Aya 84 -89: Tutapomwinua Shahidi
Siku tutakapomwinua shahidi kwa kila umma, kisha hawataruhusiwa wale ambao wamekufuru wala hawatachiliwa kutaka radhi
Haya ni makemeo na kiaga kwa wale aliowaashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya iliyotangulia kwa kusema kwake: “Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu kisha wanazikanusha”
Njia ya makemeo hayo ni kuwa Mwenyezi Mungu atawakusanya watu kesho na atamleta kila mtume ashuhudie au awe shahidi wa umma wake. Atakpotoa ushahidi Mwenyezi Mungu ataichukua kauli yake na wala hawataruhusiwa kuipinga kauli hiyo na kutoa udhuru. Mwenyezi Mungu anasema:
هَٰذَا يَوْمُ لَا يَنْطِقُونَ {35}
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ {36}
Makusudio ya kutoachiliwa kutaka radhi ni kuwa hawatatakiwa kuomba msamaha kwa kauli wala vitendo. Kwa sababu Akhera ni nyumba ya hisabu na malipo, sio nyumba ya matendo na kuomba msamaha.
Na wale ambao wamedhulumu watakapoiona adhabu hawatapun- guziwa wala hawatangojewa.
Makusudio ya wale ambao wameadhulumu ni kila dhalimu; ni sawa awe amemdhulumu Muumba wake kwa kumkanusha au amemdhulumu mwingine kwa kumfanyia ubaya; au awe amejidhulumu yeye mwenyewe kwa kujiingiza kwenye majanga. Yeye ataadhibiwa tu kwa sababu ya dhul- ma. Atapata malipo yanayolingana na kosa, hatapunguziwa wala kuzidishiwa tena bila ya kuchelewa.
Na wale ambao wameshirikisha watakapowaona wale ambao wamewashirikisha watasema: Mola wetu! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako. Ndipo wale watakapowatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo.
Watakaotupa kauli ni wale walioshirikishwa, wakiwatupia washirikina. Dhahiri ya Aya inaonyesha kuwa Mwenyezi Mungu atawafufua wale waliokuwa wakiabudiwa, wawe ni masanamu au kitu kingine, ili awape hoja wale waliokuwa wakiwafanya wengine kuwa ni waungu. Na kwamba washirikina watakapowaona hao waungu wao waliokuwa wakiwaabudu, watamwambia Mwenyezi Mungu: hawa ndio tuliokuwa tukiwashirikisha nawe. Na hao waungu wajibu kwa maneno au kwa kihali kuwa, nyinyi washirikina ni waongo na wazushi kwa kutufanya sisi ni washirika wa Mwenyezi Mungu.
Sio mbali kuwa masimulizi haya ya kauli ya washirikina ni fumbo la kufichuka uhakika kesho na kwamba hakutakuwa na nafasi ya uwongo wala kudanganya.
Na siku hiyo watasalimu amri mbele ya Mwenyezi Mungu.
Yaani washirikina na waungu wao watasalimu amri na kunyenyekea amri ya Mwenyezi Mungu na yatapotea waliyokuwa wakiyazua. Kila mzushi katika maisha haya utamrudia uzushi wake kwa hizaya na adhabu siku hiyo ngumu.
Wale ambao wamekufuru na kuzuilia watu njia ya Mwenyezi Mungu tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa walivyokuwa wafisadi.
Walifanya ufisadi kwa kukufuru kwao haki na wakafanya ufisadi kwa kuizuilia haki kwa hiyo wanastahiki adhabu mara mbili. Moja kwa ajili ya ufisadi na nyingine kwa ajili ya kufisidisha:
وَمَا هُمْ بِحَامِلِينَ مِنْ خَطَايَاهُمْ مِنْ شَيْءٍ ۖ {12}
Na siku tutakapomwinua katika kila umma akiwashudia kutokana na wao.
Yametangulia maana ya Aya hii katika Aya 84 ya sura hii. Hapa imerudia kuwakema wale waliomkadhibisha Muhammad (s.a.w.).
Na tukakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa.
Neno ‘wewe’ hapa ni Muhammad (s.a.w.) na ‘hawa’ ni umma wake. Unaweza kuuliza kwamba Muhammad (s.a.w.) ni Mtume wa Mwenyezi
Mungu kwa watu wote kwa nukuu ya Aya hii:
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ {28}
Kwa hiyo ikiwa risala ya Muhammad ni kwa watu wote, inatakikana ushahidi wake pia uwe kwa watu wote huko akhera, lakini kama ikiwa ushahidi wake huko akhera ni kwa umma wake tu, basi itabidi risala yake hapa duniani iwe kwa umma wake tu?
Jibu: hakuna uhusiano wa ushahidi wake kwa umma wote huko akhera na kuenea risala yake hapa duniani. Kwa sababu risala ya Uislamu inafikishwa na umma wa Muhammad (s.a.w.) baada yake kwa umma zote wakati wote na mahali pote. Mtume anatoa ushahidi juu ya umma wake kwamba hawakufikisha risala kwa vizazi vingne.
Na tumekuteremshia Kitabu hiki kubainisha kila kitu.
Maneno anaambiwa Muhammad. Makusudio ya kitabu hiki ni Qur’an, ndani yake mna ubainifu wa kila kitu unaoamabatana na itikadi, sharia, maadili, mazingatio na mawaidha. na uongofu kwa anayeutaka na bishara kwa Waislamu.
Makusudio ya bishara hapa ni Pepo na Mwislamu ni kila mwenye kusalimu amri ya haki na akaitumia.
إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ {90}
وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّهِ إِذَا عَاهَدْتُمْ وَلَا تَنْقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللَّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ {91}
وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِنْ بَعْدِ قُوَّةٍ أَنْكَاثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَنْ تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللَّهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنْتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ {92}
وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَٰكِنْ يُضِلُّ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۚ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ {93}