read

24. Sadaka Ikisha Tolewa Haiwezi Kurudishwa

Huwezi kurudisha sadaka na baada ya kumtoa mtumwa kama sadaka huwezi kumchukua tena katika miliki yako.

1. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. daima alikuwa akisema kuwa:
“Mtu yeyote anayetoa Sadaka na iwapo Sadaka hiyo itakataliwa au Sadaka hiyo itarudishwa basi yule mtoa Sadaka haruhusiwi kuila au kuitumia tena hiyo Sadaka kwa ajili yake. Na badala yake hana njia yoyote isipokuwa aigawe Sadaka kwa mtu mwingine. Hatakuwa na ruhusa kwa vyovyote vile vya kuitumia hiyo Sadaka isipokuwa itolewe tena Sadaka kwa mtu mwingine. Vile vile mfano wake inachukuliwa kuwa mtu anapomfanya huru mtumwa katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya kutaka furaha ya Allah swt basi kamwe hawezi kumchukua tena yule mtuma (aliyefanywa huru) akamfanya mtumwa wake. Na baada ya kumfanya huru mtumwa na huyo mtumwa atakapo rudi kwake basi hawezi kumweka vile alivyokuwa amemweka mwanzoni kabla ya kumfanya huru katika njia ya Allah swt. Na vivyo hivyo ndivyo swala hizi zinausiana na Sadaka pia.”

2. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema:
“Yeyote yule atakayekuwa ametoa Sadaka na iwapo Sadaka hiyo itamrejea yeye tena basi yeye mwenyewe hataweza kuitumia wala hataweza kuiuza, kwa sababu kitu hicho kilishatolewa katika njia ya Allah swt na kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt na hivyo hakuna kitakachoweza kushirikishwa katika swala hilo, na mfano wake pia ni sawa na ule wa kumfanya huru mtumwa hivyo hataweza kurudishwa tena katika utumwa.”

3. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:
“Iwapo mtu atanuia kutoa Sadaka kwa ajili ya mtu fulani anayeuhitaji msaada huo na wakati huo akapata kujua kuwa mtu huyo ameshaondoka, basi hawezi kuirudisha na kuichanganya hiyo mali katika mali yake na badala yake itambidi amgawie mtu mwingine.”

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
Kuna mtu alimwuliza iwapo mtu alimfanya huru mtumwa bado ambaye hajafikia umri wa kubalehe Je! sheria inasemaje?

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu:
“Hakuna tatizo lolote ndani yake lakini sheria itakayotumika hapo ni kama ile ya kutoa Sadaka (yaani baada ya kumfanya huru mara moja hauwezi kumrudisha katika utumwa tena).”