Aya 20 – 23: Wanaoomba Asiyekuwa Mwenyezi Mungu
Maana
Na wale wanaowaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa.
Yametangulia mazungumzo kuhsu ushirikina na mjadala pamoja na washirikina, katika Aya kadhaa. Sasa baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuelezea aina kadhaa za neema zake kwa waja wake, anadokeza, kwenye Aya hizi na zinaazofuatia, kuhusu wale wanaomkufuru Mwenyezi Mungu na wanaomfanyia washirika katika kuumba kwake.
Akawaambia wazi na kwa hoja fasaha, kwamba Mungu anayefaa kuabudiwa ni yule anayekuwa muumbaji sio aliyeumbwa. Na nyinyi washirikina mnaabudu aliyeumbwa sio aliyeumba.
Ni wafu si hai.
Vile vile miongoni mwa masharti ya mwenye kuabudiwa ni kuwa hai; na mnayemwabudu ameganda tu hana uhai.
Na wala hawatambui watafufuliwa lini.
Jumla hii maana yake yatafahamika kutokana na maswali mawili yafutayo pamoja na majibu yake:
Swali la kwanza: Neno hawatambui linatumika kwa wenye akili na washirikina wanaabudu masanamu, sasa imekuwaje kutumia dhamiri ya wenye akili kwa visivyo na akili?
Jibu: matumizi haya yamekuja kulingana na wanavyoitakidi washirikina kwamba masanamu yanaakili na utambuzi. Kwani kuna ubaya gani wa matumizi haya na mfano wake maadamu ni masuala ya tamko tumko tu na ibara?
Swali a pili: Masanamu hayatafufuliwa, vipi Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akasema: ‘Na wala hawatambui watafufuliwa lini’
Jibu: baadhi ya wafasiri wamejibu kwamba dhamir katika ‘hawatambui’ ni ya masanamu na ‘watafuliwa’ ni ya washirikina. Kwa hiyo maana yanakuwa masanamu hayatambui lini watafufuliwa washirikina kutoka makubirini mwao. Ikiwa masanamu hayatambui hayo, basi inakuwaje kuwa yanastahiki kuabudiwa?
Mungu wenu ni Mungu mmoja. Lakini wasioamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wana kiburi.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.), katika Aya hii, ametaja sifa mbili za wanaopinga Akhera:
Sifa ya kwanza: kwamba nyoyo zao zimepinga na kuikana Akhera. Kwa hiyo wao hawafanyi chochote kwa kutummai thawabu au kuhofia adhabu; isipokuwa wanafanya kwa misingi ya faida na manufaa ya maisha haya ya dunia. Sifa ya pili: kwamba wao wanaikimbia haki na wala hawaifuati kwa sababu ya kujiona wakubwa na kuwa na kiburi.
Hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyafanya siri na wanyoyatangaza. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi.
Hakika Yeye Mwenyezi Mungu anajua kupinga kwao kulikuwa ni kwa kujipa uluwa na kiburi, naye anawachukia wanaoinyenyekea haki na atawaadhibu yale wanayostahiki.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ مَاذَا أَنْزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ {24}
لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُمْ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ {25}
قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّهُ بُنْيَانَهُمْ مِنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِنْ فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ {26}
ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنْتُمْ تُشَاقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ {27}
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنْفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِنْ سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {28}
فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ {29}
Basi ingieni milango ya Jahannam, humo mdumu. Ni maovu mno makazi ya wafanyao kiburi.