read

Aya 84-86: Hamtamwaga Damu Zenu

Maelezo

Mazungumzo ya Mayahudi na matatizo yao hayajakwisha; na yanayokuja ni mengi. Kwa muhtasari wa Aya za Mayahudi, ni kwamba wao kila wanapopewa mwito wa uongofu na msimamo mzuri wanakakamia katika kueneza ufisadi duniani na wanaendelea katika upotevu, kama kwamba wao wameumbwa kumuasi Mwenyezi Mungu na kuikhalifu haki. Tawrat yao inawaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu, wao wanaabudu ndama; Musa anawaambia: Hii Tawrat kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wao wanasema; “Tuonyeshe huyo Mwenyezi Mungu wazi wazi”. Tena Musa anawaambia: “Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwenu na mumwombe msamaha,” wao wanafanya mzaha na stihizai.

Ikiwa Nabii Musa (a.s.) tu walimfanyia hivyo naye ni Mwisrail mwenzao, je mwingine watamfanyiaje? Mfalme Edward I aliwafukuza Uingereza na wakateswa na Hitler huko Ujerumani baada ya kuwajua walivyo. Wao wanastahili zaidi ya hayo. Tumekwishaeleza vile walivyofanyiwa na Fir’aun, Nebukadnezzar na Warumi.

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba miongoni mwa ahadi alizozichukua Mwenyezi Mungu kwa Mayahudi katika Tawrat ni kutouana wenyewe kwa wenyewe wala wasimtoe yeyote katika nyumba yake. Na Mayahudi hawakanushi ahadi hizi, bali hawana nafasi ya kuzikanusha kwa sababu zinapatikana katika Tawrat ambayo wanaiamini kwa ukweli na kwamba hiyo ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini pamoja na hayo yote waliikhalifu kwa makusudi, kwa hivyo ikawasimamia hoja.

Maana

Na tulipochukuwa ahadi yenu kuwa hamtamwaga damu zenu wala hamtatoana majumbani mwenu.

Anarudia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwakumbusha Wana wa Israil ahadi walizoziweka kwa ulimi wa Musa na Mitume wengine waliokuwa baada yake. Miongoni mwa ahadi hizo ni kutomwaga damu na kutotoana majumbani mwao.

Nanyi mkakubali na hali mnashuhudia.

Yaani mlikubali ahadi na kushuhudiana nyinyi wenyewe. Unaweza kuuliza: Kukubali na kushuhudia ni kitu kimoja, sasa vipi ikafaa kuunganisha kitu kwa kitu chenyewe?

Jibu: Inawezekana kuwa ni katika upande wa kutilia mkazo. Vile vile inawezekana kuwa makusudio ya kukubali ni kukubali Mayahudi wa zamani na kushuhudia ni kwa watakaokuja. Kwa sababu wa zamani walikubali na wakakiri ahadi.

Kisha nyinyi hao hao mnajiua, na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao.

Yaani nyinyi baada ya kukiri kwenu ahadi, mnaivunja wenyewe, mwenye nguvu anamuua mnyonge na kumtoa katika nyumba yake.

Mkisaidiana dhidi yao kwa (njia ya) dhambi na uadui.

Aya inaonyesha kugawanyika Mayahudi na kusaidiana kila kikundi na Waarabu dhidi ya kikundi kingine cha Mayahudi.
Kwa ufupi kisa kilikuwa hivi: Aus na Khazraj ni koo mbili za Kiarabu zenye asili moja, kwa sababu Aus na Khazraj walikuwa ndugu. Koo mbili hizi zilikuwa na uadui na vita kati yao kabla ya Uislamu na walikuwa wakimshirikisha Mwenyezi Mungu, hawajui pepo wala moto wala Kiyama au Kitabu.

Na Mayahudi nao walikuwa na koo tatu: Bani Qaynuqa’a, Bani Quraidha na Bani Nadhir, nao walikuwa na uadui na vita kama ilivyokuwa kati ya Aus na Khazraj pamoja na kuwa hawa Mayahudi walikuwa katika asili moja na dini yao ni moja. Wote hao, Mayahudi na Waarabu walikuwa ni wakazi wa Madina.

Bani Qaynuqa’a walikuwa wakisaidiana na Aus dhidi ya Bani Nadhir na Quraidha; kama ambavyo Bani Nadhir na Bani Quraidha walikuwa wakisaidiana na Khazraj dhidi ya Qaynuqa’a. Vita vinapochacha Myahudi alikuwa akimuua ndugu yake Myahudi na kumtoa nyumbani kwake akiweza. Lakini kama Yahudi akitekwa na Mwarabu, basi Mayahudi hukomboana hata kama ni adui yake mkubwa.

