read

Kuhusu Mwanamke

Hao… wanataka kutokomeza familia…

Familia inapokuwa imejengeka kwa misingi ili­yowekwa na Uislamu, basi inakuwa imara na yenye mshikamano na hivyo ni muhali kuisambaratisha. Na familia inaposhikana kiasi hiki watoto hukua katika mazingira ya kidini wakiwa na pambo tukufu; na hii inafanya jamii kuwa ni yenye kuhifadhika na upotofu kusambaratika na kufanywa watumwa, na sote tuna­jua kwamba kusambaratika ndiyo kipimo cha nguvu ya ukoloni. Free Mason, ili kufikia hilo wanasema:

“Ili kuleta mtafaruku baina ya mtu na ukoo wake, itawabidi muziondoe tabia nzuri zao tangu shinani, kwani kwa hio nafsi zinaelekea kwenye kuvunja udugu na kuingia kwenye mambo yaliyoharamishwa, na kwa sababu watu hao wanapenda sana domo kaya kwenye mikahawa na kuwacha kusimamia familia zao; watu kama hao ni rahisi sana kuwarubuni kwa kuwapa nyadhifa na mishahara kutoka kwa Free Mason kisha waonyeshwe ugumu wa maisha ya kila siku (ndipo mtawapata). Na pia watengeni watu wa aina hiyo na watoto wao na wake zao na muwatupe kwenye anasa za maisha ya kinyama. 1

Wazayuni nao (kwa lengo hilo hilo) wanasema: “Lengo hupatikana kwa mbinu, kwa hivyo inatupasa tuangalie wakati tunapofanya njama zetu, tusi­wafuate wale watu wema wenye tabia nzuri watu wengi wamepotezwa na pombe na vijana kuwa ma­chizi. Hii ndiyo mbinu iliyotumiwa na maajenti wetu, waalimu na watumishi, vilevile wafunge kwenye nyumba za kitajiri, waandishi wetu, na hata wanawake wetu kwenye majumba yao ya starehe. 2

Hata wana wa Nazi nao walikuwa na mwito wao; “sababisha chuki ndani ya ukoo ili uusambaratishe.”

Kwa hivyo, utaona kwamba nadharia zote za kikoloni mwito wake ni ‘kuuteketeza ukoo na majivu yake kuyatupa baharini.”

Nchini Marekani, Wazayuni wanahimiza kile kinachoitwa ‘ndoa ya pamoja.’ Yaani wakusanyike wanaume watano na wanawake watano, kisha waozwe wote pamoja kwa ‘tamko’ moja tu la ndoa, halafu inakuwa mwanamke mmoja ana waume watano, na mwanamume mmoja ana wake watano.

Ulaya ya mashariki nako (kwa walahidi)3 wanadai kuondoa sheria zilizowekwa na dini kuhusu ndoa na kuchukua mfumo wa ‘ndoa ya pamoja’ uliopende­kezwa Uingereza. Na nadharia hizi hivi sasa zinae­nezwa kwetu; je! kwa kiasi gani tutaweza kuzipinga?

Jibu: Uthabiti wetu na upingaji wa nguvu dhidi ya nadharia hizi za kikoloni ni lazima ushikamane na dini na desturi zake.

Mwanamke huchinjwa vipi?
Huku akiwa amefanikiwa na shuka nzito yenye nembo za kijani na weupe, wamemchukua mwanamke, na kumpeleka kichinjioni ili asihisi maumivu ya kifo. Wametumia neno ‘uhuru’ wakampokonya mwanamke uhuru wake, na mwili wake wakaufanya bidhaa yenye kuvutia kwenye mashirika ya biashara ya ngono! Ndiyo ni kweli kwamba hawakumtungika msalabani, lakini wamemfungia njia ili afuate mwe­nyewe kwenye biashara ya utumwa na ajiuze mwe­nyewe kwa wateja.

Wametumia neno ‘penzi lisilo la kuingiliana’ wa­kamsukuma msichana mdogo kwenye makao ya haramu na kumfanya achukue tembe za kuzuia mimba ndani ya madaftari ya hesabu anapoingia chuo kikuu kusoma.

Wametumia neno ‘kufanya kazi’ wakawapeleka wake za watu kwenye mikono ya wanaume baki vichochoroni bure!

Na wametumia neno ‘mchanganyiko wa ki-heshima’ kwa kuunda kizazi la anasa, kisicho na mwenendo wala afya nzuri, na mamilioni ya wanaharamu kwa mwaka mmoja tu!

Lau ningeliambiwa nichague jina la enzi hizi zetu ningechagua ‘Enzi za upotofu na uchizi uliosindikwa ndani ya maneno matamu.”

Hebu angelieni huku na huko, hivi kweli kuna fikra iliyobaki bila ya kusindikwa (kutiwa) ndani ya maneno matamu?

