read

22. Kumrudisha Masikini ni Karaha

Kumrudisha masikini ni karaha hata kama ustahiki wake utakuwa mashakani, lakini lazima apewe chochote na kama hakuna chochote cha kumpa basi unaweza kumwondoa kwa maneno mazuri na matamu.

1. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema:
“Msimvunje moyo mwombaji hata kama atakuwa amekuja kuomba katika usafiri wa farasi.”

2. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema:
“Iwapo mtoaji atakuwa anajua wema na fadhila za kutoa Sadaka basi kamwe hatamrudisha mtu yeyote bila ya kumpa kitu chochote.”

3. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Kamwe msiwarudishe mikono mitupu waombaji. Iwapo katika waombaji, wasingekuwa waongo na wadanganyifu. basi kamwe wasinge pona wanaowa rudisha (waombaji).”

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kamwe hakumrudisha masikini yeyote aliyemwomba asaidiwe Sadaka. Na kama Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa hana chochote cha kumpa basi alikuwa akimwambia kwa lugha tamu Allah swt atakujaalia Insha-Allah.”

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Mtume Ibrahimu a.s. daima amekuwa akiwahudumia na kuwakirimu wageni, na pale alipokuwa hakuwapata wageni wowote wale, basi alikuwa akifunga mlango wake na akitoka kwenda kuwatafuta wageni.”

Na katika hadithi hiyo hiyo tunapata wakati mmoja Malaika Jibrail alimwijia Mtume Ibrahim a.s. na kumwambia :
“Allah swt amenituma safari hii kwa mja wake mmoja ambaye ameweka marafiki Wake kama ni Khalil Wake.”

Kwa hayo Mtume Ibrahim a.s. akaingiwa na shauku ya kutaka kumjua na akasema :
“Tafadhali sana naomba unitambulishe huyo umzungumzaye, nami nitapenda kwenda mbele yake.”

Jibrail a.s. akasema :
“Ewe Khalil (rafiki)! Ndiwe wewe tu!”

Basi Mtume Ibrahim a.s. akamwambia :
“Ewe Jibrail a.s.! Je! kwa sababu gani amenihurumia (Mwenyezi Mungu) hivyo?

Hapo Malaika Jibrail a.s. akamjibu :
“Kwa sababu wewe kamwe haujamnyooshea mkono yeyote, na wewe daima haujawahi kumkatalia yeyote aliyekuja kukuomba.”

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa Mtume wa Allah swt alikuwa akisema:
“Kamwe msimrudishe mikono tupu mwombaji. Hata kama mtakuwa katika hali ya ugumu kiasi gani.

7. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema kuwa Mtume Musa a.s. wakati alipokuwa akimlilia Allah swt, Allah swt alimwambia :
“Ewe Musa mwombaji hata kama ukimpa kidogo mpe ili utunze heshima ya mwombaji, na kama hicho pia hauna basi kwa maneno matamu na kauli nzuri umwambie na kumwomba msamaha. Kwa sababu miongoni mwa waombaji, mara nyingine si lazima atokane na binadamu au Majini bali anakuwa ni Malaika wa Rehema.
Kwa hiyo Malaika huyo ndiye anaye wajaribu watu na kile nilicho kujaalieni na anaomba kutoka Neema zile mlizobarikiwa na mimi (mwenyezi mungu) kwa hivyo, ewe mwana wa Imran angalia vile tabia (mwenendo) yako itakavyo kuwa.”

8. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa riwaya kuwa siku moja mtu mmoja alikuja kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuomba, hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliwaangalia Ma-Sahaba wake na kuwaambia,
“Enyi Ma-Sahaba wangu ! Msaidieni.”

Na mmoja katika Ma-Sahaba wake akamsaidia kifaa cha dhahabu. Aliyekuja kuomba akasema, “Je! hii ndiyo yote (kila kitu) yako?”

Yule Sahaba wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akajibu:
“Naam, ndiyo hiyo”.

Yule mwombaji akasema:
“Mimi nimekubalia hivyo. Mimi si Jini wala si binadamu; bali mimi ni Malaika niliyetumwa na Allah swt nije nikujaribu na kwa hakika nimekuona wewe miongoni mwa watu wenye kushukuru neema za Allah swt. Mungu akujaalie kila la heri.”

9. Sa’ad bin Musayyab anasema kuwa siku moja wakati wa sala ya asubuhi yeye alikuwa pamoja na Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s., akatokeza mwombaji mmoja na wakati huo Al Imam Zaynul 'Abediin ibn Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema:
“Mpeni huyo mwombaji - kumbukeni kuwa - kamwe msimwondoe mwombaji katika hali ya kuhuzunika yaani msimwondoe mwombaji bila kumpa chochote”.

10. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ananakili riwaya kutoka baba yake mzazi Imam Musa al-Kadhim a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa:
“Mpokee mwombaji aondoke hata kwa kidogo na kwa mapenzi na huruma pia. Kwa sababu mara nyingi anayekuja kuomba huwa si kutoka binadamu au Majini bali huwa njia moja kujaribiwa (nyie) [mnajaribiwa] na zile neema mlizobarikiwa na Mwenyezi Mungu na mnatahiniwa namna itakavyokuwa mwenendo wenu katika kutoa sadaka katika njia ya Allah swt.”

11. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha :
“Masikini anapokuja kwenu basi anakuwa ni mjumbe wa Allah swt na yeyote yule atakaye muudhi na atakayemhudhunisha basi atakuwa amemhudhunisha Allah swt na yeyote yule atakaye kuwa amempa chochote basi ajue kuwa amempa Allah swt”.

12. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anaripoti kutoka kwa wazazi wake a.s ambao wamesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Wakati Ummah wangu utakapogeuza uso au utakapo wageuzia uso wale wanao hitaji msaada wao na watakapoanza kutembea kwa maringo basi wakati huo Allah swt atasema: kwa kiapo cha utukufu na ukuu wangu hawa watu watakomeshana wao kwa wao na hivyo ndivyo nitakavyowaonjesha adhabu yao.”