Aya 65 – 69: Mwenyezi Mungu Ametermsha Maji Kutoka Mbinguni
Nahaw (Sarufi)
Katika Juz. 7 (6: 134) Mwenyezi Mungu amerudisha dhamir ya wanyama kwa muannath ( ya kike) na hapa ameirudisha kwa dhamir ya mudhakkar (ya kiume). Wamejibu kwamba dhamir hapa inarudia kwenye baadhi; yaani baadhi ya wanyama ambao ni wakike, na kule inarudia kwa wanyama wote.
Maana
Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaosikia kwa kuzingatio na kutilia manani maji na faida zake.
Aya hii na inayofuatia ni katika Aya za mambo ya ulimwengu ambazo Qur’an inazikariri kwa lengo la kuleta uzinduzi kwenye dalili za Tawhid na ufufuo. Aya hii imekwishapita katika Juz.1 (2:22, 164), Juz. 7: (6:99), Juz. 13 (13: 17), (14: 32) na sura hii tunayoifasiri Aya ya 6.
Na katika wanyama mna mazingatio. Tunawanywesha katika vile vilivyomo matumboni mwao, vikatoka, baina ya kinyesi na damu, maziwa safi, mazuri kwa wanywao.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametaja baadhi ya faida za wanyama katika Juz. 8 (6:142) aliposema: “Na katika wanyama wale wabebao na wa kutoa matandiko.”
Katika sura hii tuliyo nayo, mbele, kwenye Aya 80, amesema: “Na akawafanyia kutokana na ngozi za wanyama wenu nyumba mnazoziona nyepesi siku ya kusafiri kwenu na siku ya kutulia kwenu.
Na katika sufu zao na manyoya yao na nywele zao mnatengeneza vyombo na vifaa vya kutumia kwa muda.” Mwanzoni mwa sura hii amekusanya faida za wanyama kwa kuhusisha maziwa akasema kuwa yanatoka katika matumbo ya baadhi ya wanyama; yaani wa kike. Angalia kifungu cha Nahw.
Wataalamu wanasema kuwa wanyama wanakula mimea, baada ya kutafuna matumbo yanatoa nje kinyesi chenye madhara na kufyonza majimaji yenye manufaa ambayo yanageuka damu inayotembea kwenye mishipa. Baadhi ya damu hii inapofika kwenye viwele inageuka na kuwa maziwa safi ya kunywa.
Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza kileo na riziki nzuri. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaotumia akili
Dhahiri ya neno kileo hapa ni kinywaji chochote kinacholevya, kiwe ni pombe au kitu kingine. Lakini Aya haidokezi hukumu ya ulevi kwa umbali wala karibu; kwamba wakati huo iliposhuka ulevi ulikuwa halali au haramu; isipokuwa inaelezea desturi ya watu kwamba wao wanatengeneza kinywaji na ulevi kutokana na matunda ya mitende na mizabibu. Ama riziki nzuri makusudio yake ni tende mbichi na za kuiva, zabibu mbichi na kavu, siki, jamu n.k.
Yamekuja maelezo kutoka baadhi ya mapokezi kwamba makusudio ya kileo katika Aya, ni kilicho haramu na riziki nzuri ni kilicho halali.
Tumefafanua dalili za uharamu wa pombe katika Juz. 2 (2: 219) na pia katika kitabu Fiqhul-imam Ja’far asswadiq Mlango wa Al-at’ima wa wal Ashriba (Vyakula na vinywaji)
Na Mola wako akampa wahyi nyuki.
Makusudio ya wahyi hapa ni maumbile ya akili ambayo Mwenyezi Mungu alimpa nyuki.
Kwamba tengeneza nyumba katika milima na katika miti na katika wanaoyajenga.
Yaani wanayoyajenga watu.
Razi anasema: “Kuna aina mbili za nyuki: Ile inayokaa milimani na kwenye misitu, hawashughulikiwi na mtu yoyote. Ndio makusudio ya kusema kwake Mwenyezi Mungu: ‘Kwamba tengeneza nyumba katika milima na katika miti’ na aina nyingine inakaa katika majumba ya watu na wanashughulikiwa na watu. Ndio makusudio ya kauli yake: ‘katika wanaoyajenga’.
Kisha kula katika kila matunda maua na mimea unayoipenda. Na ufuate njia za Mola wako zilizo dhalili. Yaani ni dhalili kwa kwa ajili yako wewe nyuki ili upate wepesi wa kupita
Na katika matumbo yao kinatoka kinywaji amabacho ni asali wanayoitema kama mate. Chenye rangi mbali mbali nyeupe, nyekundu na yanjano, kulingana na mimea waliyokula.
Ndani yake kina matibabu kwa watu; kama vile ukosefu wa damu, kutosagika vizuri chakula tumboni, vidonda vya mdomoni, matatizo ya mapafu na kibofu cha mkojo. Pia maradhi ya figo na mengineyo waliyoyataja watabibu.
Hakika katika haya kuna ishara kwa watu wanaofikiri katika alivyoviumba Mwenyezi Mungu na maajabu yake yanayofahamisha kuweko mpangiliaji hodari Mwenye hekima.
Wataalamu wameandika mengi kuhusu mipangilio ya hali ya juu ya nyuki, nidhamu yake na jinsi wanavyosaidiana katika maisha yao, kujenga nyumba na usalama. Huko nyuma tumeashiria kwamba hatimae imegunduliwa kuwa linapozidi joto nyuki huanza kazi ya kuchukua maji kwenye visiku vyao.
Wengine wanayanyunyiza ndani ya masega na wengine wanatingisha mbawa zao ili wafanye tiyara ya hewa. Kwa hiyo maji yananyunyizika kwa haraka jambo ambalo linafanya joto lipungue.
Mfano huu pekee unatosheleza yote yaliyoandikwa kuhusiana na mpangilio wa nyuki.
وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنْكُمْ مَنْ يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ {70}
وَاللَّهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ ۚ فَمَا الَّذِينَ فُضِّلُوا بِرَادِّي رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَاءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ اللَّهِ يَجْحَدُونَ {71}
وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُمْ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللَّهِ هُمْ يَكْفُرُونَ {72}
وَيَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ شَيْئًا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ {73}
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ {74}