Shia Walimu Wa Sunni
Kipimo cha kumpima mtu kuwa anafaa kupokea kwake mafundisho ya dini kwa salama na sahihi ni kutimia sharti tano hizi:
(a) Uwepo uadilifu wa mapokezi, maana yake kila mpokezi katika wapokezi wake awe Mwislamu, aliye balighi, asiwe fasiq na asiwe muongo.
(b) Yakamilike mafungamano ya Sanad, maana yake kila mpokezi katika wapokezi wake awe amepokea moja kwa moja mpaka kufikilia kwa Mtume (s.a.w.).
(c) Kuwepo udhibiti wa mapokezi, yaani kila mpokezi katika wapokezi wake awe mwenye kudhibiti vyema, sawasawa iwe kwa kuhifadhi moyoni au kuhifadhi kwa maandiko.