Dajjal
Ni neno la Kiarabu likimaanisha mhaini mkubwa na mleta balaa kubwa mno.Hivyo wale wote walio wahaini na waleta balaa basi wajijue kuwa wao pia na ma-Dajjal wa zama zetu hizi.Lakini Dajjal anayezungumziwa hapa ni yule ambaye anaitwa Sayyid na utambulisho wake ni Dajjal.Yeye atakuwa ni mchawi mkubwa.Hapo mwanzoni atakapojitokeza atadai kuwa yeye ni mtume na baadaye atajiita kuwa yeye ni mungu.Yeye atatokezea pale ambapo Mashariki ya kati itakuwa imekwisha dhoofika kwa sababu ya ukame utakaodumu kwa miaka mitatu kwa mfululizo.