Kwa ufupi ni kwamba Mayahudi hawaoni kizuizi kuwaua Mayahudi wenzao kiasi cha kusaidiana na Waarabu, lakini Mwarabu akimteka nyara Yahudi, basi Yahudi mwenzake huingiwa na huruma na kutoa fidia kumkomboa mwenzake ingawaje ni adui yake. Kwa hivyo Yahudi anahalalisha kumuua ndugu yake na kumfukuza, lakini asiwe mateka. Walikuwa wakidai kwamba Tawrat yao ndiyo inayowaamrisha kukomboa mateka wa Kiyahudi.

Ndipo Mwenyezi Mungu akawajibu kwamba Tawrat yao vile vile imewaamrisha kutouana na kutotoana majumbani; sasa vipi mmeiasi Tawrat katika kuua, na kuitii katika kukomboa mateka?

Hiindiyotafsiriya kauliyake MwenyeziMungu:

Na wakiwajia mateka mnawakomboa na hali kumeharamishwa kwenu kuwatoa. Je mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi?

Walilolikataa ni kule kukatazwa kuua, kusaidiana katika dhambi na uadui na kutoana majumbani. Waliloamini, ni lile la kutoleana fidia mateka. Na hii ndiyo istihzai hasa na kucheza na dini.

Unaweza kuuliza, lenye kuharamishwa kwao ni kuua na kusaidiana na kutoana majumbani; kwa nini Mwenyezi Mungu amehusisha kutoana majumbani katika Aya hii? Jibu: Ndio yote ni haramu, lakini Mwenyezi Mungu amehusisha kutoana kwa kutaja mara ya pili kwa sababu ya kutilia mkazo tu. Kwa sababu kutoana majumbani huendelea, kinyume na kuua kama walivyosema wafasiri wengine.

Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya duniani.

Malipo yanaweza kuwa ya heri au ya shari; kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

وَجَزَاهُمْ بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا {12}

“Na malipo yao kutokana na vile walivyosubiri ni pepo na nguo za hariri.” (76:12)

وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا{93}

“Na mwenye kumuua mumin kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, humo atadumu...(4:93)

Hao ndio walionunua maisha ya dunia kwa akhera; kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa.

Mwenyezi Mungu hakuharamisha, katika Aya hii wala nyingine chakula kizuri na mavazi ya kifahari, isipokua anamkemea mwenye kuiuza dini yake kwa ajili ya dunia yake na akaishi maisha ya kidhulma na upotevu.
Hakika Mwenyezi Mungu anakataza ufisadi duniani na sio vipambo na neema za dunia, bali hakika Yeye Mwenyezi Mungu amekanusha sana kuharamisha neema na ladha katika dunia hii; kama anavyosema:

قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا{32}

“Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amewatolea waja wake. Na, vitu vizuri katika riziki? Sema: hivyo ni kwa walioamini... .(7:32)

Yaani ni halali kwa aliyevichuma kwa njia ya halali na ni haramu kwa anayevitafuta kwa kunyang’anya, kuhadaa na utapeli.

Kwa ufupi ni kwamba misingi ya ki-Qur’an ni kuishi watu katika kusaidiana yale yaliyo na wema kwa wote. Ama misingi ya Kizayuni ya kikoloni, ni “Maadamu mimi ninaishi basi na uangamie ulimwengu” na kila mwenye kwenda na msingi huu, basi ni Mzayuni akijua au asijue; hana budi kukumbana na uadilifu wa mbingu na ardhi na kuteremkiwa na mateso na balaa.

Mayahudi Na Ukomunisti Na Ubepari

Inadhihiri kutokana na Aya tukufu kwamba kugawanyika Mayahudi katika makundi mawili ni mambo waliyoyarithi kutoka kwa mababa na mababu zao ili wazidishe moto kuwaka kwa upande fulani na wapate masilahi yao kwa upande wa pili. Kama ilivyo kuwa kugeuka geuka kwao ndio asili yao na ada yao.

Kabla ya nusu karne walikuwa wakilingania ukomunisti na ndio wao leo wanaoulemea ubepari. Hawana lengo lolote isipokuwa kuugawa ulimwengu na kuanzisha vita na fitina ili watekeleze siasa zao za ukandimizaji na ukupe wa kunyonya jasho la watu.

لَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِنْ بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنْفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ {87}

Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukawafuatisha Mitume baada yake; na tukampa Isa,
mwana wa Maryam, hoja zilizo wazi wazi, na tukamtia nguvu kwa roho takatifu. Kila alipowafikia Mtume kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlikivuna, kundi moja mkalikadhibisha na kundi jingine mkaliua!

وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَلْ لَعَنَهُمُ اللَّهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَا يُؤْمِنُونَ {88}

Na walisema: Ndiyo zetu zimefunikwa, bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao; kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini!