Mashi’a na Uandishi wa Hadith

Kwa kuwa riwaya (desturi) ya uandishi wa Hadith ilikuwapo miongoni mwa Shi’a tangia mwanzoni, wao walikuwa wanaongoza katika uandishi wa Hadith na Fiqh.
Dr. Shawqi Dayf anaandika:

Swahili

Historia ya Uandishi wa Hadith Katika Sunni

Kazi zote zilizopo hadi leo zinazohusu Hadith zilikuwa zimekusanywa katika kipindi cha karne 2 A.H./8 A.D. au katika karne ya 3 A.H./9 A.D. Historia inatuonyesha kuwa katika kukaribia karne ya 2 A.H. kulitokezea idadi ndogo ya Muhaddithun ambao walianza kuziandika Hadith, ingawaje hazikuwa na mpangilio. Baadaye mkusanyiko huu mdogo ulikuwa kiini cha kazi zote kubwa. Hata hivyo wingi wa Hadith zilizopo sasa kwa kukusanywa, zilienezwa kwa desturi ya kutamkwa (kusemwa), na wakati zilipokuja kuandikwa vitabuni, zilikuwa hazikuwahi kuandikwa popote kabla yake.

Swahili

Sababu za Uchelewesho Katika Uandishi wa Hadith

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume s.a.w.w., kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi (na kusisitiza) kuhusu uandishi wa Qur’an (kama hatua ya kinga dhidi ya kughushi na uongo). Kimatokeo Qur’an ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif).

Swahili

Hadithi ni Nini ?

Mawaidha na Nasiha, maneno aliyoyazungumza Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ni Hadith kwa kifupi, maneno yoyote yaliyotoka mdomoni kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mbali na ayah za Qur'an Tukufu, ama yale aliyoyatenda kuonyesha, hayo yote ni Hadith. Vile vile maneno na matendo yote ya Ma’asumin a.s. pia ni Hadith yaani yataingizwa katika Hadith. Kutokana na Hadith sisi tunaweza tukajua na kufuatilia na kutekeleza mambo ambayo ni Usuli, Furu’, Sunnah na Faradhi.

Swahili

Shi’ah na Hadith

Kwa hakika Mashi’ah wana mchango mkubwa sana katika uandishi wa Hadith na katika hali ambayo ni sahihi. Na wa kwanza kabisa ni mchango wa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambao hauna kifani wala usioelezeka, Je! litakuwa ni kosa gani iwapo wafuasi wake watamfuata yeye katika kuzidumisha na kuzihifadhi Sirah na sunnah za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.? Katika historia vile vile tunapata mambo yaliyowazi kabisa kuwa kulikuwa na baadhi ya Ma-Sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Swahili

Mtunzi Na Habari Zake

Kitabu hiki cha Sadaka ambacho kipo mikononi mwenu, Hadith zake zimetolewa kutoka Wasa’il as-Shi’ah na tunaona vyema kuwaleteeni habari chache kuhusu kitabu na mtunzi wake.

Sheikh Hurri ‘Aamili baada ya jitihada zake nyingine kwa muda wa miaka ishirini mfululizo amekigawa kitabu hicho katika sehemu sita katika fani mbalimbali na kuzigawia Hadith kimpangilio mzuri kabisa na kwa hakika anastahili pongezi kubwa sana kwa jitihada zake zote katika kuzipanga Hadith kimpangilio mnavyouona katika kitabu hiki pia.

Swahili

Utambulisho wa Ma’sumiin a.s.

Swahili

Mwenye Kuripoti Ahadith Aweje?

Kwa hakika somo hili ni kubwa na lenye kwenda kwa undani zaidi, lakini kwa ajili ya wasomaji, tunawaleteeni habari hizi kwa kifupi ili kuwafaidisha.

Katika lugha ya Kiarabu, mtu anayeripoti riwaya huitwa Rawi na sifa zake zimeelezwa na kubainishwa na Ma’ulamaa walio mabingwa wa ilimu ya Ahadith:

1. Rawi lazima awe mtu mwenye akili na fahamu timamu. Riwaya zozote zitakazotolewa katika hali ya kuwehuka au kurukwa na fahamu, basi hazitathaminika au kukubalika.

Swahili

Aina Za Ahadith

Sayyid Ibn Taus a.r. (amefariki 673 Hijriyyah) na ‘Allamah Hilli a.r. (amefariki 726 Hijriyyah) kwa juhudi zao, wao wamefanikiwa kutuletea kanuni nne kuu zijulikanazo usul-i-‘arbi’ah ambazo ni kama zifuatazo:

1. Hadith Sahih

Rawi wote lazima wawe waaminifu na Shia Ithna-Asheri na riwaya hizo ziwe zikifika hadi kwa Ma’sumiin a.s.

Swahili

Hadith Zilizoghushiwa

Kwa mujibu wa kanuni hizi nne, mmefahamu kuwa Hadith inapoangukia kuwa dhaifu haimaanishi kuwa ni Hadith ya uongo, yenye mfululizo dhaifu, na kwa dalili zinginezo na kwa nyenzo zinginezo inaweza kuthibitika kuwa Hadith hiyo inaweza kukubalika, lakini inapokuwa imekosewa kabisa basi huitwa Kidhb (uongo) au Iftira’ (tuhuma). Yaani utaratibu uliotumiwa wa kuwanasibisha Ma’sumiin a.s. haupo wenye ukweli, bali tunaweza kusema kuwa ni tuhuma. Hadith hizo ni uzushi mtupu.

Swahili