Aya 26 – 31: Mtu Kutokana Na Udongo
Na hakika tulimuumba mtu kutokana na udongo mkavu kwa matope meusi yenye kufinyangwa.
Watu wamezungumza mengi sana kuhusu asili ya mtu. Darwin amesema kuwa asili ya mtu ni nyani. Tumefafanua kuhusu dhana ya Darwin na asili ya mtu katika Juz. 8. (7: 11). Hapa tunayarudia maudhui hayo kwa mfumo mwingine:
Maarifa ya kujua mambo yanakuwa tu katika hali zifuatazo:- Majaribio, kushuhudia, akili na wahyi. Ni wazi kwamba, kutokana na utafiti, tunaweza kumjua mtu alivyo. Ama kujua alipatikana vipi na alikuwa katika hali gani, swali hili haliwezi kujibiwa na majaribio.
Tukija kwenye kushuhudia, hakuna mtu aliyeshuhudia uumbwaji wa mtu, wala hakuna kitu, katika vinavyofukuliwa, kinachofahamisha asili ya mtu. Hilo tumelifafanua katika Juz. 8: (7:11–18). Ama tukiuliza akili kuhusu asili ya mtu, ni sawa na kuiuliza hiyo akili, ni nani baba yake fulani, je alikuwa ni mrefu au mfupi? Kwa hiyo basi hakuna kilichobakia katika kuja asili ya kuumbwa mtu isipokuwa ni kwa wahyi tu.
Mwenye kufuatilia Aya za Qur’an yenye hekima, atakuta baadhi ya Aya zinaasema:
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ مِنَ الْمَاءِ بَشَرًا {54}
Nyingine inasema:
كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ {59}
Pia kuna ile isemayo: “Yeye ndiye aliyewaumba kwa udongo.” Juz. 7 (6:2) udongo uliokusudiwa hapa, kutokanana neno la kiarabu twin ni udongo mbichi – machanganyiko wa mchanga na maji.
Aya tuliyo nayo inasema kuwa mtu ameumbwa kutokana na udongo mkavu kwa tope nyeusi zinazoweza kufinyangwa, bila shaka hapo itakuwa ni mchanganyiko wa udongo na maji.
Kwa hiyo basi asili ya mtu ni maji na mchanga alioumbia Mwenyezi Mungu baba wa watu.
Na majini tumewaumba kwa moto wenye joto kali.
Jamaa wamekanusha kuweko majini. Baadhi ya waumini wamefasri majini waliotajwa katika Qur’an kuwa ni viini (microbe) visivyoonekana kwa macho. Wamechukulia neno Jinn kilugha, lenye maana ya kitu kililichofichikana na macho.
Wengine wakasema kuwa majini wapo. Wakatunga vitabu kuhusu idadi yao, miji yao, desturi zao, nembo zao na hata viongozi wao. Pia wakaelezea uwezekano wa jini kumuoa mtu au mtu kumuoa jini.
Sisi tunaamini kuweko majini, si kwa jingine isipokuwa tu wahyi umethibitisha hilo na inakubalika kiakili. Hatumwamini yeyote anayedai kuwa ana mawasiliano au kumuona jini. Hatukubali masimulizi yoyote yanay- ohusiana nao isipokuwa kwa kutamkwa wazi na wahyi.
Aya hii tuliyonayo imeweka wazi kuwa jini ameumbwa kutokana na moto na pia ile isemayo:
وَخَلَقَ الْجَانَّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ {15}
Kwa hiyo sisi tunaamini kuwa asili ya majini ni moto. Lakini ni aina gani ya moto na je, umbile lenyewe lilikuwaje, Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
Katika baadhi ya niliyoyasoma ni kuwa wataalamu wamegundua aina ya vidudu ambavyo haviwezi kupata uhai isipokuwa kwenye hewa ya sumu na vingine uhai wake uko kwenye visima vya mafuta na kwenye mwako.
Kwa hiyo kuna uwezekano kuwa kwenye sayari ya Jua kuna viumbe hai vinavyoafikiana na joto la Jua; kama samaki anavyoishi kwenye maji na kipepeo anavyopata rangi ya waridi na kobe kuwa na rangi ya jangwani.
Na Mola wako alipowaambia Malaika: “Hakika mimi nitamuumba mtu kutokana udongo mkavu kwa matope meusi yenye kufinyangwa.”
Mwenyezi Mungu aliwaambia hivi Malaika, lakini Malaika nao wakamawambia Mungu:
“Je utaweka humo watakaofanya ufisadi humo na kumwaga damu? Juz.1 (2:30).
Tumeeleza huko kuhusu Malaika kujibizana na Mungu na kwamba aliwa- pa nafasi ya maswali na majibizano yaliyofanana na kupinga; kisha akawafahamisha uhakika kwa njia ya upole. Pengine anaweza kupata funzo yule anayejiona ni zaidi ya wote.
Basi nitakapomkamilisha na nikamapulizia roho yangu.
Yaani nitakapompa uhai. Angalia Juz. 6 (4: 171 – 173), huko tumefafanua zaidi kuhusu neno roho
Basi muangukieni kumsujudia. Wakasujudu Malaika wote pamoja isipokuwa Ibilisi alikataa kuwa pamoja na waliosujudu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:34).
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ {32}
قَالَ لَمْ أَكُنْ لِأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُونٍ {33}
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ {34}
وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ {35}
قَالَ رَبِّ فَأَنْظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ {36}
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ {37}
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ {38}
قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ {39}
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ {40}
قَالَ هَٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ {41}
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ {42}
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ {43}
لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِكُلِّ بَابٍ مِنْهُمْ جُزْءٌ مَقْسُومٌ {44}