25. Ni Sunnah Kuwaambia Waombaji Wawaombeeni Dua
Ni sunnah kuwaambia waombaji wawaombeeni dua na vile vile ni sunnah kwa mwombaji pia kuwaombea dua wanao wasaidia.
1. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amesema:
“Dua ya mtu msiidharau au kusema kuwa haifai chochote. Mara
nyingi dua muliyoombewa na Mayahudi au Manasara hukubaliwa.
Ingawaje inawezekana kwa dua aliyo jiombea yeye mwenyewe
haiwezi kukubalika.”
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Wakati mnapo wasaidia waombaji, muwaombe wawaombeeni dua hata kama dua zao wenyewe hazikubaliki kwa ajili yao wenyewe, mradi kuna uwezekano mkubwa kwa dua zao kwa ajili yenu zikakubalika.”
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakiliwa na Abu Basir riwaya moja kuwa Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
“Wakati mtu anapomsaidia fakiri mwenye shida sana asiye na uwezo, na pale fakiri huyo anapomwombea dua, basi dua hiyo lazima inakubaliwa na Allah swt.”
3. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
“Wakati mnapowapa chochote waombaji; basi muwaombe wawaombeeni dua, kwa sababu inawezekana kwa sababu ya udanganyifu na ulaghai wake dua zake zenyewe kwa ajili yake zisikubaliwe lakini kwa ajili yenu dua zake zitakubaliwa.”
4. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.:
“Alikuwa akimwambia mfanyakazi wake, zuia kwa punde kidogo sadaka, ili mwombaji amalize kuomba dua.”
5. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.
na vile vile amesema:
“Dua ya fakiri na mwombaji kamwe hairudishwi au haitupiliwi
mbali.”
6. Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.
amemwamrisha mfanyakazi wake kuwa:
“Wakati unapowapa chochote waombaji basi muwaambie wawe
wakituombea heri.”
7. Al-Imam a.s. amesema:
“Wakati mkiwapa chochote masikini na waombaji basi muwe mukiwaomba wawaombeeni dua kwa sababu wanapo waombeeni dua kwa ajili yenu, dua zao hukubalika na inawezekana dua zao kwa ajili yao wenyewe hazikubaliki.”