37. Namna Amali Njema ya ‘Kusaidia’ Inaweza Kuharibika

Si vyema kumsema mtu baada ya kumsaidia au kumsema yule uliyempa sadaka.

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:

“Allah swt amechukia na hafurahishwi na sifa sita na vile vile mimi sizifurahii hizo sifa sita na ndio nimefanya usia kwa mawasii na wafuasi waumini wote kuwa vitu hivyo sita wajiepushe navyo na mojawapo ni kule baada ya kutoa sadaka mtu akaanza kumsema yule aliyepokea (hiyo sadaka).

Swahili

38. Si Haki Kuwa Mwenye Shida Asipoomba Basi Asisaidiwe

Mtu anapotoa kitu kusaidia basi hairuhusiwi kumwambia kuwa umetoa zaidi kupita kiasi.

Swahili

39. Ni Sunna Kusaidia Kisiri

Kumsaidia mtu kabla hajaomba na kumsaidia katika hali ya kutokujulikana ni nani anayesaidia ni sunnah.

Swahili

40. Ni Sunnah Kuendeleza Moyo wa Kutoa

Ni sunnah kuendeleza na kutunza msaada na ukarimu na kuendeleaza moyo wa kutoa.

Swahili

41. Kuhurumia na Kusaidia ni Sunnah na Hukumu Zinazohusiana Nazo

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa akisema:
“Kila aina ya wema na huruma ni sadaka.”

Swahili

42. Ni Sunnah Kuwahudumia Kwanza Watu wa Nyumba Yako

Ni sunnah kuwawia wana nyumba wako kwa wema kabla ya kutoa sadaka kwa watu wa nje.

Swahili

43. Ni Karaha Kukwepa Njia Wanayopita Wenye Kuhitaji Msaada

Ni karaha kukwepa njia wanayopita maskini na ni sunnah kutokezea mbele ya waombaji na kuwasaidia kitoshelevu kwa kutoa sadaka.

Swahili

44. Ni Sunnah Kutoa Kitu Chochote Kila Siku Katika Njia ya Allah swt

Safwan anasema kuwa siku moja Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. alimwuliza mmoja wa wahudumu wake:
“Je! leo mmetoa chochote katika njia ya Allah swt ?”

Naye alijibu “hapana, leo sijatoa chochote bado.”

Kwa hayo Imam a.s. alisema:
“Sasa usipotoa hivyo unategemea Allah swt atupe baraka kwa misingi gani? Lazima utoe kwa njia ya Allah swt hata kama itakuwa ni Dirham moja.”

Swahili

45. Kuwasaidia Wale Ambao Hawajitokezi Mbele ya Watu Kuomba

Kutoa sadaka ni sunnah lakini kusaidia, kutoa msaada kwa kutegemeana na wadhifa wa mtu ni faradhi.

Swahili

46. Sadaka itolewe Kutoka Mali iliyo Halali

Sadaka kutolewa kutoka mali iliyo halali na hairuhusiwi kutoa sadaka kutoka mali iliyo haramu.

Swahili