Itikadi ya Shi’a Kwa Ufupi
Itikadi ya Shi’a ni itikadi ya Ki-Islamu aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa misingi yake ifuatayo:-
Itikadi ya Shi’a ni itikadi ya Ki-Islamu aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa misingi yake ifuatayo:-
Kuenea kwa vitabu katika siku za hivi karibuni na kuanza kwa mijadala baina ya Waislamu jambo hili limesaidia kuweka wazi ukweli huu - haki ya kufuatwa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s) kwa wengi miongoni mwa maulamaa wa Sunna au wataalamu wao, kwa ajili hiyo jopo la hawa maulamaa wamejiunga na madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s) na wametunga vitabu vilivyojaa dalili zilizo wazi, na haya ni majina ya baadhi yao:
Sheikh Muhammad Maraiy Al-Antwakiy ana kitabu Limadha ikhtartu madhihabash-Shi’ati madhihabi Ahlul-bait (a.s)
Salafia wanakhalifu kundi la Sunnatu wal-Jamaah katika kuchukua mafunzo ya Ki-Islamu, wakati ambapo Sunni wote wamefuata maimamu wanne na wanafanya ibada kulingana na fatwa zao, salafia wanawachukulia mabwana hawa ni kama maulamaa wengine wa waislamu, na wala uislam haujafungamanishwa kwao tu, bali kufahamu uislamu sahihi ni kurejea kwenye kitabu na Sunna kwa kunukuliwa na sahaba yeyote. Na aliyekuja baada yao.
Imethibitika kwamba hakuna dalili ya kufuata madhehebu manne na wengine katika wanaojiita Ahlus-sunna juu ya usahihi wa manhaji yao, sio katika Qur'an wala katika Sunna. Ama wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s) wanayo hazina kubwa kati ya dalili za Qur'an na Sunna juu ya wajibu wa kuwafuata wao, kama tutaweka hoja za Shi’a katika mizani na tukaweka hoja za Ash'ariah (ambazo hazipo) katika upande mwingine wa mizani basi upande wa hoja za Shi’a ungekuwa ni mzito kwa Hadith ya Thaqalayni (vizito viwili) peke yake.
Hoja ya Hadith iko wazi kabisa kwamba nusra ni kupanda safina ya Ahlul-Bait, na maana ya kupanda Safina yao ni kuwafuata wao, kuwaiga, kuwasikiliza na kuwatii, amesema Ibnu Hajar Ashafi: "Kufananishwa kwao na safina kama ilivyotangulia ni kwamba atakaye wapenda, akawatukuza kwa kushukuru neema waliyonayo na akachukua uongofu wa Maulamaa wao ameokoka kutokana na giza la ikhitilalifu na atakayeacha hayo ataangamia katika Bahari ya kukufuru neema na ataangamia katika dimbwi la upotovu.
Amesema Mtume (s.a.w.w) "mfano wa Ahlul-Bait wangu kwenu ni kama mfano wa Safina ya Nuhu, atakayeipanda ataokoka na atakayeiacha ataangamia.
Wameipokea Hadith hii masahaba nane, na wafuatao wamesema ni sahihi:-Al-Haakim katika Mustadrak J: 3 uk 151.
As-Suyutuy katika Nihayatul-Afadhali fiy Manaaqibil-Aali.1
Hadith ya thaqalayni iko wazi katika wajibu wa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Ahlul-Bait (a.s) kwa pamoja, kusalimika kutokana na upotovu haukupatikana isipokuwa kwa kushikamana navyo kwa pamoja kwa kauli yake (s.a.w.w) "kama mkishikamana navyo" na wala hakusema na kimojawapo, na katika yafuatayo ni maneno ya baadhi ya wajuzi wa Ahlus-sunna ambao wanatilia mkazo tuliyoyasema:
Je, kuna dalili?
Swali hili hili ambalo tulilielekeza katika kundi la Sunni tunalielekeza katika kundi la wafuasi wa Ahlul-Bait (a.s); Je, kuna dalili juu ya kufuata Ahlul-Bait (a.s); Je, kuna aya? Kuna dalili nyingi katika vitabu vya Sunni na zote zinatilia mkazo juu ya wajibu wa kuwafuata Ahlul-Bait (a.s) na katika kurasa zifuatazo tutataja zilizo muhimu zaidi.
Baada ya safari hii katika Madrasatul Ash'ariah tumeona kwamba hakuna dalili inayowajibisha kuyafuata, na tumeona baadhi ya matatatizo ambayo yalidhihiri humo, na hii inatupeleka katika wito wa Ushi’a ili tuone waliyonayo.
Linaweza kujitokeza swali katika akili kama Maimamu wamekataza watu kuwafuata wao kwa nini leo tunaona waislamu wanawafuata?