Sura Ya Kumi Na Saba

Ni ukweli ulio thabiti kwamba Abu Dharr alikuwa karibu sana na Mtukufu Mtume na Ahlul Bait wake na aliendelea kuwa msiri wao mkubwa. Aliona kwa uangalifu sana kila kipengele cha maisha yao, na alijifunza mengi kutokana nao. Ameona kwa macho yake si mara moja lakini mara nyingi kwamba Mtukufu Mtume alikuwa anajilaza msikitini akiwa na njaa na watoto wake nyumbani walikuwa na njaa. (Alaimun Nubuwwah, al-Mawardi, uk. 146 chapa Misri).

Swahili

Sura Ya Kumi Na Sita

Kama tulivoeleza kwa ufupi kwenye kurasa za nyuma, Uthman, alikua anagawa fedha ya Waislamu miongoni mwa ndugu zake tu huku anawanyima haki watu masikini. Abu Dharr, kwa ajili ya ushupavu wake wa kidini katika kufuatilia mafundisho matukufu ya Mtume, alilazimika kupiga kelele kukemea maovu hayo. Matokeo yake alipelekwa Syria. Halafu aliitwa kutoka Syria na kurudi Madina kwa namna ya kuadhibiwa. Akawekwa katika taabu nyingi.

Swahili

Sura Ya Kumi Na Tano

Abu Dharr alipokuwa anaondoka, watu walimsindikiza kumuaga hadi walifika Dair Maran sehemu iliopo nje ya jiji. Hapo aliswali Swala ya jamaa. Halafu akahutubia watu na tafsiri yake ni kama ilivyotolewa na Hayatul Qulub.

Swahili

Sura Ya Kumi Na Nne

Abu Dharr alikuwa mtu mkweli. Alikuwa anawaonya watu wengine wafanye matendo mema. Muawiyah alikuwa mtu aliyependa mambo ya dunia. Kila mara Abu Dharr alikuwa anamwelekeza kufanya matendo mazuri hadi watu wa Syria walianza kuona aibu. Siku moja Muawiyah alimwambia Abu Dharr, “Wewe si muadilifu kiasi cha kunielekeza mimi kufanya matendo mema mbele ya umma.” Aliposikia hivi Abu Dharr akasema, “Nyamaza! Huoni hata aibu!”

Swahili

Sura Ya Kumi Na Tatu

Waandishi wa historia wanasema kwamba Uthman alipochoshwa na kilio cha kutetea ukweli cha Abu Dharr alimfanyia kila aina ya ugandamizaji huko Madina. Amri yake ilikuwa hakuna ruhusa mtu yeyote kusema na kukaa naye. Alilazimishwa kunyamaza, lakini kilio chake cha kutetea ukweli kiliendelea.

Swahili

Sura Ya Kumi Na Mbili

Abdul Hamid wa Misri na Allamah Abdullah Subaiti wameandika kwamba Abu Dharr alikaa Madina baada ya kifo cha Umar. Aliona kwamba Uthman alikuwa anawapendelea Bani Umayyah ambao mvuto wao ulipenya kwa kina kirefu katika serikali ya Kiislamu ambapo ilikwisha pata utukufu wa himaya. Watu waliendekeza ufahari na maonesho na waliishi maisha ya anasa sana. Watu walipendelea zaidi pato la dunia.

Swahili

Sura Ya Kumi Na Moja

Abu Dharr, kwa sababu ya desturi yake, mwenendo wake, tabia na amri ya Mtume, alishindwa kunyamaza inapobidi alisema kweli na aliishi maisha ya kimya. Kazi kubwa zaidi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu ilikuwa kukaa karibu na kaburi la Mtume na kuwasifu Aali Muhammad (Uzao wa Mtume).

Inaonekana na kwenye vitabu vingine vya historia kwamba Ali alimshauri afuate sera ya upole. (Nasikhul Tawarikh, Juz ya 2, uk. 803).

Swahili

Sura Ya Kumi

Baada ya kifo cha Mtume, wale masahaba ambao hawakuridhika kwa kitendo chake cha Ghadir Khum ambao walimpinga Ali, haraka sana walikusanyika Saqifah Bani Sadah mahali ambapo palitayarishwa maalumu kwa mashauriano yasiyofaa (Ghayathul Lughaat) na watu wachache wapatao 200 ambao walikuwemo Muhajirina na Ansar waliokubali na wasikubali walikuwemo, walianzisha msingi wa serikali ya mtu binafsi. Waliporudi Madina kutoka Saqifa, baada ya maziko ya Mtume, walianza kudai kiapo cha utii kutoka kwa watu kwa lengo la kupatia serikali hiyo ya kibinafsi sura ya pamoja na aina ya kidemokrasia.

Swahili

Sura Ya Tisa

Wataalamu wa historia na wahadithi wa madhehebu yote mawili (Shia na Sunni) wanakubaliana kwamba pale ambapo Mtume (s.a.w) alitaka kuanza safari yake ya kwenda kwenye hija yake ya mwisho, alitangaza waziwazi kwamba masahaba wote lazima wafuatane naye kwenye safari hiyo.

Baada ya tangazo hili, masahaba wa Mtume walianza kufika Madina kutoka sehemu zote. Pia aliwataarifu watu kwamba wale ambao hawangeweza kufika Madina, waende Makkah moja kwa moja ili wahiji pamoja naye.

Swahili

Sura Ya Nane

Masimulizi ya hadithi ni kitu chenye muhimu mkubwa. Wala si kila mtu anaruhusiwa kusimulia, ama kusikiliza simulizi zao. Ujuzi wa wahadithi ndio kipimo chake. Abu Dharr ni mmojawapo wa wasimulizi wa kuaminika, kutegemewa na wakweli ambao simulizi zao hazitiliwi shaka au kukataliwa. Amekuwa na Mtukufu Mtume kwa muda mrefu sana wa uhai wake. Kwa maelezo yake ni mengi sana miongoni mwa hayo, machache yameandikwa hapa.

Swahili