42. Ni Sunnah Kuwahudumia Kwanza Watu wa Nyumba Yako
Ni sunnah kuwawia wana nyumba wako kwa wema kabla ya kutoa sadaka kwa watu wa nje.
1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. siku moja aliwasaidia waombaji watatu na wa nne alipokuja hakumpa chochote. Na hapo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema:
“Iwapo mtu atakuwa na Dirham elfu thelathini au arobaini na zote akazigawa kwa kusaidia au sadaka bila ya kubakiza chochote kwa ajili ya wana nyumba wake basi huyo mtu atakuwa mmoja miongoni mwa watu watatu ambao dua zao hazikubaliwi na Allah swt. Na katika watu hawa watatu: mmoja ni yule ambaye bila kutimiza wajibu wake anagawa mali yote kama sadaka au kusaidia, na baada ya hapo anakaa akiomba dua:
“Ewe Allah swt naomba unipe riziki.”
Basi hapo atajibiwa, “Je! mimi nilikuwa sikukufanyia njia ya kujipatia riziki?”
2. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Bora ya sadaka zote ni ile inayotolewa wakati mtu anapokuwa na uwezo wa kutoa yaani katika hali ya utajiri na unapokuwa sawa.”
3. Hisham bin Al Muthanna anasema:
“Kuna mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuhusu tafsiri ya ayah Surah An-a’am, 6, Ayah 141:
‘Na Yeye ndiye aliyeziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.’
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu,
“Katika Ansaar alikuwako mtu mmoja (aliwapa jina lao) ambaye alikuwa ana shamba. Pale mazao yake yalipokuwa yakiwa tayari yeye alikuwa akigawa yote katika sadaka, na alikuwa hawapi chochote watoto na wana nyumba yake; na kwa tendo lake hili Allah swt alikuwa akimhesabia yeye kama ni mfujaji na mbadhirifu.”
4. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Baada ya mtu kujitolea kile kiasi alicho na dharura nacho kwa mujibu wa mahitaji yake na baadaye katika kiasi kinachobaki akitoa sadaka basi hiyo sadaka ni bora kabisa.”
5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema:
“Mojawapo katika Nasiha na Mawaidha ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ilikuwa ni kila aina ya wema ni sadaka mojawapo, na sadaka iliyo bora kabisa ni pale kutoa wakati mtu ameshajitimizia wajibu wake na ametosheka, na mkumbuke kuwa muwape wale ambao kwao nyie mnawajibika kuwatimizia mahitaji yao.
Mkono wa mtoaji ni afadhali kuliko mkono wa mpokeaji. Kwa hakika mtu ambaye anachuma kwa uwezo wake na kutumia kwa ajili yake na kuwatimiza mahitaji yao basi Allah swt kamwe hatamlaumu.”
6. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliijiwa na mtu mmoja na kumlalamikia kuhusu njaa:
“Basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimtuma mmoja wa wake zake naye alipowaendea wakamwambia kuwa wao walikuwa hawana chochote isipokuwa maji ya kunywa tu, na kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia, Je! kuna yeyote yule atakaye mchukua mtu huyu kuwa mgeni wake kwa usiku huo?”
Na kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema,
“Ewe Mtume wa Allah swt ! Mimi nakubali kumchukua huyu kama mgeni wangu kwa usiku wa leo.” Na walipofika nyumbani kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Imam a.s. alimwuliza Bi. Fatimah az-Zahra a.s. “Je! nyumbani kuna chakula chochote?”
Kwa kusikia hayo Bi. Fatimah az-Zahra a.s. akasema, tuna chakula kiasi cha kuwalisha watoto wetu tu lakini na mgeni pia ana haki yake.”
Na hapo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. akasema
“Wewe walaze watoto, na uizime taa.”
Asubuhi Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alipokuja mbele ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwelezea kisa kilivyotokea na wakati bado akiwa anaelezea kisa hicho ayah ifuatayo iliteremshwa Surah Al Hashri, 59, ayah 9:
‘Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.’