Zamani neno ‘zinaa’ liliwaogofya wasichana kama makali ya kisu; wakalibadilisha neno hilo kwa neno ‘uhuru wa mapenzi’ ili asiogope!

Neno ‘msago’, wakalibadilisha kwa ‘penzi la penzi’ ili liwe tamu na lipendwalo!

Neno ‘mwanaharamu’ lilikuwa lina aibu kwenye jamii, hivi sasa limekuwa ‘mtoto wa kimaumbile’ ili asionewe haya na mtu yeyote!

Basi, kama yalivyobadilika maneno, na mtazamo wa jamii pia umebadilika. Mwanzo mtazamo wa jamii ulikuwa mzuri, wenye mshikamano kisha ukawa umepotea, umezama kwenye taabu na masumbufu.

Zamani msingi wa jamii ulisimamia kwenye imani na mapenzi na siku hizi kwenye utengano, uchu na uhalifu. Hivi ndivyo mwanadamu walivyomuuwa kwa mwanadamu.

Ee chonde wanaadamu!

Safari ya ki-chizi inaelekea wapi?

Safari hiyo inayoanzia kwenye Mini inaishia wapi?

Jambo hili si gumu kama hesabu, tujumlishe, tutoe au tugawanye ndipo tupate majibu; la, majibu ni hali halisi kama tunavyoiona hivi sasa kwenye jamii ya kisasa inayoishi kwenye enzi hizi za upotofu wa kijinsiya na ufuska.

Kwa mtazamo wa haraka haraka tunapoangalia ndani ya jamii za kisasa tutagundua mambo yenye kuogofya yafuatayo:

Safari yenyewe hawa-anzii kwenye Mini kama inavyodaiwa, bali inaanza pale mwanamke anapo­anza kujionyesha nywele na sehemu zingine.

Kisha safari hiyo huendelea mpaka kufikia kwenye Mini ambayo itaonyesha miguu.

Kisha inaendelea mpaka kufikia kwenye Micro, ambayo iko senti mita ishirini na nne juu ya magoti.

Haishii hapo, kisha inaingia kwenye ‘stesheni’ ya Short (bukta) karibu na kwenda uchi.

Kutoka hapo inasimama kwenye ufuo wa bahari kwa kustarehe kijinsiya kufanya mapenzi na kuoga maji ya moto (k.v. Sauna n.k.)

Kisha inafikia kwenye vilabu vya watembea uchi (Neudists) kama walivyozaliwa.

Kisha wiki nzima kwenye vilabu vya ngono zisizo za kawaida na kwenye maandamano ya mashoga na wanawake wanaopenda jinsiya na wake wenzao wakidai haki zao za kufanya mapuuzi kwa uhuru!

Kutoka hapo anafikia kwenye kujianika uchi na wenda-uchi wenzake kwa muda mrefu mabara­barani, viwanjani na hata kwenye mabwawa ya kuogelea.

Kuishi hatua za mwisho mwisho ni uvutaji wa bangi, hashish na ‘unga’ (heroin).

Mwisho wa safari ni kuharibika akili, wazimu na kujiua kwa pamoja.

Safari hii mbaya haichukui muda mrefu kufika, lakini kwa kweli inachukuwa maisha ya watu wengi mno katika jamii. Isitoshe ni safari moja lakini yenye vituo kumi ambavyo mtu lazima avipitie vyote kimoja baada ya kingine bila ya kuviacha vingine kwa sababu ‘orodha’ yake ni moja tu haiepukiki.

Wasomi wa elimu ya maadili wanasema: “Ngono ina­pelekea mtu kufanya nyingine, tendo la haramu ni su­maku ya kuvutia lingine la haramu, na kuvama kwenye maasiya kuna sababisha kuvama zaidi kwenye maasiya.” Na kama wasomi hao hamuwaamini, macho yenu je?

Hebu njooni, kisha tuinue shingo zetu kidogo tuiangalie jamii hii ya kisasa ‘ya viwanda’ ambayo inatukuza mitambo tu bila ya kujali gharama ya utu wa binadamu ambao umezidi kuzorota siku baada ya siku mbele ya moshi wa viwanda. Hebu njooni tuangalie takwimu zinavyoonyesha.

Nchini Ufaransa kuingiliana ngono, kinyume na maumbile kunafanywa bila ya kuona haya. Wana­sema wake nchini humo “Baada ya yote hayo, tuna wanaume wengi wa nje tunaowazalia watoto.”4 Nchini humo, mtu haoni vibaya kujichua, kufanya ulawiti, kuingiliana na wanyama na midomoni amba­ko huko ndiko kunapendezwa. Na huko Marekani, nako, mwanamke kwenda uchi ndiyo maendeleo na kunakubalika na kupigwa picha za jinsiya sehemu moja moja imekuwa pia ndio maendeleo.

Katika ripoti ya kila mwaka, imeelezwa kwenye mwaka 1965 ya manispaa ya mji wa San Fransisco, jimbo la Carlifornia kuzidi kwa makosa ya kijinsiya na kwamba, matoleo ya picha chafu za kijinsiya na watumishi wa nyumbani na wahudumu wa mahoteli walio vifua na mapaja wazi wanapohudumu wamezidi mno. Vilevile pana wasichana wanaojionyesha miili yao uchi, mihadarati, na ulawiti kwa wanaume wamefikilia nusu milioni mwaka huu.”5

Safari hiyo ya wendawazimu inaendelea nchini Marekani, hebu angalia:

“Maofisa wa polisi walivamia ghafla jumba moja jipya liliopo mjini Atlanta, Georgia wakafanya msako, na wakapata mafaili ambayo inakisiwa kuwa ni ya kilabu cha kubadilishana wake! Msemaji wa polisi alinukuliwa akisema kwamba: “Kuna jarida linalotolewa na kilabu hicho lisemalo kwamba mlango wa kilabu u wazi kwa makapera na walioowa, wake kwa waume, na kwamba kilabu hicho kina matawi yake mjini New York, Chicago, Dallas, Orlando na Florida.”

Polisi mwingine naye anasema: “Kitendo cha ku­badilishana wake kinazidi kuongezeka siku baada ya siku katika kilabu hicho.”

Huko Sovieti safari hiyo potofu inaishia kwenye talaka, kwenye gazeti litokalo nchini humo la Pravda kuna makala maalum iliyoandikwa na mtaalamu wa mambo ya jamii Dkt Kharshev isemayo: “Katika kila watu kumi, watu tisa huwachana kwenye nchi za umoja wa kisovieti na sababu kubwa ni kuharibika kwa tabia na ulevi wa kupita kiasi. Na asilimia themanini ya uhalifu unaotendwa na vijana wadogo unatokana na kusambaratika kwa familia, vilevile wengi wanaoana hawaishi pamoja zaidi ya miaka mitatu au hata baadhi yao kwa miezi au wiki chache tu.”6

Nchini Uingereza, ripota moja wakike wa jarida moja la kiarabu, ameeleza kwamba siku moja alikwenda nchini humo na kupokewa uwanja wa ndege na rafiki yake wa siku nyingi: alipomuona tu kitu cha kwanza alichokigundua kwa rafiki yake huyo ni kubadilika kwa sura yake ambayo mwanzoni ilikuwa nzuri na kuonekana mzee! Akataka kujua sababu iliyomfanya azeeke mapema hivyo akiwa na umri wa miaka ishirini na mitano tu; alimjibu: “Ah, kwa sababu ya matatizo mengi ya kisaikolojia.” Akamuuliza: “kulikoni, mumeo kakuwacha na kuchukua mrembo mwingine nini?” Akajibu! “Ndio kaniacha, lakini siyo kwa ajili kapata mrembo mwingine, la bali mwanamume kama yeye! Yule mwandishi alishangaa mno: “Nini? Mwanamume kama yeye?” Akajibu: “Ndiyo, ame­kuwa mlawiti.”

Mwandishi huyo anaongeza: “Wimbi linaloikumba jamii ya Uingereza ni hilo la mapenzi ya waume kwa waume, na utaweza kufahamu hilo kwa kuangalia matangazo yake kwenye majarida. Ikiwa zamani mwanamume alikuwa akitaja sifa anazotakiwa awe nazo mwanamke anayetaka kumuoa, ama hivi leo atatoa sifa za mvulana anayetaka kumuoa! Zamani msichana anapotafuta mchumba hujitaja sifa zake gazetini, mathalan, msichana, umri miaka kumi na nane rangi ya nywele: kahawia, elimu: chuo kikuu: angependa kuolewa na mume aliye chini ya miaka thelathini n.k leo hii mvulana ndiye anayejitangaza, mathalan, umri miaka ishirini rangi ya nywele; nyeusi, rangi ya macho; kijani. Elimu: mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu, angelipenda ‘kuolewa’ na mume asiyezidi miaka hamsini… n.k.!

Je, si nilikwambia safari ya upotofu ni moja tu, mtu hawezi kufuata njia moja akaacha nyingine!

  • 1. Sehemu ya hotuba iliyotolewa na mwanachama mashuhuri wa Free Mason Bw. Beckrator, mnamo 1921.
  • 2. Yamenukuliwa kutoka kwenye Protocal 1 za Wazayun (Wayahudi).
  • 3. Walahidi: Watu wasioamini Mungu.
  • 4. Dr. Melene Michele – Wolfromm. Cetle chose - La.
  • 5. Gazeti la Herald Tribure. Toleo la Ulaya, 10 Mach 1996.
  • 6. Gazeti la Al-Ihram la Misri 26 April 1966 lilinuko kutoka gazeti la Pravda la Sovieti la tarehe 25 April 1966.