Pote Lenye Kuokoka

Amesema Mtukufu Mtume (s.a.w.) "Watafarakana umma wangu makundi sabini na tatu, kundi moja tu kati ya hayo litaokoka, na yaliyobaki yatatiwa motoni. Ali akauliza: "Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu! Kundi gani litakalookoka? Mtume (s.a.w.) akajibu: "Wewe na watu wako".

Taz: Ithbatul Hudat J. 2 Uk. 260

Swahili

Lengo La Israa Na Miraji

Tukitaka kujuwa shabaha na hekima na muujiza wa Israa na Miiraji, lazima kusoma nassi zake na vipengele vyake kwa undani na makini. Na hapa tutaonyesha mambo yafuatayo:

Israa na Miiraji ni muujiza mkubwa wa kudumu, na leo katika karne hii ya ishirini tukio hili linakubaliwa na elimu ya sayansi na Teknolojia. Mwanadamu hashangai tena leo kusikia kuwa mtu amekwenda umbali wa maili nyingi zaidi katika upeo wa juu.

Swahili

Musa Na Sala Tano

Imepokewa katika riwaya kuwa: Sala tano zimefaradhiwa wakati Mtume (s.a.w.) alipopelekwa katika msafara wa Miiraji huko juu Inasemwa kuwa, zilifaradhiwa sala hamsini kwa kila siku, na Mtume (s.a.w.) alipokuwa akirudi na agizo hilo, alipofika mbingu ya sita akakutana na Nabii Musa (a.s.) akamshauri Mtume Muhammad (s.a.w.) arudi kwa Mola wake amuombe ampunguzie Sala hizo.

Swahili

Israa Na Miiraji

Israa ni: Mwendo wa usiku, kama ilivyokuja katika Qur'an: "Utukufu ni wa yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku, kutoka Msikiti mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (Falastin) ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumuonyeshe baadhi ya ishaara zetu" 17:1

Swahili

Majibu Yetu

Swahili

Kusoma Qur'an Kwa Ajili Ya Maiti

Wako baadhi ya Waislamu wanapinga kumsomea Qur'an maiti, wakisema kwamba kufanya hivyo ni bid'a na bid'a mahala pake ni motoni. Katika kupinga jambo hili wanatoa hoja zao kama ifuatavyo:

Imethibiti kuwa: Mtume (s.a.w.) hakumsomea Qur'an maiti yeyote katika uhai wake, kama jambo hilo ni jema Mtume asingeliacha kufanya kheri hiyo. Kwa hiyo, yeyote leo anae soma Qur'an kwa ajili ya mait, akaamini kuwa itamnufaisha, bila shaka mtu huyo anadai kuwa Mtume amefanya khiyana katika umma huu. Na hilo ni kosa kubwa kuamini kuwa Mtume hakufikisha baadhi ya mambo katika umma wake.

Swahili

Qur'an Imeumbwa

Ndugu zetu masunni wanaamini kuwa: Qur'an ni ya tangu na tangu (Qadim) Mashia Ithan Ashar wanaamini kuwa: Qur'an imeumbwa.

Kwahiyo, hapa tutachunguza kama ifuatavyo: Katika matumizi ya lugha ya kiarabu, tamko la "JAA'L".

Linapotegemezwa kwa Mwenyeezi Mungu huwa kwa maana ya "KHALQ" yaani, "KUUMBA". Na hapa tutataja baadhi ya mifano hiyo:

"Wajaa'la min'ha zawjaha" yaani, "Na ameumba mkewe".

"Huwalladhi jaa'la lakumul layla" yaani, "Yeye ndiye aliyewaumbia usiku".10:6

Swahili

Hadithi Zisemazo Kuwa Ataonekana

Anasimulia Abu Huraira katika Hadithi aliyoipokea kuwa: (siku ya kiyama) "Mwenyeezi Mungu atawaijia (watu) akiwa na sura tofauti na ile wanayomjua, awaambie: Mimi ndiyo Mola wenu. (Watu) watajibu:

Mwenyeezi Mungu atuepushe nawe, sisi tutabaki hapa hapa mpaka Mola wetu (tunayemjua) atufikie, na akija sisi tutamjua. Mara Mwenyeezi Mungu atawafikia kwa sura yake ile wanayomjua atasema: Mimi ni Mola wenu. Nao watajibu: (kweli) wewe ndiye Mola wetu, na watamfuata".

Taz: Sahihi Bukhari J. 4 Uk. 92

Sahihi Muslim J. 1 Uk. 86

Tafsirul Khazin J. 7 Uk. 137

Swahili

Mwaka Mpya Wa Kiislaam

Inasemwa kuwa, katika mwaka wa kumi na sita Hijra, masahaba walikutana kujadili juu ya tarehe ya Kiislaamu itakayojulisha mwanzo wa mwaka.

Imam Ali (a.s.) Alisema kuwa: "Ifanywe kuwa ni mwanzo wa mwaka mpya, ile siku Aliyohama Mtume (s.a.w) akaacha ardhi ya shirki"

Taz: Fat'hul Bari J. 7 Uk. 209

Tarikhut Tabari J. 2 Uk. 112

Tarikh Ibn Athir J. 2 Uk.526

Alkhutat wal'athar J. 1. Uk. 284

Swahili

Utangulizi

Alhamdulillah, Rehma na Amani zimshukie Mtume wetu na Muombezi wetu Muhammad (s.a.w.) na Aali zake watukufu waliotakaswa. Ninamshukuru zaidi Mwenyeezi Mungu kwa kuniwafiqisha kuchapisha kitabu: Muongozo wa Wasomao, kama alivyoniwafiqisha kabla ya hiki kuchapisha vitabu: Mut'a ndoa sahihi na Meza ya uchunguzi na vingine vingi, Alhamdulillah, Muongozo wa Wasomao, ni kitabu kilichokusanya maudhui nyingi tofauti kwa muhtasari.

Swahili