read

Aya 104-105: Enyi Mlioamini

Maelezo

Enyi mlioamini msiseme ‘Raaina’ bali semeni ‘Undhurna’ Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Waislamu walikuwa wakisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Raina; Yaani tusikilize. Mayahudi nao wakalitumia neno hili kwa maana ya mpumbavu (katika lugha yao). Walipolaumiwa, wakasema tunasema kama wasemavyo Waislamu. Ndipo Mwenyezi Mungu akawakataza hilo kwa kauli yake: Msiseme Raina na semeni: Undhurna. Makusudio ya Undhurna katika Aya ni kuangalia Mtume hali yao wakati anapozungumza; angoje ili wafahamu na waelewe maneno yote”.

Uzindushi

Mwito wa kwanza katika Sura ya Baqara umekuja kwa watu wote na mwito wenyewe ni Uislamu na kumwabudu Mwenyezi Mungu; pale aliposema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika Aya ya 21: “Enyi watu mwabuduni Mola wenu ambaye amewaumba...”

MwitowapiliulikuwakwawanaIsrail,taifakubwaambalolililetataifala Kikristo. Mwito huu wa pili ulikuja kukumbusha kuondolewa mateso kwa waana wa Israil na kupatiwa neema; ni pale aliposema Mwenyezi Mungu katika Aya 40: “Enyi wana wa Israil kumbukeni neema yangu niliyowaneemesha... ”.

Mwito wa tatu umekuja kwa umma wa Muhammad (s.a.w.) katika Aya hii: “Enyi mlioamini msiseme ‘Raaina’”, ambayo ni kuwafundisha Waislamu adabu za sheria baada ya kusilimu na kumwamini Mwenyezi Mungu.

Utaratibuhuuwamiitohiimitatundioutaratibuwakikawaida; yaani kuanza kuwalingania watu kwenye imani ya Mwenyezi Mungu, kisha kumtajia fadhila za Mwenyezi Mungu yule mwenye kumwamini Mungu kabla ya Utume tena kumfunza kuamini adabu za Mwenyezi Mungu yule mwenye kuamini Utume. Hii ni namna mojawapo ya ufasaha wa Qur’an.

Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu wala washirikina mteremshiwe heri kutoka kwa Mola wenu.

Si ajabu kwa washirikina, Wayahudi na wakristo pamoja na makafiri, kuchukia yote aliyoteremshiwa Muhammad na vile alivyohusishwa na Mwenyezi Mungu kwa fadhila na hidaya na utengeneo; isipokuwa ajabu ni kutolichukia hilo.

Na Mwenyezi Mungu humhusisha kwa rehema Zake amtakaye.

Amirul Muminin anasema: “Makusudio ya rehema hapa ni Utume.”

Husuda Na Hasidi

Husuda ni tabia za watu wengi, isipokuwa wale waliohifadhiwa na Mwenyezi Mungu, na wala haiko kwa washirikina, Mayahudi au Manaswara peke yao, bali iko pia kwa Waislamu wengi; hata kwa wanavyuoni wakubwa na baadhi ya wale wenye vyeo vya kuwa Marja (Mufti mkubwa) wa kidini ingawaje cheo hicho ndicho pekee kinachokurubiana na cheo cha maasum.”

Mwenyezi Mungu, Mitume Maimamu na wenye hekima, wamezungumzia sana kuhusu hasadi. Miongoni mwa hayo ni kauli ya Imam Jafar Sadiq: “Hasadi asili yake ni upofu wa moyo na kukana fadhila za Mwenyezi Mungu, na hayo yote mawili ni mbawa za kufuru.” Lugha fasaha zaidi niliyoiona katika kuisifu hasadi ni kauli ya bwana wa mafasaha na kiongozi wa wenye hekima, Amirul Muminin (a.s.) alipowaeleza kuwa ni mahasidi wa raha na wenye kutilia mkazo balaa. Akasema tena: “Inatosha kuwa ni shari kwa mahasidi kuhuzunika wakati unapofurahi.”

Huenda itakuwa ni vizuri kunakili mfano huu kutoka kwa mwanahekima mmoja aliyesema: “Mfano wa hasidi ni kama mtu anayetupa jiwe kwa adui yake, kisha jiwe limrudie mwenyewe upande wa kuume na apandwe na hasira. Mara ya pilitena analitupa kwa nguvu kuliko kwanza, na limrudie upande wa kushoto na hapo ataingiwa na chuki na kisha alitupe jiwe kwa nguvu zote na hamasa halafu limrudie kichwani na limjeruhi na huku adui yake yuko salama.”

Ni muhali kwa hasidi kuweza kutubu husuda yake, kwa sababu hasidi ni sawa na mwoga na bakhili. Atawezaje bakhili na mwoga kutubu? Ndio maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume kuwaambia mahasidi.

قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗ{119}

...Sema; kufeni na ghadhabu zenu.” (3:119)

مَا نَنْسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنْسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {106}

Aya yoyote tunayoifuta au kuisahaulisha tunaleta iliyo boro kuliko hiyo au iliyo mfano wake. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu?

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ {107}

Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni mfalme wa mingu na ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi asiyekuwa Mwenyezi Mungu.