Tukio La Jamal

Jamal ni ngamia. Inaposemwa Tukio la Ngamia, maana yake yule ngamia aliyempanda Mwana Aisha akaenda nae katika uwanja wa Basra.

Katika mwaka wa thelathini na sita Hijria, Talha na Zubeir walimuomba ruhusa Imam Ali kwenda Makka kwa ajili ya Umra. Walipokuwa njiani wakakutana na Mwana Aisha akawauliza habari za Uthman, wakamwambia kuwa Uthman ameuliwa. Mwana Aisha akasema "Muuweni na'athala hakika amekufuru."

Taz: Tarikh Ibn Athir J.3 Uk. 206

Lisanul Arab J.14 Uk. 193

Assiratul Halabiyya J.2 Uk. 286

Swahili

Imam Ali

Imam Ali (a.s.) ni; "Ndugu ya Mtume na Wasii wake na Khalifa wake kwa Waislamu wote."

Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 63

Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 62

Tarikh lbn Asakir J.1 Uk. 85

Assiratul Halabiyya J.1 Uk. 311

Musnad Ahmad J.5 Uk. 41

Kanzul Ummal J.15 Uk. 115

Kifayatut Talibi Uk. 620

Mizanul I'tidal J.2 Uk. 273

Majmauz Zawaid J.9 Uk. 113

Manaqib Ali Uk. 200

Swahili

Uthman Bin Affan

Mara alipochaguliwa Uthman, Abu Sufiyan alikwenda kumpongeza Uthman. Katika baadhi ya risala yake alisema hivi, "Sasa (utawala) umekufikia baada ya kushikiliwa na Bani Taymi, basi zungusha kama mpira (wanavyopasiana) na weka viongozi wake wakuu Bani Umayya. Kwa sababu huu sasa ni ufalme, wala sina habari kama kuna pepo wala moto."

Taz: Al-Istiia'b J.2 Uk. 690

Swahili

Tukio La Shura

Imepokewa kwa Qatada kuwa: Umar alipozidiwa karibu atakufa, aliwaita Waislamu mbele yake akasema: "Laiti Abu Ubaida bin Jarrahi angelikuwa hai ningelimchagua kuwa khalifa wenu, na laiti Salim mtumwa wa Hudhaifa angekuwa hai ningemchagua kuwa Khalifa wenu."

Swahili

Mambo Aliyoyaweka Katika Dini

Umar binil Khattab aliweka: "Talaka tatu kuwa tatu" (zinazotolewa kwa mara moja)

Taz: Tafsirul Qurtubi J.3 Uk. 130

Sahihi Muslim J.4 Babut Talaka

Fiq'hus Sunna J.2 Uk. 231

Musnadu Ahmad J.1 Uk. 314

Umar ameweka: "Assalatu khairun minan-nawm" (katika adhana ya asubuhi)

Taz: Al-Muwattau J.1 Uk. 25

Umar aliweka: "Swala ya Tarawih" (kwa jamaa).

Taz: Tarikhu Ibn Athir J. 3 Uk. 31

Tabaqatul Kubra J. 3 Uk 281

Tarikhul Khulafai Uk. 136

Swahili

Mambo Aliyoyaondoa Katika Dini

Umar binil Khattab ameondoa: "Ndoa ya Mut'a na Tamattuu ya hija."

Taz: Tafsirut Tabari J.5 Uk. 9

Tafsirul Qurtubi J. 5 Uk. 130

Tafsirul Razi J. 3 Uk. 200

Umar ameondoa: "Hayya a'la khairil-amal" (katika adhana na Iqamah).

Taz: Lisanul Mizani J.1 Uk. 268

Mizanul I'tidal J.1 Uk. 139

Sunanul Bayhaq J.1 Uk. 524

Da'aimul Islami J.1 Uk. 45

Swahili

Abubakr Amteua Umar

Abubakr alipokuwa mgonjwa taabani alimwitisha Uthmani bin Affan ili aandike wasia juu ya Umar binil Khattab, akamwambia:

"Andika Bismillahir Rahmanir Rahimi, hili ni agizo la Abubakr bin abi Quhafa kwa Waislamu wote", mara Abubakr akazimia; Uthman akaendelea kuandika: "Amma baada ya haya, nimekutawalisheni Umar binil Khattab na sikuacha kukupendeleeni kheri." Kisha Abubakr akazimuka, akauliza: Umeandika nini? Uthmani akamsomea yale aliyoyaandika, Abubakr akashangilia sana kisha akasema, "Uliogopa kuwa khitilafu ingetokea kama ningezimia moja kwa moja?"

Swahili

Tukio La Hijra

Mwenyezi Mungu anasema:- "Kama hamtamsaidia basi Mwenyezi Mungu amekwisha msaidia walipomfukuza wale waliokufuru, alipokuwa wa pili katika wawili walipokuwa wote, wawili katika pango. Alipomwambia swahibu yake; usihuzunike hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Ndipo Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake na akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona." 9:40

Uchunguzi wetu katika Aya hii utahusu silabi zilizotumika katika mfumo wa Aya hii, kwa hiyo tutajadili hapa nukta saba:

(a) Amekwisha msaidia

(b) Walipomfukuza

Swahili

Abu Bakr

Aliposhika utawala Abubakr, alitoa hutuba kwa mara ya kwanza, na hii ni sehemu ya hutuba hiyo; "Hakika mimi ninae shetani hunifikia mara kwa mara basi wakati wo wote atakaponifikia muniepuke."

Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 460

Mwenyezi Mungu anasema "Hakika sisi tumewajaalia mashetani kuwa marafiki wa wale wasioamini." 7:27

Abubakr anae shetani, na kila mwenye kuambatana na shetani si mu'umin, Abubakr ni nani?

Swahili

Ali Hakumbai Abubakr

Mwana Aisha amesema kuwa:- "Ali (a.s.) hakumbai Abubakr ila baada ya miezi sita kupita."
Abubakr alikwenda nyumbani kwa Imam Ali (a.s) akawakuta Bani Hashimu wamekusanyika, Imam Ali akamwambia, "Sisi haikutuzuilia kukubali ewe Abubakr, kwa kupinga heshima yako wala ubora aliokupa Mwenyezi Mungu, lakini sisi tunaamini kuwa jambo hili (la uongozi) ni letu na nyinyi mmelipokonya kwetu."

Kisha akawa anamtajia nafasi aliyonayo kwa Mtume (s.a.w.) na haki zake mpaka Abubakr akaangua kilio.

Taz: Tarikhut Tabari J. 2 Uk. 448

Swahili