read

23. Maskini Au Mwombaji Asaidiwe Mara Ngapi?

Baada ya kumsaidia masikini mara tatu unaweza kumwambia aondoke.

1. Walid bin Sabih anasema kuwa:
“Siku moja mimi nilikuwa kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. na hapo akatokezea mwombaji mmoja. Imam a.s alimpa chochote huyo mwombaji na akatokezea mwombaji wa pili naye akapewa chochote. Hivyo hivyo akatokezea mwombaji wa nne basi Al Imam a.s akamwambia Allah atakusaidia upate zaidi njia yako atakupanulia. Na baada ya hapo Imam a.s akasema iwapo mtu atakuwa na Dirham takriban elfu thelathini au arobaini, na akanuia akawa na mpango wa kuzitumia zote ambazo kimatokeo hatabakiwa na chochote basi mtu kama huyo atawekwa miongoni mwa wale watu ambao Allah swt huzitupilia mbali dua zao.”

Kwa hayo mimi nikasema,
“Ewe mwana wa Mtume wa Allah.! Je! ni makundi gani ya watu hawa watatu?

Kwa hayo Imam a.s akajibu,
“Mmoja wao ni yule ambaye ana mapesa na mali na baada ya kutumia vyote anaomba ‘ewe Mola wangu naomba unipe riziki’. Basi hapo Allah swt anamjibu ‘Je! mimi sikukupanulia njia na kukuwekea sababu za wewe kujiwekea riziki yako?”

2. Ali ibn Hamza anasema kuwa:
”Katika kujibu swali (aliyoulizwa), mimi nilimsikia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s akisema mwalishe watatu - na kama mnataka kuwapa chochote zaidi muwape ama sivyo nyie mmeshatimiza haki ya siku yenu hiyo”.