Tauhidi Katika Ibada

Msingi wa wito wa Manabii [a] siku zote umekuwa ni kulingania kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na siyo kumuabudu mwingine peke yake, au kumshirikisha na Mwenyezi Mungu. Na msingi wa hukmu za mbinguni tangu mwanzo wa kutumwa ujumbe wa Manabii ilikuwa ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kukata mizizi ya shirki.

Ukweli halisi ulivyo ni kwamba, lengo la kutumwa kwa Manabii ni kulingania (watu) kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake, na kupiga vita ushirikina wa aina zote na khususan kupinga shirki katika ibada.

Qur'an Tukufu inaashiria ukweli huu wazi wazi na inasema:

Swahili

Kutabaruku Na Sera Ya Waislamu

Mtazamo wa haraka katika sera ya Waislamu kuanzia kwa Masahaba mpaka leo, unatuonyesha wazi sunna inayofuatwa kuhusu kutabaruku kwa Mtume [s] yeye mwenyewe na athari zake tukufu katika kpindi chote cha historia ya Uislamu.

Na katika maelezo yafuatayo tutaeleza mifano michache inayohusu kutabaruku:

Bibi Fatimah Az-Zahra ambaye ndiye mwanamke bora ulimwenguni na ni binti ya Mtume [s], alifika kwenye kaburi la baba yake na akachukua gao la udongo wa kaburi akawa anaunusa na kulia huku akisema:

Swahili

Mtazamo Wa Qur'an Juu Ya Kutabaruku

Katika Qur'an tunatosheka na aya moja tu, nayo ni ile inayomnukuu Nabii Yusuf [a] akisema:
"Nendeni na kanzu yangu hii mukaiweke usoni kwa baba yangu (macho yake yatarudi) ataona." Qur'an, 12.93.

Nabii Yusuf aliituma kanzu yake kwenda kwa baba yake na akawaambia ndugu zake "Nendeni na kanzu yangu hii na muiweke usoni kwa baba yangu ili macho yake yarudi apate kuona.

Mwenyezi Mungu anasema: "Na alipokuja mtoaji habari njema, aliiweka kanzu ile usoni kwake na macho yalirudi akaona." Qur'an, 12:96.

Swahili

Kutabaruku Kwa Athari Za Mawalii Wa Mwenyezi Mungu Na Kuomba Uponyo

Mawahabi wanaitikadi kwamba kutaka baraka kwenye Athari za Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Mawahabi pia wanamuona kuwa ni mshirikina mtu ambaye ataibusu mihrabu ya Mtume [s] na mimbari yake, japo hatafanya hivyo kwa nia ya ibada, isipokuwa ni kwa ajili tu ya mapenzi yake kwa Mtume [s] ndiyo maana katabaruku na kutaka uponyo kwenye Athari zake.

Swahili

Maneno Na Matendo Ya Mawahabi Yanapingana

Ajabu waliyonayo Mawahabi ni kama ifuatavyo:

Ni vipi wanaharamisha hafla ya utajo na uzawa mtukufu wa Mtume [s]; Mtume ambaye ndiye aliyewapa wanaadamu wote zawadi kubwa kuliko zote tena ya kudumu (nayo ni Uislamu) na tena Mawahabi kwao wao wanaona kumheshimu Mtume [s] na kuadhimisha uzawa wake ni shirki, lakini wao hao hao ndiyo wanaofanya maadhimisho makubwa kwa ajili ya watu wao na viongozi wao, na wanatoa mamilioni ya Riali (pesa za Kisaudia) ili kufanya maadhimisho haya na ili kuonyesha heshima kwa utumishi wa hao viongozi wao?

Swahili

Kuadhimisha Kuzaliwa Kwa Mawalii Wa Mwenyezi Mungu Na Kufa Kwao

Je, kuadhimisha uzawa na vifo vya Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni Bid'a?
Hakika Mawahabi wao wanadai kuwa, kufanya maadhimisho hayo ni haramu.... kwa madai yao haya, wanaonyesha wazi chuki na uadui walionao dhidi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu na viongozi wa Uislamu, hasa pale wanapozuwia kufanyika mikusanyiko ya kusherekekea kuzaliwa kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na ile ya kuomboleza vifo vyao.
Wahabi mmoja ambaye ni Rais wa kikundi cha "AnsarusSunnatil-Muhammadiya" aitwaye "Muhammad Hamid Faqii", katika hashiya yake juu ya kitabu kiitwacho Al-Fat-hul-majid anasema:

Swahili

Kuwawekea Nadhiri Watu Waliokufa

Kabla ya kueleza chochote, tunataja kwanza "Taarifu" ya "Nadhiri".

Maana ya nadhiri ni mtu kuilazimisha nafsi yake kutenda kitu maalum iwapo makusudio yake yatatimia au haja yake ikikubaliwa, na atasema wakati awekapo nadhiri, kwa mfano: "Ni wajibu juu yangu iwapo nitapasi mtihani nitahitimisha Qur'an kwa ajili ya Mwenyezi Mungu."

Hii ndiyo nadhiri ya kisheria, na ni lazima iwekwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu.

Swahili

Baadhi Ya Maandiko Yaliyoandikwa Kuhusu Tawassul

Inafaa tuashirie baadhi ya vitabu vinavyotegemewa vilivyoandikwa na wanachuoni wa Kisunni kuhusu kutawassal kwa Mtume Mtukufu [s], na pia kuvirejea vitabu hivi kutayaweka wazi maoni ya wanachuoni wa Kiislamu juu ya kutawassal kwa Manabii na Mawalii, na kutia nguvu kwamba kutawassal tangu hapo mwanzo lilikuwa ni jambo linalotendeka na ni sunna iliyokuwa ikifuatwa na Waislamu siku zote kinyume cha wanavyodai Mawahabi.

Swahili

Ushairi Wa Safiyyah Akiomboleza Kifo Cha Mtume [s]

Bibi Safiyyah binti Abdil-Muttalib (Shangazi ya Mtume) alisoma Qasida baada ya kufariki Mtume [s] kuomboleza kifo chake, na sehemu ya Qasida hiyo ni hii ifuatayo:

"Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wewe ndiyo matumaini yetu, ulikuwa mwema wetu na wala hukuwa mnyanyasaji, na ulikuwa mwema mpole ewe Mtume wetu, basi leo na akulilie yeyote mwenye kulia."1

Swahili

Mwenendo Wa Waislamu Katika Tawassul

Sera ya Waislamu katika zama za uhai wa Mtume [s] na baada ya kufa kwake inakubaliana na kutawassal kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu na kuomba uombezi kupitia vyeo vyao na heshima zao mbele ya Mwenyezi Mungu.

Ifuatayo ni mifano ya sera hiyo ya Waislamu.

1. Ibn Al-Athir mwana historia mashuhuri aliyefariki mwaka 630 anaandika hivi:

Swahili