read

Kuiga: Maafa ya Ulaya Mashariki

Watu wa Ulaya mashariki walipojitenga na dini tu, hadhi yao ikaporomoka wakawa ni wenye kuiga tu. Wengine nao walipofika mwezini, vijana wetu nao wakavutiwa sana na hilo wakasoma magazeti yao ili wapate ramani iliyowafikisha huko mwezini lakini hawakuipata, ila tu waliambulia bimbiriza – mavi, habari za vijana wa Pop Music na fikra ya uhuru, wao wakadhani mambo haya ndiyo ramani ya kufika mwezini. Wakaacha kila kitu. Wakavaa mavazi ya kike! Jee! hii si aibu?

Hapana, maadam Waamerika wanafanya basi si aibu, si wao wamefika mwezini? Hayo ndiyo maneno yao.

Wengine wamefika kwenye safari ya Mars, vijana wetu pia wakavutiwa na hilo, wakasoma magazeti yao, wakapewa, wakipata “Sandwichi za kisaikolojia” zenye alama nyekundu na manjano wakadhani kula sandwich hizo ishirini kunatosha kumpeleka mtu kwenye Mars, wakamiminika madukani kuzinunua kwa fujo, mwishowe walicheza shere dini na maadili mema.

Walisikiliza idhaa zao wakasikia kwamba “kwa hakika hakuna misingi thabiti au ukweli unaopelekea kuwa na tabia njema, bali tabia zenyewe zinabadilika kutokana na jinsi hali za kijamii zinavyogeuka chini ya athari za kiuchumi, na kwamba fikra za binaa­damu ni chombo kinachofuata maada tu (dunia) na vivyo hivyo mfumo wa kitabia ni chombo kingine cha ki-maada tu.”

Vijana wetu wakashikamana na fikra hizo kama wahyi ulioshuka, wakawa wanaishi na familia na jamii zao kwa kutumia falsafa hiyo mbovu, wakaa­nguka kwenye mlizamu (mfereji wa maji ya mvua) badala ya kutua mwezini na kwenye Mars. Ikawa kisa chao hiki kinafanana na kisa cha bwana mmoja aliyepata madaraka makubwa katika jamii, wenzake wakataka kujua sababu hasa iliyomfanya apate madaraka hayo, baada ya kipindi kidogo cha uchunguzi wao, mmoja wao akadai kwamba ame­gundua sababu, akawaambia wenzake, “nimegu­ndua sababu iliyomfanya mwenzetu awe na mada­raka ni kuwa kila anapoketi mahali huchezesha ki­dole chake gumba cha mguu kwa vidole vyake vya mkono na kulia! wenzake hao wakaingilia kujichezeachezea vidole vyote vya miguu, wakiwa na ndoto ya kubeba wadhifa mkubwa kama mwenzao!”