Majadiliano Juu Ya Ufumbuzi
1. Wakati tunapoomba kwa Allah (s.w.t.) kuwaachilia wafungwa wote, hatuombi kuachiliwa kwa kila aina ya mfungwa, awe mfungwa wa Allah au mfungwa wa Shetani. Bali tunaomba kwa ajili ya wale wafungwa wote ambao ufungwa wao huwazuia kutokana na ufanisi wa kimwili na kiroho. Hata hivyo, wokovu kutokana na ufungwa wa kiroho kama tulivyotaja hapo juu, uko mikononi mwa mfungwa mwenyewe. Kama akiamka kutoka kwenye usingizi wake mzito na kubadilisha tabia zake mbovu, atajipa uhuru yeye mwenyewe.