5. Mtoe Sadaka Kwa Mikono Yenu Wenyewe
Mtoe sadaka kwa mikono yenu wenyewe hususani wananyumba watoe sadaka kwa mikono yao na wanayempa wamwombe, awaombee dua njemaa.
1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema kuwa:
“Kwa kutoa Sadaka kwa mkono wako mwenyewe basi unajiepusha na ajali mbaya, unajiepusha na balaa na maafa sabini na mitego ya mashetani sabini na ambamo kila shetani yuko anakuambia ‘ewe fulani! Usitoe Sadaka kamwe.”
2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Mgonjwa atoe Sadaka kwa mkono wake mwenyewe na anayempa amwambie amwombee dua”.
3. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hadith zake amesema kuwa:
“Mkono uliye juu yaani mtoaji ni afadhali kuliko mkono ule ulio chini yake, yaani mpokeaji.”
4. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:
“Kuna aina tatu ya mikono:
wa kwanza ni mkono ule wa Allah swt ambao uko juu kabisa na kwa hakika neema zote ni za Allah swt,
mkono wa pili ni ule mkono wa yule mtu anaye toa, ambaye anatoa katika njia ya Allah swt na
mkono wa tatu ni wa yule anaye pokea ambao mkono uliochini wa yule anayetoa. Kwa hivyo enyi watu chochote kile kinachobakia miongoni mwenu mtoe katika njia ya Allah swt na msikalifishe nafsi zenu”.