Utangulizi
Waislamu wamegawanyika makundi wawili kuhusu maana ya maneno "Ulul-Amr" yaliyotumika katika Aya ya 59 ya Surat An-Nisa.
Wako wasemao kuwa maana ya maneno haya ni "Watawala kutoka miongoni mwenu" - yaani watawala wa Kiislamu; na hii ndio tafsiri ifuatwayo na Waislamu walio wengi (Masunni).
Wako wengine wasemao kuwa, maana ya maneno hayo ni "Makhalifa (au Maimamu) Ma’asumiin (Watakatifu) Walioteuliwa na Allah kushika mahali pa Mtukufu Mtume [s] baada ya yeye Mtume [s] kuondoka. Hii ndio tafsiri ifuatwayo na Mashia-lthna-ashariyah.