Mke Kukaa Eda Ya Kufiwa Na Mumewe

Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Swahili

Thawabu Ya Kwenda Kuzuru Makaburi Ya Ndugu Zetu Mumineen (Wenye Imani)

Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliwaambia Masahaba: "Watuzeni maiti wenu?

Swahili

Ruhusa Ya Kulia Ufiwapo

Ni sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) kumlilia maiti wako.

Mtukufu Mtume (s.a.w,) alimlilia Bwana ZAIDI (R.A.) na Bwana JA'AFAR (R.A.) na pia alimlilia Ami yake Sayidna HAMZA (a.s.) na mwanawe Sayidna lbrahimu (a.s.) Mtume (s.a.w.) alipomwona ami yake Hamza (a.s.) ameuwawa akalia, na alipoona namna Ilivyotendewa kinyama maiti tukufu ya Hamza (a.s.) akalia sana kwa kwikwi.

Swahili

Shukrani

Kitabu hiki kiliandikwa kwa lugha ya Kiajemi na Jumuiya ya "Dar-Rahe-Haq" ya mjini Qum (Iran).

Kilitafsiriwa kwa Iugha ya Kiingereza na kutiwa nyongeza fulani fulani na Haji Ahmad Hussein Sheriff na kutangaziwa na Jumuiya “A Group of Muslim Brothers", S.L.P . 2245, Tehran, Iran (ambayo siku hizi huitwa "World Organization for Islamic Services (WOFIS).*

* Tafsiri hiyo ya Kiingereza iliitwa "Philosophy of the Marriages of the Holy Prophet Muhammad (s).

Swahili

Utangulizi

Bismillahir-Rahmaanir-Rahim

Mwanzoni mwa karne ya kumi na nane waandishi wa Kikristo waligundua mbinu mpya za kuushambulia Uislamu. Nia yao ilikuwa ni kuyaeneza maandishi yasiyo na ukweli ili kupotosha watu kutoka katika lengo na msingi madhubuti wa Kiislamu na kuitweza heshima ya Mtume wetu Muhammad (s).

Swahili

Uamuzi Wa Historia

Wanahistoria waadilifu wa Kiislamu na Wakikristo wote kwa pamoja wanakubaliana kuwa ndoa alizozifunga Mtume wa Islamu (s) hazikusababishwa na tamaa ya kuitosheleza ashiki yake. Kama ingekuwa hivyo, basi asingemuoa mwanamke aliyekuwa mjane mara mbili, aitwae Khadija, mwenye umri ya miaka 40 na yeye Mtume wa Islamu (s) akiwa kijana wa umri wa miaka 25 tu, umri ambao mtu huwa katika kiwango kamili cha ashiki.

Swahili

Wapinzani Wanyamaza

Hebu tuyaangalie maisha ya Mtume wa Islamu (s). Tunaona kuwa katika umri wa ujana wake aliridhika kuwa na mke mmoja aliyekwisha kuwa mjane mara mbili na mwenye umri mkubwa na wala (Mtume (s)) hafikirii mwanamke mwingine. Kisha tunaona kuwa, katika miaka 10 ya mwisho ya maisha yake, akiwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akiwa katika uzee wake na akiwa amezungukwa na matatizo magumu sana ya dola mpya ya Kiislamu, alianza kuoa wake wengi.

Hebu waulize waandishi hawa wa Kikristo, "kwa nini itukie hivi?"

Swahili

Orodha Ya Majina Ya Wakeze Mtume (S)

Baada ya kifo cha mke wake wa kwanza Bibi Khadija (a), Mtume (s) alioa wanawake wafuatayo:

(1) Saudah, (2) Ayesha, (3) Ummus-Salamah bint Khuzaimah, (4) Hafsah (5) Zainabu Binti Jahash, (6) Ummu-Habibah (Ramla), (7) Maymunah, (8) Zainab bint Umais, (9) Juwairiyah, (10) Safiyyah na (11) Khaulah binti Hakim.

Hebu tuyachunguze matukio na hali zilizosababisha ndoa hizi kufungwa. Ukweli ni kuwa, tunaweza kusema kuwa ndoa hizi zilifungwa kwa moja au zaidi ya sababu hizi zifuatazo:

Swahili

Maneno Mawili

Bismillahir Rahmanir Rahiim
Natanguliza kumshukuru Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Maimamu a.s. walionijaalia Tawfiqi ya kuweza kuwaleteeni mbele yenu kitabu hiki.

Mimi nimekitarjumu kitabu Dhambi Kuu la kutokulipa Zaka, Khums na Sadaka katika Kiswahili na wakati nikiwa nikiifanya kazi hiyo, niliona itakuwa afadhali iwapo Sadaka pia nitakitayarishia kitabu chake. Na hivyo ndivyo kitabu hiki kipo mikononi mwenu.

Swahili

Tujielimishe Kuhusu Ilimu Na Mengineyo

Swahili