read

40. Ni Sunnah Kuendeleza Moyo wa Kutoa

Ni sunnah kuendeleza na kutunza msaada na ukarimu na kuendeleaza moyo wa kutoa.

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Jambo jema kabisa linalonisaidia mimi katika kufanya wema katika kuwasaidia ni mkono ambao unawafikishia na mkono mwingine unashirikiana naye. Na kwa hakika hao wanaokuja kuomba wanakuja na maombi yao ndipo wanapokuwa karibu nami zaidi. Kwa hakika nimeona kuwa wale wanao sahau waliyoyatenda mema kabla na baada ya kuurudisha mkono wao nyuma huonekana kuwa wao wanaanza kuyasahau mema yote. Kwa hakika moyo wangu kamwe haukuniruhusu kuwafukuza na kuwakatalia waombaji. Na baada ya hapo Imam a.s. alisoma mashairi ifuatayo:

Wakati inapokuijia mtihani kwako kwa heshima zako pia inabidi uombe,
Basi uende kwa mtu mmoja aliye mkuu na aliye Sharifu kwa ajili ya kuomba kwake.
Kwa hakika, huyo mtu Sharifu na mkuu atakapokusaidia basi humo ndani hakutakuwa na maonyesho wala masengenyo, na badala yake ndani kutakuwa na unyenyekevu na kuhuzunika pamoja nawe.

Kumbuka wakati utakapotaka kupima katika mizani uombaji na utoaji sadaka na mema basi utaona sahani ya mizani ya uombaji utakuwa daima ni mzito kuliko nyingine yote.”

2. Warram bin Abi Faras ameandika riwaya kutoka Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:
“Wenye imani dalili zao ni nne,
kwanza nyuso zao huwa zina bashasha,

ndimi zao zinakuwa zenye ukarimu na mapenzi,

nyoyo zao zinakuwa zimejaa huruma, na

wanakuwa na mkono wenye kutoa, mkono unaopendelea kutoa sadaka na misaada nk.”