Utangulizi wa Chapa ya Pili
Shukrani zote ni za Mola wa viumbe, amani na rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Muhammad na Ahali zake wema watoharifu.
Giza halijaacha kueneza nguvu zake za upofu ili kuzuia mwanga wa nuru tukufu ya Mwenyezi Mungu, na linajaribu kuziba kila njia wanayoifikiria wapenzi watukufu katika kuingia humo, lakini jua linatoa mwanga wake juu ya ardhi bila ya kujali mkusanyiko wa mawingu yenye giza nene, ambayo yameafikiana kuzuia nuru yake.