Sheria za Kiislamu katika Zama Hizi
Katika sehemu nyingine ya mjadala wangu, kuna masuala mengine mengi ya kujadiliwa lakini hapa nitayataja kwa muhtasari tu. Uislamu una mfumo mahsusi wa utungaji wa sheria. Ajabu ya mfumo huo ni kuwa sheria zake zinaweza kwenda sambamba na maendeleo ya zama, na hata zinaweza kuwa ni mwongozo kwa maendeleo na wakati huohuo zikaweza kupambana na upotovu na ufisadi.