Sura Ya Saba

Zipo nasaha nyingi ambazo Mtume alimpa Abu Dharr. Hapa tunadokeza kuhusu chache miongoni mwao. Muhammad Harun Zangipuri ameandika ka mujibu ya mamlaka ya ‘Amali’ ya Shaykh Tusi kwamba Mtume alimwambia Abu Dharr:

“Ewe Abu Dharr! Muabudu Mwenyezi Mungu kama vile unamuona Yeye, na Yeye Anakuona wewe na hata kama humuoni wewe.”

“Tambua kwamba kwanza kabisa ibada Yake ni kumtambua, yaani kuelewa kwamba Yeye ni wa kwanza kabla ya chochote. Yeye hana mshirika. Yeye ni wa Milele hana mwisho.”

Swahili

Sura Ya Sita

Shahidi Thalit Allamah Nurullah Shustari ameandika:
Abu Dharr alikuwa mmoja wa masahaba mashuhuri sana na anahesabiwa miongoni mwa masahaba wa mwanzo kabisa walioingia kwenye Uislamu. Katika kuukubali Uislamu alikuwa mtu wa tatu, hivyo kwamba, aliingia kwenye Uislamu baada ya mama wa Waumini Khadijahtul Kubra na Amiri wa Waumini Ali. Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu cha ‘Isti’ab’ alikuwa na sifa ya juu katika ujuzi, kushikilia maadili, uchaji Mungu na kuwa mkweli, miongoni mwa masahaba wote.

Swahili

Sura Ya Tano

Historia inashuhudia kwamba Abu Dharr alielimika sana baada ya kuwa Muislam hivyo kwamba hapakuwepo wa kumlinganisha naye miongoni mwa masahaba. Alipata utakaso ulio bora wa imani na unyofu wa moyo hivyo kwamba alihakikisha kwamba yeye ni nguzo ya nuru kwa watu wenye utambuzi. Alizirutubisha akili za watu kwa ushauri, baada ya kuja kwa Uislamu, aliwafundisha watu masomo ya usawa na upendo na aliwafundisha jinsi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume.

Swahili

Sura Ya Nne

Abdul Hamid Jaudatus Sahar wa Misri ameandika, Uislamu ulienea Madina kama moto wa mbuga ya majani makavu.” Kabila la Ghifar lilifurahishwa sana na hali hiyo. Waislamu walipongezana wao kwa wao kwamba makabila mawili ya Aus na Khazraj, ambao walikuwa wasemaji sana, wapiganaji wazuri sana na waunga mkono wazuri sana walikubali kuingia kwenye Uislamu, na pia kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikwisha ridhika kuinyanyua dini Yake na alinuia kumsaidia Mtukufu Mtume na kutimiza ahadi yake.

Swahili

Sura Ya Tatu

Baada ya kuingia kwenye Uislamu, Abu Dharr aliondoka Makkah kwenda nchini kwake. Abdullah Subaiti ameandika kwamba Abu Dharr alipoondoka, alikuwa anabubujika imani, kamili, na alikuwa na furaha sana. Alifurahia sana kwamba Mwenyezi Mungu, alimwongoza kwenye imani ambayo imekubaliwa na waliotakasika na dhamira imeridhika nayo na akili inakaribisha kwa ukamilifu.

Swahili

Sura Ya Pili

Baada ya kumsikiliza kaka yake, Abu Dharr alisema, “Sijaridhishwa na ripoti yako. Nitakwenda huko mimi mwenyewe, nimuone na nimsikilize mimi binafsi.”

Abu Dharr alifika Makkah, aliingia kwenye eneo la Ka’abah na akaanza kumtafuta Mtume, lakini wala hakumuona pale, ama kusikia akitajwa. Alikaa hapo hadi machweo ya jua. Ali aliwasili hapo na akapita karibu na pale alipoketi Abu Dharr. Alimuuliza, “Unaonekana kuwa msafiri. Ni kweli?”

Abu Dharr: “Ndio.”
Ali: “Njoo nifuate.”

Swahili

Sura Ya Kwanza

Abu Dharr alikuwa mmojawapo wa hao masahaba wa Mtume wa Uislamu, Muhammad (s.aw.) ambao walikuwa wachaji Mungu na wapenda uhuru na walikuwa na tabia bora kwa mujibu wa maneno ya Mtukufu, Mtume: Pepo na wakazi wake wanawangojea kwa hamu. Alifaidika kuwa na Mtume katima uhalisi wake.

Abu Dharr mwenyewe anasema, “Jina langu halisi ni Jundab bin Junadah, lakini baada ya kuingia kwenye Uislamu, Mtume alinipatia jina la ‘Abdullah’ na hili ndilo jina ninalolipenda hasa.”

Swahili

Utangulizi

Baada ya miaka kumi na tatu ya mfululizo wa mateso na mapambano, Mtume wa Uislamu aliondoka Makkah na kwenda Madina. Alihisi kwamba kipindi cha uvunjaji sheria na kutangazwa kwa siri kwa Uislamu kilikwisha na kwa msaada wa masahaba wake waaminifu na jasiri angeweza kujenga jumba kubwa la dola ya Kiislamu na kuweka msingi wa serikali ya kisiyasa kama anavyotaka Mwenyezi Mungu.

Swahili

Kuhusu Wachapishaji

Leo hii akili yenye hadhari inaona kiakili mabadiliko ya maisha ya mwanadamu. Sayansi na teknolojia na mafanikio yao ya kushangaza yanaonekana yamefika kwenye kilele chao. Mahitaji ya kidunia hisia kali za matamanio ya mamlaka na ukubwa, ni mambo ambayo yamemwelekeza mwanadamu kwenye muflisi wa maadili mema.

Swahili

Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jina la: “Abu Dharr”

Kitabu hiki kinahusu maisha ya Sahaba mkubwa na mashuhuri; Abu Dharr (Jundab bin Junadah). Abu Dharr alikuwa mtu wa tano kuingia kwenye Uislamu na upanga wake ulikuwa unafaa sana katika kuendeleza Uislamu. Aliona mikengeuko mingi katika Uislamu tangu kuanza kwake, na baada ya kifo cha Mtukufu Mtume mambo hayakuwa mazuri.

Swahili