16. Kilio Cha Mtubia Bora Kuliko Tasbihi Za Malaika

"Nyie nyote mmeketi hapa katika hali ya 'saumu ' na joto kali, wazee na vijana wetu watakapoomba duaa katka hali hii, basi itakuwa na athari kubwa na sauti hizi tukufu zitafikia hata Malaika." Hayo ndiyo yaliyokuwa yamesemwa na Shahidi Mihrabu, mbele ya umati wa watu.

Swahili

15. Tuifaidi Tawba

Sisi tusiupoteze muhula huu wa TAWBA kutoka mikononi mwetu, na tusije tukaingia makaburini mwetu bila ya kufanya TAWBA, kwani huu ndio mlango wa Rehema. Neema hii ya TAWBA (kurejea katika haki) hubadilisha giza kuwa nuru, baya kuwa jema na vile vile kuuzima moto wa Jahannam. Iwapo utakufa huku umejitwisha mzigo mzito wa madhambi yako, utambue wazi kuwa kaburi ni mahala pabaya sana pa kutokewa adhabu.Lakini iwapo utakwenda huko umeshatubu, basi kaburi ni mahala pazuri kwa waliofanya TAWBA- wingi wa rehema.

Swahili

14. Istighfaar, Kurudia Tawba Na Alfajiri

(d) Kusoma Istighfaar:
Kuhusu TAWBA inatubidi tusome sana Duaa zilizofundishwa na Mtume s.a.w.w.na Maimamu a.s. Khususan Sahifai Sajjadiyyah au Sahifai Kaamila (Dua Na. 31 ipo imewekwa humu mwishoni juu ya TAWBA) na asome 'Munajaati Khamsatashara (munajaat kumi na tano) za Imam Ali a.s. katika Mafatihul Jinaan (funguo za Peponi). Katika duaa hizo tutaona vile TAWBA inavyoombwa na vile tunavyoweza kujihisi kimoyo wakati tuzisomapo.

Swahili

13. Tawba: Saumu, Ghusli Na Sala

Kabla ya kufanya TAWBA, tutimeze aamali zifuatazo:
(a) Kufunga saumu kwa siku tatu:
Al-Imam Jaafer as-Sadique a.s. amesema kuwa Allah amewaamuru
wenye kufanya Tawbatan-nasuha, kufunga saumu katika siku za
Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.
(Wasail, Kitabu Jihad,Babu 88, Uk. 363).

Swahili

12. Kuzidi Kwa Masikitiko

Tawba Ya Mitume

Imeshadhihirika hadi sasa kuwa TAWBA sahihi ni ile ya masikitiko moyoni mwa mtu. Vile itakavyokuwa masikitiko yake zaidi ndivyo hivyo itakavyokuwa msamaha wa madhambi yake. Hivyo tuombe TAWBA zaidi ili madhambi yetu yote yasamehewe. Njia iliyo bora zaidi ni kuisoma Qurani Tukufu na kutafakari juu ya aya zake.

Swahili

11. Uzani Wa Makosa

Mtenda madhambi haimpasi kulifikiria kosa lake kuwa dogo bali daima awe akifikiri kuwa amelitenda tendo au dhambi kubwa mno mbele ya Allah swt. Inambidi aelewe wazi wazi kuwa adhabu, ghadhabu za Allah swt ni kali mno kiasi kwamba hata dunia au mbingu haziwezi kustahimili.

Allah swt anatuambia katika sura Buruuj aya 12:

Hakika kutesa kwa Mola wako ni kukali sana. (85:12)

Vile vile katika sura Muzammil, Aya 12-13 twaambiwa:

Swahili

10.Hali Ya Tawba Kamilifu Na Sunna Zake

Kama ilivyokwisha elezwa kuwa TAWBA ya hakika ni ile ambayo inayotokana na hisia tokea moyoni mwa mtu na kumfanya kujutia matendo yake aliyokwisha tenda.Vile itakavyokuwa masikitiko na majuto ya mtu, ndivyo TAWBA yake itakavyokuwa na ukaribu wa kutakabaliwa. Ikiwa mtu atahisabu dhambi zake kuwa ni kubwa sana basi ndivyo hisia zake za masikitiko na majuto yatakavyokuwa makubwa. Mfano wake ni kama ule wa mtu ambaye amekusanya mali yake yote aliyoichuma maishani mwake na kuchoma kwa moto.

Swahili

9. Darja Za Tawba

Mbele ya Allah swt, TAWBA ni kule kunapomfanya mtu ajirudi (kutoka maasi). Hivyo wafanyao TAWBA ni wa aina zifuatazo:

1.Kurudia Imani kutoka kufuru,yakini kutoka shaka, kuelekea utoshe
lezi kuacha kila akida za ubatili na kuingia katika haki.

2. Kuacha maasi na kuelekea katika utiifu na utekelezaji.

Swahili

8. Kufanya Tawba Papo Hapo Ni Faradhi

Shaykh Bahai (A.R.) anaandika katika kusherehesha 'Arbain' kuwa: "Madhambi huenea mwilini mwa mtu kama vile sumu kali inavyoenea mwilini mwa mtu, basi juhudi za haraka sana zinavyofanywa kuzuia sumu isienee mwili mzima, ndivyo vivyo hivyo inavyotakiwa kufanya TAWBA ya madhambi yaliyokwisha fanywa ili maovu yake yasienee katika mwili mzima.Kuna hatari mbili ya kutokufanya TAWBA, kwanza iwapo atabakia hai, basi kuna uwezekano mkubwa kwake yeye kurejea katika madhambi aliyokwishayatenda na kuongezea mengine kwani alikuwa hakufanya TAWBA, pili iwapo atafariki (kwani h

Swahili

7. Fadhila Za Tawba

(a) Mwenye kufanya TAWBA ni mpenzi wa Allah swt.

Allah swt anasema katika Sura al-Baqarah, Aya 222:-

"Hakika Allah huwapenda wanaotubu........" (2:222)

Al-Imam as-Sadique (a.s.) anasema:

"Allah hufurahia mno toba zifanywazo na Muumin kama vile sisi tunavyofurahi mno wakati tunapomwona rafiki yetu mpenzi aliyekuwa amepotea."(al-Kafi)

Swahili