36. Tawba Ndiyo Sababu Ya Kusamehewa

Allah swt anatuambia 'Saabiquu' yaani haraka haraka mtangulie. Je ni wapi huko tena? Basi jibu ni kuelekea kwake Allah swt, hiyo TAWBA inaweza kuwa sababu ya rehema za Allah swt. Faradhi na Sunna zote ni sababu za rehema na Maghfirah za Allah swt. Matendo yote mema ni wasila wa Maghfirah zake Allah swt. Iwapo utauondoa mwiba njiani basi iwe ni kwa ajili ya Allah swt, na ulifanyalo jambo lolote lile, liwe kwa ajili ya Allah swt na yawe yote kwa ajili ya kutaka radhi na maghfirah zake Allah swt.

Swahili

35. Kuiacha Tawba Na Kuendelea Na Madhambi

Imam Muhammad al-Baqir a.s. anaielezea 'kugang'ania hivi; katika Usuli Kafi:

"Iwapo mtu mmoja amefanya madhambi na wala yeye hanuii kuyaacha kabisa na wala hafikirii swala la kufanya TAWBA, basi kwa sababu hiyo itakuwa ni mazoea yake ya kutenda madhambu na hakutakuwa dawa nyingineyo yenye kuponya tabia yake hiyo ila TAWBA tu."

Swahili

34. Katika Tawba Ulimi Ndiyo Mfasiri Wa Moyo

Katika TAWBA, kama tulivyokwisha elezea hapo awali kuwa kitu cha lazima ni kusikitika na kuhuzunika kwa mtu, vile vile kujuta kwa moyo wake wote pamoja na kunuia kwake kuacha madhambi hayo na yote mengineyo. Na katika hisia hizo nzito atamke maneno mazito ya kuomba msamaha wa Allah swt na kusema: 'Astaghfirullah Rabbi wa atubu Ilayhi.'

Swahili

33. Tawba Ni Mlango Wa Rehema

TAWBA ni mlango mmoja mtukufu kabisa wa Rehema za Allah swt na TAWBA ni bahati ya watu wenye imani na wapenxi wa Ahli Bayt a.s. Tujue kuwa hakuna dhambi lolote lile lisiloweza kusamehewa, hata TAWBA ya Makafiri au mapagani pia huweza kukubaliwa.

Lakini mapenzi ya Ahli Bayt ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. ni sharti mojawapo au sivyo mtu anaweza kukosaukubalio wa TAWBA yake hadi kufari dunia.Kwani mapenzi hayo yapo yameamrishwa na Mwenyezi Mungu katika Qurani Tukufu na vile vile Mtume Mtukufu s.a.w.w. pia ametulazimisha kwa hayo.

Swahili

32. Mapenzi Ya Ahli Bayt Huelekeza Kwa Tawba

Watu wenye Imani na mapenzi ya Ahli Bayti Toharifu ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. wanapotokezewa kufanya dhambi, basi ni rahisi kwao kujaaliwa tawfiki ya TAWBA. Allah swt kwa nuru na baraka za Mtume mtukufu s.a.w.w. na ma-Imam a.s.atawafanyia matokeo yao yawe mazuri.

Swahili

31. Majuto Ya Moyoni Yawe Kwa Ajili Ya Allah Tu

Iwapo mtu atasema kuwa mimi nimekwisha fanya TAWBA na huku moyoni hana majuto yoyote ya madhambi, basi huyo ni MWONGO. Kwani uhakika wa TAWBA ni kujuta kwa madhambi aliyoyatenda mtu. Inawezekana mtu akajuta au kusikitika kwa dhambi alizozitenda na wala majuto yake si kwa ajili ya kutaka kufanya TAWBA na vile vile mtu anaweza kujiepusha na matendo ya madhambi kwa sababu za kidunia tu kama vile anahofia asidhurike kwa hasara za kimwili au heshima yake itapotea kwa kujihusisha navyo au anaogopa asije akafungwa jela.

Swahili

30. Je Tawba Iweje?

Kufanya TAWBA ya Allah swt ni jambo la daraja la juu, na iwapo jambo hili likiandikewa kitabu kwa ufafanuzi zaidi, basi kitatokezea kitabu kikubwa mno, lakini sisi hapa tutajaribu kuelezea vile TAWBA inavyotakiwa kufanywa. Iwapo mtu atatokezea kusema kuwa ,mimi nimefanya TAWBA, nimehuzunikia na kusikitikia madhambi yangu, na vile vile nimeomba msamaha wake Allah swt lakini moyo wake haukusikitika au haukuhuzunika na wala hakuacha kutenda matendo ya madhambi. Basi watu kama hawa hawatafaidika kamwe na faida za TAWBA zisizo za Nasuha.

Swahili

29. Tusome Tasbihi Kwa Vidole Kwani Vitatoa Ushahidi Wake

Katika tafsiri 'Ruh al-Bayaan, kwa mukhtasari kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. aliwaambia wanawake kuwa wawe wakisema kwa wingi sana tasbili.

Ipo riwaya nyingineyo isemayo kuwa Mtume mtukufu s.a.w.w. anasema:
"Usiku wa Me'raj nilimwona Malaika mmoja akijenga jengo. Alikuwa akiweka tofali la dhahabu na mara tofali la fedha, na mara nyingine alikuwa akingojea. Mimi nilimwuliza 'je kwa nini unangojea?' Alijibu: "Wakati mja wake Allah swt anapoanza Tasbihi, sisi huwa tunaanza kujenga jengo zuri sana, na mara anyamazapo, nasi pia twangoja.

Swahili

28. Mbele Ya Allah Swt Miguu Na Mikono Vitasema

Baadhi ya Mufassirina wanasema kuwa siku ya Kiyama kitakachoweza kusema ni mdomo tu, je viungo kama mikono na miguu vinaweza kusema?Wao wanasema kuwa hali ya udhahiri wa mwanadamu tu ndio utakaodhihirisha hali yake huyo mtu, na wala si mikono au miguu. Basi hao tunamwambia kuwa 'matamshi' si mahitajio ya ulimi bali ni Allah swt anayejaalia uwezo wa mdomo kutamka maneno. Kutamkwa kwa maneno ni Sifa ya Allah swt na wala si kasoro. Iwapo ingalikuwa hivyo, basi ng'ombe na punda pia wanayo midomo na ulimi hata mirefu kuliko wanaadamu.

Swahili

27. Viungo Vya Mwili Vitatoa Ushahidi Dhidi Ya Madhambi Yetu

Baadhi ya Maulamaa wameelezea ushahidi utakavyokuwa wakati wa Qiyama ambapo sehemu zote na viungo vyote vya mtu vitatoa ushahidi.Allah swt anatuambia katika sura ar-Rahmaan, Aya ya 41:

"Wenye hatia (wenye madhambi) watatambulikana kwa alama zao, na wao watakamatwa kwa nywele za utosi wao na miguu yao." (55:41)

Swahili