akasema: "Ewe Umar! Kwa kweli Mtume amekufa", Umar akajibu: "Wewe muongo, Mtume hajafa isipokuwa wewe ni mtu unayesumbuliwa na fitina. Mtume hatakufa mpaka wanafiki wamalizike wote."

Taz: Albidayatu Wannihaya J.5 Uk. 212

Swahili

Riwaya Kuhusu Swala

Imepokewa kwa Mwana Aisha kuwa, Mtume (s.a.w.) alipougua maradhi aliyofia, aliamrisha kuwa: Abubakr asalishe watu, mimi (Aisha) nikasema, Abubakr ni mtu mpole sana, atakaposimama mahala pako atashindwa (kusalisha); Mtume akaamuru: Abubakr asalishe. Nikasema kama nilivyosema kwanza, Mtume akakasirika akasema: Nyinyi ni watu wa Yusuf. Mara Mtume akahisi woga moyoni mwake, akatoka akichechemea kwa kushikiliwa na watu wawili (Ali na Abbas) alipofika Msikitini, Abubakr akarudi nyuma ya safu ya kwanza.

Swahili

Tukio La Karatasi

Waandishi wa tarikh na Hadithi wamelieleza tukio la Karatasi kama hivi:

"Mtume (s.a.w.) alipokuwa mgonjwa mahtuti, watu wengi walikusanyika ndani ya nyumba ya Mtume akiwamo Umar Ibn Khattab. Mtume (s.a.w.) aliwaambia kuwa: "Nileteeni Karatasi niwaandikieni maandiko hamtapotea baada yake." Umar akasema: Mtume anaweweseka! Mtume akawaambia: "Niondokeeni" wakaondoka.

Katika kauli nyingine inasema: Umar alimwambia Mtume baada ya kuagiza karatasi: "Mtume yamemzidi maradhi inakutosheni Qur’an mliyo nayo."

Kauli ya kwanza na ya pili utazipata katika:

Swahili

Jeshi La Usama

Katika mwaka wa kumi Hijra, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipeleka jeshi kwenda kupigana Roma. Katika jeshi hilo Mtume aliamuru liongozwe na Usama bin Zaid akasema:- "Nenda ukapigane alikouliwa baba yako."

Uteuzi huu Masahaba haukuwapendeza, kwa hiyo walisikika wakipinga amri hiyo wakisema: "Itakuwaje mtoto mdogo huyu apewe madaraka makubwa juu yetu?"

Swahili

Qur'an Na Ahlul Bait

Imepokewa kutoka kwa Sahaba Zaid bin Arqam: Amesema Mtume (s.a.w.):- "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Qur'an na Ahlul Bait wangu, viwili hivi havita achana mpaka vitakaponifikia katika Haudh."

Taz: Tafsir Ibn Kathir J.4 Uk. 122

Tafsirul Khazin J.1 Uk. 4

Tarikh Bughdad J.8 Uk. 442

Sahihi Muslim J.4 Uk. 1873

Sahihi Tirmidh J.2 Uk. 308

Jamiul Usul J.1 Uk. 187

Albidayatu Wannihaya J.7 Uk. 362

Swahili

Mubahala

Kabla hatujaingia ndani kuzungumzia suala la Mubahala, kwanza ni vizuri tufahamishe maana ya Mubahala. Mubahala ni:

Kuapizana.

Ujumbe wa Kikristo kutoka Najran ulifika kwa Mtume kujadili suala la Nabii Isa (a.s.). Mtume aliwajulisha kuwa: "Hakika mfano wa Isa (a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa." 3:59

Kwakuwa Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu.

Swahili

Uimam

Msimamo wa Aya zilizokuja juu ya uongozi, ukisoma yalioandikwa katika vitabu mbali
mbali na Hadithi zilizothibiti, na tarikh inayoonyesha katika jambo hili, utapata mambo makuu matatu ambayo yanaonyesha kuwa: Uimam/Ukhalifa lazima uteuliwe na Mwenyezi Mungu; na kwa upande wa pili utaona kuwa Nyimati zilizopita zilifuata uongozi uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, wala jambo hilo halikuachiwa watu wenyewe kwa njia ya kuchaguwana.

Swahili

Utangulizi

Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwafikisha mara nyingine kukamilisha kuandika kitabu hiki, baada ya kitabu chetu:- "Mut'a ndoa sahihi."

Mambo yanayoweza kuamsha misimamo ya watu na kuleta msukumo mpya katika kumwandaa binadamu ili apige hatua mbele, ni kujua habari za watukufu wao waliotangulia. Kwa sababu kujua habari za watangulizi wetu ni mizani ya kutupimia sisi tunaokuja baada yao.

Swahili

Mwandishi Wa Kitabu Hiki

Jina langu ni Omar Jumaa Mayunga. Nimezaliwa mwaka 1947, Mkoa wa Tabora katika Wilaya ya Igunga Tarafa ya Simbo.

Mwaka 1957 baba yangu alianza kunisomesha Qur'an Tukufu, ilipofika mwaka 1959 nilianza masomo ya Kizungu katika Shule ya Msingi ya Simbo hadi mwaka 1962 nilipokaa nyumbani kuendelea na masomo ya Qur'an.

Swahili