Aya 74: Kuwa Ngumu Nyoyo
Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo.
Yaani ilikuwa ni wajibu kwa wazee wenu - enyi Mayahudi wa Madina - wazingatie na zilainike nyoyo zao baada ya kushuhudia waliyoyashuhudia katika miujiza na maajabu; ambayo miongoni mwake ni kufufua aliyeuliwa, lakini, kwa ukhabithi wao, wakafanya kinyume na vile inavyotakiwa; wakafanya ufisadi na nyoyo zao zikasusuwaa kama kwamba zimetokana na mawe, bali baadhi yake ni ngumu zaidi kuliko mawe, kwani kuna mawe, mengine yanayobubujika mito ndani yake, na kuna mengine yanayopasuka yakatoa maji.
Unaweza kuuliza: Mito ni maji, sasa mbona yametajwa maji na mito? Inawezekana kutofautisha jengo na nyumba?
Jibu: Hakika Aya tukufu imegawanya maji kwenye mafungu mawili mengi ambayo ni mto, na machache ambayo ni chemchem. Ibara ya mgawanyiko imekuja kwa tamko la maji, kwa hivyo kumetajwa kububujika maji kwa maana ya wingi na kupasuka kwa maana ya uchache.
Vyovyote iwavyo, lengo la Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwa amefadhilisha aina za majabali na mawe kuliko nyoyo za Mayahudi, ni kwa sababu jiwe linaweza kupasuka likatoa maji, na kwamba jiwe mara nyingine huwa linatikisika likaondoka pale lilipokuwa.
Lakini nyoyo za Mayahudi hazina hata chembe ya kheri wala hazitikiswi na uzuri wowote na hazielekei kwenye uongofu.
Unaweza kuuliza kuwa mawe hayana uhai wala utambuzi, kwa hiyo hayawezi kumwogopa Mwenyezi Mungu, sasa kuna wajihi gani katika kauliyakeMwenyeziMungu:“Nakunamenginehuangukakwasababuya kumwogopa MwenyeziMungu.”
Swali hilo limejibiwa kwa majibu mengi, yaliyo karibu zaidi ni mawili: Kwanza, hayo ni makisio kwamba lau kama mawe yangelikuwa na fahamu na akili kama Mayahudi, yangelianguka kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu. Mifano hii ni mingi sana katika maneno ya waarabu.
Jibu jingine, ni kwamba ni kawaida ya mawe kumnyenyekea Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyeumbamaumbileyote.
Mwenyezi Mungu anasema: “Zinamsabihi (zinamtakasa) mbingu zote saba na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, na hakuna chochote ila kinamsabihi kwa sifa Zake njema.” (17:44)
Utakuja ufafuanuzi tutakapofika Aya hiyo inshallah.
Tofauti Ya Hulka
Anaweza kuuliza muulizaji: Je ndani ya binadamu kuna nguvu inayompa msukumo wa harakati; au yanayompa harakati ni matukio ya nje, kiasi ambacho ndani ni tawi lakini nje ndio shina? Au kila moja ni shina hiyo yenyewe peke yake, kwamba mtu mara nyingine hupata msukumo kutoka ndani na mara nyingine nje au mara nyingine ndani na nje? Kama tutafaradhia kuwa ndani ya binadamu kuna msukumo wa aina ya peke yake usioshirikiana na kitu kingine, Je msukumo huo ni wa aina moja kwa watu wote au kila mtu ana wa aina yake?
Jibu: Hakika mtu anakuwa mtu kwa silika yake na nguvu yake ya kiroho. Lau tunavitoa vitu hivyo au tanavizuia utendaji kazi wake, basi binadamu atakuwa ni kama ganda tupu au unyoya katika mavumo ya upepo.
Ndio! Ni kweli kwamba nguvu za kindani zinafanya kazi pamoja na matukio ya nje na kuathirika nazo, lakini kufanya kazi ni kitu kingine na kuathirika ni kitu kingine. Kwa mfano, silika ya kuchunguza inakuwa pamoja na mtu na ndio maana mtoto anakuwa mdadisi kwa umbile lake; bali silika hiyo ni katika mambo yanayomuhusu mtu.
