read

20. Kuwasaidia Majamaa na Ndugu Kuna Thawabu Zaidi

1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripoti riwayah moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mtu mmoja alimwuliza Mtume s.a.w.w. :
“Ewe Mtume wa Allah! Je! ni Sadaka ipi iliyo bora kabisa?”

Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu:
“Sadaka ile ambayo watakayo pewa wale jamaa na ndugu ambao hata kama alikuwa amekorofishana nao au amegombana nao au hawana uhusiano nao kwa sababu ya magomvi.”

2. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Iwapo wewe unatoa kumi kwa ajili ya Sadaka , basi ili kuwasaidia Mu’min toa kumi na nane na yule ambaye hawezi kabisa msaidie kwa ishirini na kwa ajili ya kuwasaidia jamaa na ndugu kwa wema utoe ishirini na nne.”

3. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema Riwayah kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa amesema:
“Mtu yeyote atakaye wasaidia jamaa na ndugu zake katika kwenda Kuhijji au ‘Umra, basi Allah swt atamjaalia thawabu za Hijja mbili na ‘Umra mbili, na yeyote yule atakayemsaidia ndugu yake Mu’min basi Allah swt atamlipa kwa kisicho na kifani.”

4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema kuwa:
“Iwapo mtu atawasaidia jamaa au ndugu zake ambao wana shida ni muhtaji basi hiyo siyo Sadaka.”

5. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwayah moja ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema:
“Kwa mtu yeyote yule ambaye atakwenda mwenyewe kwenda kumsaidia jamaa au ndugu yake mwenye shida na kutoa kitu chochote kwenye mali yake na kumsaidia basi Allah swt atamjaalia ujira wa mashahidi mia moja na kwa kila hatua atakayotembea atamwandikia mema elfu arobaini, na kiasi hicho hicho cha maovu yake yatasamehewa. Na vile vile kiasi hicho hicho ataongezewa daraja lake mbele ya Allah swt na atamwandika miongoni mwa wale waja wake halisi waliofanya ibada yao kwa uhalisi kwa muda wa miaka mia moja.”

6. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., aliulizwa na mtu mmoja :
“Ewe Mwana wa Mtume wa Allah! Je! yeyote yule anayekuja kuomba mlangoni anastahili kupewa Sadaka au badala yake tuwape jamaa na ndugu zetu Sadaka hiyo?”

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :
“Kwa hakika kuwapelekea msaada [Sadaka] jamaa na ndugu wa mtu zina thawabu nyingi zaidi.”

7. Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. aliandikiwa barua na mtu mmoja akimwuliza:
“Iwapo mtu anaweza kunuia kuwa mimi katika mali yangu nitatoa sehemu fulani ya mali nitamsaidia mtu fulani na katika kipindi hicho iwapo atakuja kujua kuna mtu katika ndugu na jamaa zake ambaye ni kweli anashida na anahitaji msaada wake basi Je! huyo mtu anaweza kubadilisha nia yake ya kumsaidia jamaa yake badala ya kumpa mtu aliyekuwa amenuia hapo kabla?”

Al Imam Muhammad Sahibuz-Zamaan a.s. akamjibu kuwa:
“Utaangalia ukaribu wa watu hao na yule aliye karibu nawe katika madhehebu umpatie na lau kama wote wawili kama watakuwa wanatokana na dhehebu moja tu basi kwa mujibu wa kauli ya Al Imam Musa al-Kadhim a.s. kuwa kugawanywe kati kati yaani watu wote wawili wapewe nusu kwa nusu, kwa sababu iwapo kutakuwa na jamaa na ndugu ambao wana shida na taabu basi huwezi kutoa Sadaka na kuwapa wengine. Na kwa hakika kwa kufanya hivyo utakuwa umepata thawabu na fadhila za Sadaka.”