28. Baada ya Kutimiza Mahitaji ya Familia, Wasaidiwe Wengine
Mtu ambaye amesha timiza mahitaji ya watoto wake na ndugu na jamaa zake basi inambidi ajitaabishe nafsi yake kwa kuwahudumia wengine, hata kama huduma hiyo itakuwa ni bure lakini ni sunnah.
1. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliulizwa na mtu mmoja :
“Ewe Mawla! Je! ni mtu gani mwenzi wako aliyebora kabisa?”
Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alijibu,
“Ni wale ambao wanawawia na kuwafanyia mema ndugu zao katika imani katika hali ya raha, starehe na shida.”
Na aliendelea kueleza kuwa,
“Ewe Jamil, yeyote yule aliye nacho kingi basi kutenda kwake mema ni rahisi sana. Kwani Allah swt amewasifu wale walio nacho kidogo na huku wanafanya mema.
Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Hashri, 59, Ayah 9:
“Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.”
2. Jamil bin Darraj anasema kuwa:
“Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alitukusanyisha na kutuambia,
“Miongoni mwenu bora kabisa ni yule ambaye ni mkarimu na mtenda mema kwa wenzake na mwovu kabisa ni yule ambaye ni bahili na anawawia wengine kwa hali hiyo na bora ya matendo ni kule kutendeana mema pamoja na ndugu zenu na vile vile kuwatimizia haja na mahitaji yao na kwa hakika matendo haya yanamuudhi na kumvunja nguvu Shaitani na kunamwepusha mtu asiingie Jahannam na badala yake aingizwe Jannat. Ewe Jamil! Naomba uwafikishie habari hizi muumin halisi.”
3. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimfanyia usia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa kumwambia:
“Ewe Ali! Nina ku-usia mambo matatu ambayo kwa hakika yanathibitisha imani.
• Moja ni kwamba wakati wa shida na dhiki kutoa mali au chochote na kuitumia katika njia ya Allah swt
• pili kuwawia waadilifu watu
• tatu ni kuwapa elimu wale wanao tafuta elimu kama wanataka kujifunza elimu.”
4. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amenakili riwaya moja kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambaye amesema:
“Bora ya sadaka ni ile ambayo inatolewa bila ya kuwa na shida yoyote na inatolewa kwa furaha.”
Mwandishi anasema hadithi hii inawahusu wale ambao wana watoto, familia na ndugu na majamaa. Yeye anakuwa na majukumu ya kuwauliza na kuwatimizia haja hawa watu wanaomtegemea yeye na hivyo baada ya kumalizana nao anatoa sadaka kwa furaha.
5. Sama’a anasema kuwa:
“Siku moja alimwuliza Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.,
“Iwapo mtu atakuwa na chakula cha kumtosha siku moja, Je! anaweza kumsaidia yule mtu mwingine ambaye hana chochote? Au tuseme kama mtu ana chakula cha kuweza kumsaidia mwezi mmoja anaweza kuwasaidia wengine ambao hawana kiasi hicho au yeye hana zaidi bali ana kiasi kile tu cha kumtosha yeye na hivyo hawezi kumsaidia mwingine, basi mtu kama huyo atakuwa amelaumiwa na kushutumiwa?”
Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akamjibu,
“Katika suala hili yapo mambo mawili, miongoni mwenu kuna watu ambao wao wanawasaidia na kuwapenda wengine zaidi kuliko nafsi zao na ambapo Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al-Hashr, 59, Ayah 9 :
“Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa, bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.”
Na jambo la pili ni kwamba yule ambaye ana kiasi kile tu ambacho kinamtosha yeye tu, basi mtu kama huyo hayuko katika lawama.
Naam, mkono ulio juu uko afadhali kuliko mkono uliopo chini (yaani yule anayempa mtu ni mkono wa juu na yule anayepokea ni mkono wa chini) na daima wakati wa kutoa lazima aanzie na wale ambao kwa hakika wako chini ya utunzaji wake (anawajibika kuwatunza na kuwasaidia na kuwatimizia mahitaji yao).”
6. Al Imam Musa al-Kadhim a.s. aliambiwa na ‘Ali bin Sued Assinani: “Ewe Mawla! Naomba unifanyie usia.”
Kwa hayo Imam a.s. alimwambia,
“Fanya Taqwa. Na umwogope Allah swt”.
Na hapo Imam a.s. alinyamaza kimya, basi yeye akasema :
“Ewe Imam a.s.! Nina shida kubwa sana. Mimi nimeshindwa kabisa sina uwezo wowote, yaani fikiria kwamba sina nguo yoyote juu ya mwili wangu iwapo fulani ibn fulani asingenivulia nguo zake akanipa na kunivalisha mimi.”
