read

Sura Ya Kumi na Sita: An Nahl

Sura Annahl (Nyuki) Ina Aya 128

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

أَتَىٰ أَمْرُ اللَّهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ {1}

Imefika amri ya Mwenyezi Mungu msiifanyie haraka. Ametakata na kutukuka kuliko vile wanavyovishirkisha.

يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ أَنْ أَنْذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ {2}

Huwateremsha Malaika na roho kwa amri yake juu ya anayemtaka katika waja wake; kwamba onyeni kuwa hakuna Mola aabudiwaye isipokuwa mimi tu, basi niogopeni.

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ تَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ {3}

Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, ametukuka kuliko vile wanavyovishirkisha.

خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُبِينٌ {4}

Amemuumba mtu kwa tone la manii, mara amekuwa hasimu aliye dhahiri.