Aya 34: Msujudieni Adam
Mwenyezi Mungu aliwaamrisha malaika kumsujudia Adam kwa kudhihirisha ubora wake kuliko wao na kuliko viumbe vyake vyote.
Hapana tafsiri ya ubora huu isipokuwa ubora wa elimu au ubora wa aliye nayo. Kwa sababu elimu, kama ilivyothibiti, ndiyo kipimo cha kila hatua anayopiga mtu ya maendeleo na ukamilifu; kama vile ambavyo ujinga ni msingi wa kurudi nyuma.
Hawezi kuwa juu isipokuwa kwa elimu. Mwenye elimu siku zote hufuatwa, na mjinga siku zote hufuata. Kwa ajili hii Uislamu umewajibisha elimu kwa kila Mwislamu mwanamume na mwanamke.
Wafasiri wengi wamesema kwamba sijda ilikuwa ni ya ki-maamkuzi tu; Kama kuinama na kuinua mkono. Kwa sababu kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu. Lakini haya sio kweli kwa mujibu wa mwenye tafsiri ya Majmaul-Bayan, kwani kama ingelikuwahivyo,basi, Iblis asingelikataa kumsujudia.
Kimsingi sijda ilikuwa ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu sio kwa ajili ya Adam. Amri ya kumsujudia Adam iliwahusu Malaika wote bila ya kumvua yoyote, hata Jibril na Mikail pia, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na tulipowaambia Malaika, msujudieni Adam. Basi wakamsujudia isipokuwa Iblis; yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake.” (18:50)
Hakuna njia ya kumjua Iblis, shetani na jini, isipokuwa kwa njia ya wahyi tu; kama ilivyo katika kuwajua Malaika. Maelezo yamekwishaelezwa katika Aya iliyotangulia.
Wafasiri wameonyesha utafiti usiokuwa na manufaa. Kwa hivyo tumeuacha kwa kufupiliza yayale yanayofahamishwa na dhahiri ya maneno. Tumekwisha onyesha katika kurasa zilizotangulia baadhi ya yale yanayonasibishwa kwa Iblis katika vigano. Ni picha iliyo wazi ya watu wengi wa siku hizi katika kucheza kwao matamko, ambako hakutimizielimu aufaniyoyotezaidi ya kubobokwa tu.
وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنْتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ {35}
(nafsi zao).
فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ {36}
فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِنْ رَبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ {37}
قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنْ تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ {38}
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ {39}