Katika kumjibu Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimjibu:
“Funga saumu na utoe sadaka.”
Naye kwa kunyenyekea alisema:
“Je! nitoe katika yale ambayo mimi ninasaidiwa na watu? Na nitoe kiasi gani kutoka humo?”
Al Imam Musa al-Kadhim a.s. alimjibu:
“Chochote kile Allah swt anachokufikishia katika riziki yako toa humo sadaka, kwa kufanya hivyo acha nafsi yako ivumilie kidogo kwa ajili ya kuwatolea wengine walio na shida pia.”
7. Abu Basir ananakili riwaya moja ama kutoka kwa Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. au Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:
“Yeye aliuliza, bora ya sadaka zote ni ipi?”
Imam a.s. akamjibu:
“Sadaka bora ni kutoka ile mali ambayo mtu hana nyingi (kitu ambacho unacho kidogo au cha kukutosheleza tu wewe, unatoa humo sadaka), Je! wewe huna habari Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al-Hashr, 59, Ayah 9 :
“Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.”
8. Katika hadithi moja ndefu Masufi walileta dalili moja mbele ya Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa:
“Allah swt amesema katika Qur’an Tukufu, Surah Al-Hashr, 59, Ayah 9 :
‘Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa , bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.’
“inamaanisha sisi tutoe mali yetu yote (na tusibakishe chochote kwa ajili yetu).”
Imam a.s. aliwajibu:
“Kwa ayah hiyo ni ufafanuzi ambavyo watendaji walikuwa wakitenda kama Allah swt alikuwa ameruhusu. Hakuna aliye wazuia hao, na ujira wao pia upo kwa Allah swt, lakini hiyo ni amri ya Allah swt ambayo ni kinyume na matendo yao.
Na sababu ya kufanya hivyo ni kwamba Allah swt anamwonea huruma muumin ili huyo muumin asiweze kuwaletea shida na kuwadhuru nafsi za wananyumba katika familia yao watoto dhaifu na watoto wadogo, wote walio dhaifu, na ambao hawawezi kustahimili njaa, wazee waume kwa wanawake.
Iwapo mimi nitakuwa na kipande kimoja cha mkate na nikagawa sadaka, basi wale wote wanaonitegemea mie wataangamia na kuteketea.
Ndyio maana Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, iwapo mtu atakuwa na kokwa tano za tende au mikate mitano au Dinar tano au Dirham tano na yeye anataka kuzitumia zote, basi itakuwa ni vyema kabisa iwapo yeye azitumie kwa ajili ya wazazi wake, na baadaye kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake na tabaka la tatu kwa ajili ya ndugu na jamaa zake ambao wana shida na wanahitaji msaada wake, na baada ya hapo awasaidie majirani ambao ni mafakiri, na mwishoni kabisa atumie kwa ajili ya kuwasaidia wengineo katika njia ya Allah swt.
Na baadaye akaendelea kusema kuwa siku moja ilitokea mtu mmoja kutokea Ansaar alifariki (kufa). Kwa mujibu wa usia wake yeye alikuwa na watumwa watano au sita ambao wote walifanywa (kwa mujibu wa usia huo) huru na wakaondoka zao na huko nyuma familia yake hakuwaachia chochote watoto wadogo wadogo na wana nyumba yake wote wakawa ni muhtaji, wakawa wao sasa wanategemea misaada kutoka wengine ilhali huyu bwana alikuwa na watumwa watano au sita.
Na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipojulishwa habari hizo alisikitika mno na akasema,
“Laiti kama nyie mngelikuwa mmenijulisheni kabla kuwa mtu huyo amewafanya watoto na wenye nyumba yake kuwa muhtaji (ni watu wenye kuhitaji misaada na sadaka) basi mimi kamwe nisingelikubali mtu huyu azikwe katika makaburi ya Waislam.’
Halafu anaedelea kusema kuwa baba yangu (yaani Al Imam Musa al-Kadhim a.s.) amenakili riwaya kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa mtoaji sadaka inambidi kwanza awatimizie mahitaji ya wale wanao mtegemea yeye; na wale ndugu na jamaa walio wakaribu zaidi ndio awape kwanza (yaani wazazi, mke, watoto na ndugu zake na majamaa wanaofuatia wa karibu zaidi) na baada ya hapo majamaa na ndugu wenye uhusiano wenye ujamaa nao wa mbali ndio wapewe”.