Mwanamke Wa Dini; Majukumu Na Wajibu Wake

“...Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na nafsi moja...” (7:189)

Wajibu na majukumu ya mwanamke ni kama ya mwanamume, na suala lake ni kama la mume yaani suala la haki, ujumbe na marejeo. Isitoshe, mustakbali wa kazi yoyote ni dini kwa njia moja au nyengine mwanamke naye ana kazi yake.

Kuna kazi zingine ambazo hakuna awezaye kuzisimamia na kuzitekeleza ila yeye, kwa maana hiyo, huwezi kupata harakati zozote zenye kufaulu ila mwanamke atakuwa na fungu lake kubwa humo.

Swahili

Masuala Ya Upande Wa Kike

Baadhi ya watu hujiuliza kuhusu Hijab, kwa nini dini ikawajibisha? Wengine huuliza: Je, inafaa mwanamke afanye biashara, au ukulima?

Wengine wanataka kujua, je! mahari ni thamani (bei) ya mwanamke? Na wengine wanauliza kama inafaa mwanamke mmoja aolewe na waume wengi!

Ama kuhusu Hijab, kwa hakika mtazamo wa dini kwa mwanamke ni mtazamo wa kijumla, yaani ujumla mwanamke ni binaadamu na siyo wa kuji­starehesha naye tu.

Swahili

Haki za Ndoa

Kwa mtazamo wa dini, mke ni mshirika katika maisha; yeye ndiye anayemkamilisha mume na mume ndiye anayemkamilisha mke. Wewe wamuhitajia, naye pia akuhitajia. Mke si mtumishi, bali ni ‘mke’ kwa hivyo anafaa kutumikiwa.

Swahili

Mwanamke Mshirika Katika Maisha

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

“Enyi watu! Hakika tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane. Hakika ahishimiwaye zaidi miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule am­cha­ye Mungu zaidi..” (49:13)

Je, dini zimemdhulumu mwanamke? Wako wasemao hivyo lakini kabla ya kujibu swali hili, kwanza ni lazima tufafanue mambo mawili:

Swahili

Maswali Na Majibu

Sehemu hii ni ya maswali na majibu ya maswali yaliyoulizwa baada ya hotuba iliyotolewa katika Semina hiyo ya "Golden Crescent Group" iliyofanyika mjini Lushoto mnamo tarehe 22 Oktoba 1977.

Swali 1: Je, inaruhusiwa kwa Msichana aliyevaa ushungi kusoma katika Shule za Mchanganyiko (za Wavu….. na Wasichana)?

Jibu: Iwapo msichana huyo atazifunika sehemu zote za mwili ila uso na vitanga vya mikono (toka vifundo vyo kitanga hadi ncha za vidole), basi itaruhusiwa.

Swali 2: Kama jibu ni "Ndio", basi hataweza kujibu maswali atakayoulizwa na mwalimu, je, itambidi anong’one?

Swahili

Umuhimu Wa Hijaabu

Ili kuona jinsi Hijaab ilivyopewa umuhimu katika Sheria za Kiislamu, inatosha kutazama jinsi Sheria na amri nyinginezo zinavyorekebishwa na kubadiliwa ili kuihifadhi sheria ya Hijaab:

(1) Kusali msikitini ni bora kuliko kusali nyumbani. Thawabu huongezeka kwa kadri jamaa iongezekavyo.

Lakini kwa wanawake ni kinyume na hivi. Kuna thawabu nyingi kuswali nyumbani kuliko kuswalia msikitini, na ni thawabu zaidi kuswali katika chumba cha ndani zaidi kuliko kuswali katika baraza au ukumbi.

Swahili

Aya Ya Hijaab

Kwanza, hebu ngoja tuzisome Aya za Qur'ani Tukufu zinazohusu jambo hili. Ziko Aya tatu katika Sura ya An-Nur.

(1-2) Aya mbili za kwanza ni hizi:

"Waambie waaminio wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, hili ni takaso kwao; bila shaka Mwenyezi Mungu Anazo habari za yale wanayoyafanya.

Swahili

Utangulizi

Neno “Hijaab” ni neno la Kiarabu lenye maana ya kisetiri, pazia, buibui, mtandio, au ushungi. Neno hili limetumika katika Qur'ani Tukufu kwa maana ya kuwatenga wanawake kutokana na wanaume wanaoweza kuoana nao, lakini hawakuoana nao (wanaume walio Ghair-Mahram wao).

Hivyo, kwa wanawake wa Kiislamu, kutochanganyika na wanaume wageni na kuvaa buibui au ushungi watokapo nje ya nyumba zao, ni amri ya Mwenyezi Mungu, wala si lolote lile miongoni mwa yale wanayoyafikiria wajinga au yale wanayoyasema maadui wa Uislamu; kama tutakavyoona katika hotuba hii.

Swahili

Shukrani

Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya Urdu na Mtukufu Sayyid al-Ulama Maulana Sayyid Ali Naqi Saheb, Mujtahid wa Chuo Kikuu cha Lucknow, Uhindi.

Kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza na Sayyid Hashim Riza Rizvi, B.A., B.T., Yadgar-e-Husaini H.S. Allahabad, Uhindi na kutolewa na Imamia Mission, Lucknow U.P., Uhindi.

Kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka hiyo tafsiri ya Kiingereza na Bwana J. J. Shou wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania na kikachekiwa na kusahihishwa na Mwalimu Dhikiri (Zakir Ali) U.M. Kiondo, Edita wa "Sauti ya Bilal".

Swahili

Nyongeza

Mifano ya Maandishi na Hadithi za Imamu (a.s.)

1. Jiepushe na kuwa pamoja na mjinga hata kama yu akutakiaye kila la kheri na usijiepushe na mtu mwenye hekima hata kama ni adui yako. Kwani mjinga atakuumiza uhitajipo msaada ambapo utu wa mtu mwenye hekima utamzuia kufanya jambo lililo chanzo cha uadui.

Swahili