Kisha silika hii inakua na kukoma kwa kuona matukio ya nje vilevile kwa utafiti na uvumbuzi; na kwa kukua kwake binadamu anaweza kuathirika vitu vya nje kulingana na haja yake na matakwa yake. Kwa hivyo harakati za binadamu zinachimbuka kutoka ndani na nje, yaani kutoka katika nafsi yake na kutoka katika matukio.
Hapa kuna kifungu cha tatu ambacho nimekigundua kutokana na majaribio yangu maalum; Kifungu hicho nimekipa jina “Tawfik katika heri na kufaulu”. Kifungu hiki hakitokani na nafsi wala matukio, bali kinatokana na nguvu iliyojificha ambayo iko katika ulimwengu uliojificha (usiojulikana), inawaandalia baadhi ya watu njia ya heri na inaingia katika kuwaelekeza watu kwenye lile linalomridhshia Mwenyezi Mungu bila ya mtu kutambua.
Ni kawaida kwamba hatanikubalia juu ya hili isipokuwa yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na hekima yake na kumpa cheo kinachomstahiki. Ninakiri kwamba mimi sina ufahamu wa ujumla wa kifungu hiki, isipokuwa nimekifahamu kutokana na majaribio yangu; kama nilivyotangulia kueleza.1
Ama jawabu la kuwa je, watu wanakuwa na namna moja katika silika na sifa za kinafsi, linataka ufafanuzi. Katika sifa za kinafsi kuna zile ambazo watu wanashir-ikiana; kama vile utambuzi wa kupambanua kati ya haki na batili, heri na shari, na kati ya baya na zuri.
Lau si ushirikiano huu isingeliwezekana kwa vyovyote vile kuthibitisha uovu na wema na isingelifaa kwetu kumlaumu au kumsifu mtu kwa kufanya jambo fulani. Vile vile kuna ushirikiano katika kujipenda na upendo wa mzazi na mwana, na mengineyo ambayo wanayo watu wote, ijapokuwa kuna tofauti ya wingi na uchache.
Kuna sifa nyingine za kinafsi, ambazo watu wanatofuatiana kama vile; ushujaa, woga, ukarimu, ubahili, ugumu wa moyo, ulaini wa moyo, udhaifu wa matakwa na nguvu yake na kupondokea kwenye heri au shari. Watu katika sifa hizi wanatofuatiana, kila mtu sio karimu au bahili, wala mwoga au mshari.
Unaweza kuuliza: Hakika kauli yako si inakhalifu kawaida maarufu iliyozoeleka, kuwa hakuna mtu yoyote isipokuwa ana pande mbili, mzuri na usiokuwa mzuri; na wewe umetilia mkazo upande mmoja tu, na ukaufinyia jicho upande mwingine?.
Jibu: Hakika uvivio wa heri ambao mara nyengine tunauona kwa baadhi ya watu wa shari, unakuwa umeingia kighafla tu, bila ya kukusudiwa; na kwamba suala la kuwa kila mtu ana pande mbili linawezekana kwa wasiokuwa Mayahudi. Kwa sababu, Mayahudi hawana lolote wao isipokuwa uovu tu; hawana wema kabisa. Ushahidi wa hayo ni Tawrat yao, Qur’an tukufu na historia sahihi.
Vile vile vitendo vyao katika Palestina na kwingineko, mambo ambayo ni dalili wazi kwamba dini, maadili na mfungamano wote wa kiutu, kwao ni biashara na manufaa tu. Maudhui haya tutayarudia kila itakapolazimika.
أَفَتَطْمَعُونَ أَنْ يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِنْ بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ {75}
- 1. Jambo la kushangaza lilotokea kwa sadfa.Baada ya kuandika maneno haya nikasoma nakala fulani, kuwa kiongozi mmoja wa kijeshi wa Kiingereza maarufu sana anayeitwa Montgomery alijieleza kwa kusema: Hakika yeye ni askari mdogo chini ya uongozi wa nguvu kuu; na kwamba yeye hakushinda katika vita isipokuwa kwa matakwa ya kudra hiyo; na kwamba bila ya kuamini nguvu hii kubwa yenye akili, haiwezekani kushinda katika vita vya dunia vya pili. Yeye anaamini kwamba kuna nguvu iliyofichika ambayo iliwaandalia njia ya kumshinda Romel, ambaye alikuwa akiitwa mbweha wa jangwani, naye alikuwa amirijeshi mkubwa wakati huo.