Hadithi Ya Jabir

Hadithi ya Jabir inafahamika kuwa ni miongoni mwa hadithi wanazozitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi; na imepokewa hadithi hii katika Sihah na Sunan kwa matamko tofauti tofauti, na wanapatikana katika Sanadi zake zote na mapokezi yake wanapatikana watu wawili.

1. Ibnu Juraih
2. Abuz-Zubair.

Na ili kuthibitisha kusihi kwa hadithi hii itategemea kuzifahamu hali za wapokezi wake na watu wa Sanad yake.
Katika maelezo yafuatayo tutaitaja hadithi hiyo kwa matamko mbali mbali tena tofauti:

Swahili

C. Hadithi Ya Abul-Hayyaj

Hivi sasa umefika wakati wa kuichunguza hadithi wanayoitegemea Mawahabi kuharamisha kujenga juu ya makaburi. Kabla ya yote tunaitaja hadithi yenyewe kwa sanadi aliyoipokea Muslim katika kitabu chake.

Swahili

B: Umma Wa Kiislamu Na Kujenga Juu Ya Makaburi

Uislamu ulipokuwa umeenea katika bara Arabu, na nuru yake ikaenea katika sehemu kubwa ya mashariki ya kati, makaburi ya Manabii yaliyokuwa yakifahamika yalikuwa yamejengewa na kuwekwa mapaa yaliyoyafunika.

Baadhi ya makaburi hayo yalikuwa yana Maquba imara na kuna madharih mazuri, na baadhi yake yapo mpaka leo.

Katika mji wa Makka yenyewe utaliona kaburi la Nabii Isma'il na mama yake, Hajirah, yapo katika mahala panapojulikana kama "Hijri Isma'il".

Swahili

A: Mtazamo Wa Qur'an Katika Kujenga Juu Ya Makaburi

Qur'an haikuweka wazi hukumu ya kujenga juu ya makaburi; isipokuwa inawezekana kuifahamu hukumu yake kwa kupitia baadhi ya aya tukufu ambazo zimelizungumzia jambo hili kiujumla.

Hebu fuatilia ufafanuzi ufuatao:

1). Kujenga Juu Ya Makaburi Ya Mawalii Na Kuviheshimu Vitu Vitukufu Vya Mwenyezi Mungu

Hakika Qur'an Tukufu inakichukulia kitendo cha kuheshimu mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu kuwa ni dalili ya ucha Mungu (Utawa).

Swahili

Mawahabi Na Qadhiyyah Ya Kujengea Makaburi Ya Mawalii

Kwa mujibu wa fikra ya Mawahabi, kujengea na kuimarisha majengo juu ya makaburi ya Manabii, Mawalii na Wachamungu ni miongoni mwa mambo yasiyoweza kuvumiliwa.

Swahili

Ibnu Taymiyyah Ni Nani?

Bwana huyu alikuwa ni miongoni mwa wanachuoni wa Kihanbal, na alifariki mwaka 728 A.H. Jina lake ni Abul-'Abbas Ahmad bin 'Abdul-Halim, anayejulikana sana kwa jina la Ibnu Taymiyyah.

Kutokana na rai zake mbovu, na fikra zake zilizo kinyume na itikadi za Waislamu (pamoja na kuwepo tofauti ya kimadhehebu baina yao) Wanachuohi wa zama zake walikuwa wakimpinga na kutangaza vita dhidi yake, isitoshe walimhukumu kuwa hi fasiki (mharibifu wa Dini) na hasa pale alipoandika vitabu vinavyoeleza itikadi zake na akavisambaza miongonini mwa watu.

Swahili

Vidokezo Juu Ya Maisha Ya Muasisi Wa Uwahabi

Madh-hebu ya Kiwahabi yanahusishwa kwa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab kuwa ndiyo muanzilishi wake. Madh-hebu ya Sheikh huyu yameitwa "Wahabiyya" kwa munasaba wa jina la baba yake aliyekuwa akiitwa "Abdul-Wahab".

Swahili

Lengo La Kitabu Hiki

Katika kitabu hiki tumejaribu kuchukua Masail ya msingi ambayo kuna hitilafu ndani yake baina ya Mawahabi na Madh-hebu mengine ya Kiislamu, na kuyatolea hukumu kwa mujibu wa Qur'an Tukufu na Sunna Tukufu ili tufahamu rai ya Uislamu katika Masail hayo.

Na kitabu hiki siyo pekee ambacho tulichoandika kuhusu maudhui hizi, bali kimetanguliwa na vitabu vitatu na kila kimoja miongoni mwa hivyo kimebeba jukumu la kuchunguza na kuhakiki baadhi ya Masail haya, na vitabu hivyo ni:

Swahili

Mwito Wa Kufanyika Kongamano La Kiislamu

Kwa hakika ni muhimu sana kufanyika kongamano la Kiislamu ambalo ndani yake yatatatuliwa Masail yenye Khitilafu kwa mujibu wa muongozo wa kielimu na Mantiq na dalili, kwani wakati huu wa sasa ziko khitilafu kubwa mbili ambazo ni Uwahabi na madhehebu mengine ya Kiislamu juu ya Tauhidi na shirki, basi Je, kwa lengo la kukurubiana pande hizi mbili si inafaa kufanya mkutano wa kielimu ambao Masail haya yataaridhiwa katika meza ya uchunguzi na uhakiki kwa lengo la kuondoa batili na kuithibitisha haki, kwani huenda ikachomoza nuru ya kuonyesha njia kwa wanaobabaika?

Swahili

Kiasi Chenye Makosa

Tunakwenda sambamba na mwandishi huyu wa Kiwahabi katika kitabu chake kisichokuwa na maana, na tunamuona anamkosoa Imam Ali ibn Abi-Talib [a] kwa njia ya kutaka kufahamu na kuuliza sababu za kufanya haraka kumuuzulu Muawiyah mara tu Imam Ali [a] alipotawalia (Ukhalifa) na anajiuliza anasema: Kwa nini, kwa nini?

Swahili