18. Kutokuelewana Na Magomvi

Uislamu unatambua waziwazi kuwa hii njia ya kubuni mambo tu haisaidii kuwa mema. Isipokuwa kanuni zinazotumika na desturi miongoni mwa bibi na bwana ndizo zinazoleta amani katika nyumba.Hotuba kubwa kubwa hazitamsaidia mtu wa kawaida iwapo hayatakuwa kwa mujibu wa akili na vile vile lau hazitakuwa katika uwezo wake.

Ndoa bora za Kiislamu ni zile ambazo bibi na bwana wanapendana na wanaheshimiana na kila mmoja kuheshimu haki za mwenzake.

Swahili

17. Usamehevu

Kama iliyoelezwa hapo awali, hisia za mwanamke ndizo zinazotawala akili zao. Iwapo msichana hatakuwa amelelewa vyema kwa mujibu wa desturi na tamaduni za Kiislamu, basi kuna uwezekano mkubwa sana kuwa atakuwa ni msichana mwenye hasira na ulimi mkali.

Kwa upande mwingine mwanamme sio wa desturi hiyo, kwa hiyo Uislamu umemfaradhia mtu awe na subira na usamehevu wakati wa hasira za mke wake. Inambidi mwanamme amvumilie mke wake kwa kuweka maanani udhaifu wake na kwa kukumbuka kuwa mwanamke anatawaliwa na hisia zake.

Swahili

16. Haki Za Mke

Qurani Tukufu inafafanua misemo ya kuwazulia Waislamu juu ya utumwa wa wanawake katika Islam, swala ambalo wanamagharibi waliomajahili ndio wanaotumia kama silaha dhidi ya Waislamu. Ilikuwa ni dharura katika kuimarisha na kudhibiti hali bora ya nyumbani ili kumzatiti mwanamme katika mamlaka sawa sawa juu ya wanawake. Na Aya hiyo ya Qurani ndivyo inavyofanyia ishara juu yake. Mbali na haya sehemu zote mbili yaani bibi na bwana wamepewa haki zilizo sawia. Kila sehemu wamepata nusu sawa sawa.

Swahili

15. Uzazi

Uendelezaji wa binadamu na asili ya kuwapo kwake na kwa ujumla ni wajibu wa kila aina, vyote viko pamoja na mwanamke. Kwa hakika mwanamke amebarikiwa jambo hilo, yeye anatimiza wajibu wake kwa binadamu kwa ujumla.

Uislamu haujapitiwa (hauja acha kujaali) vile mwanamke anavyobeba mzigo huu na maswala kama hayo katika jambo hili. Uislamu umemuahidi thawabu kubwa kabisa na rehema na baraka za kila aina katika jambo hili gumu mno. Mwanamke inambidi apitie hatua nne katika swala hili, kwanza kushika mimba; pili kuzaa; tatu kunyonyesha na nne uleaji malezi bora ya watoto.

Swahili

14. Kudhibiti Mambo Ya Nyumbani

Kwanza kabisa ni muhimu kuwa mwanamke aweze kuweka maanani mapato ya bwana wake kuliko dunia nzima.

Ndipo hapo itambidi aweze kuweka malengo ya matumizi katika misingi hiyo. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Allah swt atamjalia nguo sabini elfu huko Jannah yule mke ambaye atakuwa ameridhika kwa kiasi cha mapato mume wake anachokipata kwa uwezo wake."

Swahili

13. Utiifu Kwa Misingi Ya Mapenzi

Itatubidi lazima tukumbuke kuwa sheria iliyo ya uchokozi na udhalimu, kamwe haiwezi kuwa sahihi. Hivyo misingi ya mamlaka ya bwana yamewekwa kwa mapenzi na wala sio kwa vitisho na uonevu. Allah swt anatuambia katika Quranii Tukufu sura Ar-Rum 30:21

"..... naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu..."

Swahili

12. Ubora Wa Mwanamme

Kama tulivyoona mapema wazazi ni mabwana wa watoto. Hadi hapo vijana wanaume wanapohusika sheria hii inaendelea.Ama wasichana baada ya kuolewa, ubwana wa wazazi wao unakwisha na wao wanaingia chini ya hukumu za mabwana wao.

Mwanamke mmoja alimwuliza Mtume s.a.w.w.: "Ewe Mtume wa Allah swt, je, ni nani anayo haki zaidi juu ya mwanamme?" Mtume s.a.w.w. alimjibu: "Wazazi wake." Baadaye alimuuliza: "Je! nani mwenye haki zaidi juu ya mwanamke?" Mtume s.a.w.w. alimjibu: "Bwana wake."

Swahili

11. Nafasi Ya Mwanamke Ni Nyumbani

Vyovyote vile, mwanamme amefanywa kuwa mlinzi wa mwanamke, kwa sababu ya mwili wake wenye nguvu, akili na busara yake na kwa sababu amewajibishwa kumstiri na kumshughulikia mke wake. Hivyo kwa sababu hizi na zinginezo mwanamke amelazimishwa kumtii bwana wake.

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: “Wanawake waliotukuzwa kuliko wote mbele ya Allah swt ni wale ambao ni watiifu kwa mabwana zao na ambao wanabakia katika mipaka ya nyumba zao.”

Swahili

10. Haki Za Mwanamme

Qurani Tukufu imekusanya kanuni zote za maisha ya nyumbani. Kama ilivyoelezwa hapo awali, kimaumbile mwanamke ni jinsia dhaifu.Kwa hivyo asitegemewe kujitia katika machachari ya kutafuta maisha; badala yake mwanamme ndivyo inavyombidi atafute kwa ajili ya wote. Iwapo nyumba ni ufalme basi mwanamme ni mfalme na mwanamke ni waziri mkuu.Aya hii ya suratun Nisa inatuelezea vitu vitatu vilivyo vya hakika. Hebu tujaribu kuangalia na kuchambua:-

Swahili

9. Mipaka Ya Kiislamu

Hadi sasa hivi sisi tumekuwa tukiangalia mipaka ya kikudura [yaani mipaka ya kiasilia] ya wajibu wa mwanamme na mwanamke (Yaani wajibu wa bibi na bwana). Sasa hebu tuangalie vile Uislamu unavyoweza kutuongoza katika mipaka ya Dini.

Kama ilivyoelezwa hapo mwanzoni kuwa Uislamu unataka kumwelimisha kijana wa kiume ili anapokuwa awe mtu wa matendo yaani mtu mzima na pia kuwaelimisha wasichana ili wanapokuwa wawe malkia wa nyumba, waweze kutimiza majukumu yao.

Swahili