Somo La Kumi: Mwonekano Wa Utu Wa Imam Ali Bin Abu Talib (A.S.)
Sifa za ukamilifu zilikusanyika kwa Imam Ali bin Abu Talib. Alikuwa na sifa nzuri za kusifika, mahsusi za kupendeza, nasaba bora na sharafu tukufu, asili takatifu na nafasi yenye kuridhiwa. Sifa ambazo hakubahatika kuzipata mtu yeyote mwingine, kwani yeye ni jemedari wa waumini, mbora wa mawasii na khalifa wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w.) kati ya makhalifa waongozao kwa amri ya Mwenyezi Mungu.