Utangulizi

Hamna shaka kuwa historia ya mwanadamu ndio chemchemu na chanzo cha maarifa, chanzo ambacho mataifa yanakihitaji katika safari yake yenye kuendelea. Na ndio chanzo pekee chenye uwezo wa kuhuisha na kulisukuma taifa mbele na kulipa sifa na hadhi maalum huku kikilifunganisha taifa hilo na mizizi yake ya ustaarabu ambayo hulizuwia taifa dhidi ya mmong'onyoko.

Swahili

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho Tarikh wa Sirati ‘l-Qadati ‘l- Hudaah. Sisi tumekiita, Historia na Sira ya Viongozi Waongofu.

Swahili

Uharamisho wa Riba

Dhambi la riba ni miongoni mwa Madhambi Makuu. Dhambi hili limeelezwa vyema kabisa katika riwaya na Ahadith za Mtume Muhammad s.a.w.w., Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Al-Imam Ja’afer as-Sadiq a.s., Al-Imam Musa al-Kadhim a.s. na Al-Imam Muhammad at-Taqi a.s.

Kwa mujibu wa Qur’an tukufu, kuchukua riba ni dhambi ambalo linasababisha adhabu kali kabisa kutoka kwa Allah swt. Adhabu za kuchukua na kutoza riba ni kali kabisa kuliko madhambi mengine. Kama ilivyoelezwa katika Surah Aali Imran, 3, : 130 - 131:

Swahili

Maneno Mawili

Kama inavyoonekana katika picha ya ukurasa wa kwanza, utaona kuna kifurushi cha fedha zilizo kidogo yaani mkopaji anapokopa hukopa kidogo na anaporejesha, hurejesha kifurushi kinono, kama kinavyojionesha. Yaani tuseme riba inamnyonya mnyonge anakwisha na kinamnenepesha mtoza riba.

Vile vile unaweza kufaidika kwa kupata vitabu na Makala yanayozungumzia maswla mengi mno katika internet kwa anwani ifuatayo :
http://www.al-islam.org/sw

Swahili

Uharamisho wa Uwongo, Juzuu ya Kwanza

Kimekusanywa na kutarjumiwa na
Amiraly M H Datoo
Bukoba - Tanzania

Maneno Mawili

Namshukuru Allah swt pamoja Mtume Muhammad s.a.w.w. na Maimamu a.s. kwa kunijaalia kukitayarisha kitabu hiki.

Ni matumaini yangu kuwa maudhui haya yatawafaidisha na kutuelimisha sisi sote ili tuweze kujiepusha sisi wenyewe na tusiwachochee wengine wakatumbukia katika ugonjwa huu wa kusema uwongo.

Swahili

Uharamisho Wa Kusema Uwongo

Uharamisho Wa Kusema Uwongo1
Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu Surah An-Nahl,16, Ayah ya 105 :
‘Wanaozua uwongo hawana imani’

Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :
Mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni msema uwongo.”

Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema :
Allah swt humlaani mwongo hata kama atasema ukweli”

Swahili

Maneno Mawili

Namshukuru Allah swt pamoja Mtume Muhammad s.a.w.w. na Maimamu a.s. kwa kunijaalia kukitayarisha kitabu hiki.

Ni matumaini yangu kuwa maudhui haya yatawafaidisha na kutuelimisha sisi sote ili tuweze kujiepusha sisi wenyewe na tusiwachochee wengine wakatumbukia katika ugonjwa huu wa kusema uwongo.

Vitabu vingine pia vimetayarishwa katika mfululizo huu wa kuyarekebisha na kuyatokomeza mabaya katika jamii yetu kama :

1. Uharamisho wa Kamari

2. Uharamisho wa Ulevi

3. Uharamisho wa Riba

4. Uharamisho wa Uwongo (juzuu ya kwanza)

Swahili

Ukweli Katika Minyororo (Imamu Ali Naqi)

Imamu Katika Qur'an Na Hadithi

Mwenyezi Mungu anasema:

(Ewe mwanadamu! Ikumbuke) siku Tutakapowaita kila watu pamoja na Imamu wao; basi atakayepewa kitabu (chake cha Amali) kwa mkono wa kulia, hao watavisoma vitabu vyao (kwa furaha); (Bani Israel, 17:71)

Mtukufu Mtume [s] amesema:

"Yeyote yule afaye pasi na kumjua Imamu wa zama zake, atakuwa kafa kifo cha ujinga."

Mtukufu Mtume [s] amesema:

Swahili

Walid Na Harun Rashid

Na haikukomea hapo tu. Inaonyesha kuwa matendo haye yalikuwa yakitendeka mara kwa mara. Walid bin Yazid bin Abdul Malik alikuwa Khalifa mwingine wa ukoo wa Bani Umayyah. Yeye alikuwa mlevi. Usiku mmoja alikesha akinywa pombe na mmoja wa suria wake hadi waliposikia Adhana ya Sala ya Alfajiri. Walid akaapa kuwa yule suria wake atasalisha. Hivyo yule suria akavaa joho la Khalifa na akasalisha katika hali ile ya ulevi na uchafu.

Swahili

"Ulul Amr" Ni Nani?

Allah Anasema katika Kitabu chake kitukufu:

"Enyi mlioamini Mtiini Allah, na mtiini Rasuli (Wake Muhammad) na Wale waliopewa mamlaka kutoka miongoni mwenu, ...... (Qur'ani, 4:59)

Aya hii inawawajibisha Waislamu aina mbili za utii. Kwanza, kumtii Allah; Pili kumtii Rasuli. Hii ina maana kwamba ni lazima "Ulul Amr" wawe na cheo kama kile cha Rasuli; au sivyo Allah asingetuamrisha kuwatii wao na kule kumtii Rasuli, katika Aya hii.

Swahili